Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

mzee umenikumbusha mbali sana kipindi tunazamia Complex tunapitia mliman ukifika pale juu kuna mmasai unampatia mia 300 unazama ndani
 
mzee umenikumbusha mbali sana kipindi tunazamia Complex tunapitia mliman ukifika pale juu kuna mmasai unampatia mia 300 unazama ndani

[emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] complex watoto wa kamnyonge walipenda kucheza na kukaa maeneo ya spika kila walijuana na yule Dj lima
 
Hatari sana mimi nimkulia Mwisenge katika maeneo ya kwa Geofrey yule mfuga ngombe hali ilikua mbaya saana mpaka mzee akanipeleka Boading Arusha kisa tuu nisiingie katika makundi Mbaya namkumbuka sana kuna mshikaji alikua katika kundi la Jamaica Moko pale majita road alikua anaitwa Kabadi jamaa alikua mtata sana
kabadi mkubwa ama mdogo kama ni mkubwa saiv ni boda na ni mstarabu sana huyo mdogo nae saiv yupo mwanza
 
Back to 1980's Tycoon Musoma walikuwa Panju na Ibrahim Kassam (Waasia) akimiliki kiwanda cha soda za VIMTO hapo Musoma maeneo ya Shule Pendwa Musoma Tech. Sina hakika kama kiwanda cha Vimto bado kipo huko Musoma, ingawa kwa sasa AZAM kachukua hilo jina na kuzipachika Juice zake VIMTO.
Yawezekana tulikuwa wote miaka hiyo.Hata jina lilikuwa Musoma Sec. tu,mambo ya Tech. yalikuja nishasepa 1991! Nyani,Baba,Chomoa,Bonge(Seleli) na jamaa wa kilimo alikuwa anajiita"jack of all but master of none" n.k. Maisha yanaenda mbio sana aisee!
 
Alikuwa anaitwa Mutalagala kama sijakosea alifariki 2007 nyumbani kwake nasikia walikuwa wakiweka vibao kama kapumzika, au hayupo, n.k
Hakuwa tajiri bali alikuwa mwenyekiti wa ccm! Alikuwa kimbau mbau fulani hivi.Umaarufu wake ulichagizwa na vibao kubandikwa mlangoni kuonyesha 'YUKO MKUTANONI,YUKO SAFARI,KALALA,BAFUNI,N.K" Bila kusahau kiswahili chake!
 
Nakumbuka enzi hizo kwenda Disco Toto Tembo Beach kila sikukuu za Mwisho wa mwaka, Wasanii wakija Karume Stadium tunasubiria mda wa fungulia mbwa ndipo tuingie wakati kiingilio ni 1000 tu watoto.

Watu maarufu kama Tajiri mwenye mbwembwe Nyakiteri, Dereva wa mbio za magari Mama's, Hussein Sokoni, Redio yetu pendwa Victoria FM hapo utawakuta wakina Boke Wambura, Maregesi Girishon, Emmanuel Chibasa, Issa Nundu, mzee wa Mafua Robson Wangaso na wengineo, mitaa ya Nyasho hapo ndilo chimbo la kujipatia mavazi.

Fujo za Musoma Tech na Songe hadi kupelekea Songe kuwa ya wadada, Mitaa maarufu kama Mukendo, Iringo, Mwigobelo, Majita Road bila kusahau vibaka wa Magamaga, na kila likizo tunakutana tuition Mwembeni hapo utakutana na watoto wa Isenye, Ikizu na sisi wa Bweri Makatani.

Umemaliza bweri makatani mwaka gani?
Maana mimi nimemaliza apo 2010
 
Mass town mwaka 2005 yalianzishwa makundi ya vijana kwa ajili ya kampeni za siasa vijana wapige kura kuanzia miaka 18 mpaka 30 muasisi akiwa mgombea ubunge ccm. Baada ya kampeni kuisha tu hilo kundi la WEST LAWAMA likageuka na kua kundi la wahuni wavuta bangi vibaka na waanzisha fujo musoma.mjini.ilipofika mwaka 2007 yaliibuka makundi ya vijana mengi sana karibia kila kata inakundi lake la kufanyiana fujo na makundi ya mitaa mingine:

1. USWAZI kata ya kamyonge mpaka mkendo, iringo
2. MBIO ZA VIJITI kata ya nyakoto na kigera
3. MDOMO WA FURU kata ya nyamatare
4. WABEPARI kata ya mwisenge

Ilifika kipindi wakawa musoma nzima wanafunzi wengi wako kwenye makundi ya uhuni. Siku za sikukuu hasahasa complex na tembo beach lazima mzike uzimwe mapema kisa fujo za haya makundi hasimu MBIO NA USWAZI . Tulishudia mapanga live kama picha za wahindi. Ilifika kipindi wakawa wanafungiana maeneo ya kutembea kama vile nyasho ikotokea umekutana nao we kimbua tu utapigwa lugoe.

Kuna vijana walikua maarufu sana enzi hizo kwa ubabe na uhuni kama vile Kasinia na wengine wengi nishawasahau.

Umeongea vzr ila naisi makundi makubwa apo yalikua ni MBIO ZAVIJIYI na JAMAICA Mokazi nina historia ndefu ya jamaa yangu alieachwa kilema na aya makundi visa vya wanafunzi wa kike kutekwa na kufanyiwa ubakaji na hawa jamaa, wizi wa kunyanga’nya na kudhulu, kuna mtu amefaliki alikua nihatari anaitwa MUGASA
 
Mgasa, Kinche, Bonny Weed, Ally Bega, Duchu, Maromaro (R.I.P). List ni ndefu sana kwa wanangu wa Jamaica Mockers.

Mbio za vijiti unakutana na akina Jigga, Jira, Chui, Mapacha (jamaica pia walikua na mapacha).

Huku West Lawama unakutana na wakongwe akina Majani.

Yale maisha yamefanya tukawa tough sana. Kusurvive katikati ya gangs kama zile inahitaji roho ngumu. Bahati nzuri nilikua muhuni mpenda shule, hiyo ndio ponapona yangu. Othrerwise ningekua either jela au kaburini.

Unamjua mpka Ally bega we nzee ni hatari sana uyu jamaa katika kundi zima ndio alikua msela wangu sijui yuko wapi asee
 
Back
Top Bottom