Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Hapa unaongelea kina kibundari, Nature, kina mako chali, maromaro ( marehemu), walikua wengi sana asee watoto wa nyasho, marehemu Sefu
Dah, mwanangu Mako Chali sijui yuko wapi siku hizi! Sefu unaemuongelea ni yupi? Au ni yule aliekula mzinga na pikipiki Majita road?
 
Sehemu bora kabisa musoma kuwahi kutokea ilikuwa diocese ya musoma( kituo cha matumaini ya vijana).

Kilikuwa kituo bora cha michezo na masomo, vyote vilitolewa bure kabisa kilikuwa kisima cha maarifa, kituo hiki cha kanisa romani cathoric baada tu ya kufungwa ndipo yalipoanza kuibuka makundi ya uharifu na wahuni

Pale ilikuwepo michezo ya aina zote unayoifahamu wewe, maktaba na madarasa ya kufundishia fani mbalimbali ikiwemo uchoraji n.k

Vijana na watu wote walikuwa wanakutana pale kushiriki michezo na masomo hivyo hapakuwa na makundi ya kihuni, zilikuwepo timu za mipira na michezo mingine pamoja na wasomi.

Sijaona kikiongelewa humu mkumbuke na mazuri, msikumbushane matukio ya wahuni tu.

Nimeuzuria sana apo mzee since niko na 8 yrz mpk 17
 
Dah, mwanangu Mako Chali sijui yuko wapi siku hizi! Sefu unaemuongelea ni yupi? Au ni yule aliekula mzinga na pikipiki Majita road?

Yah SEFU alikula mzinga wa pikipiki mimi nimekulia sana maeneo ya mkendo kubwa , makongoro na iringo ndio viwanja vyangu
 
Nakumbuka Club Metropole kama sijakosea mtaa wa Mkendo kati pale nilicheza disco enzi hizo za 2000s km kawaida ya Mapoti Muziki hauishi bila ya Ugomvi!
 
Huu Uzi umenimalizia ubuyu wangu wa laki mbili
IMG_20201025_221424.jpg
 
Nilikua huko last year, Rwamlimivis one of the best well built streets kwa sasa pale musoma. Bado hawajapata lami tu. Pamejengeka sana, pamejaa sana. Pia uwanja wa mpira unajengwa kule, karume panavunjwa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege!

musoma mjini kulijengwa vizuri sana
 
Naona watu wanaijua musoma Sana ila kiukweli kwa sas ni sehemu salama nimeona mnawajua mapacha wa jamaika mockers hii ni kweli jamaa walikuwa watata Sana waliwahi mfata demu primary shule ya musoma wakampiga mabapa ya sime kisa kawakataa ninayo mengi ila karibuni musoma maisha mepesi Sana huku
 
unaishi sehemu gani
 
Nakumbuka Club Metropole kama sijakosea mtaa wa Mkendo kati pale nilicheza disco enzi hizo za 2000s km kawaida ya Mapoti Muziki hauishi bila ya Ugomvi!
Aisee hapo niliwahi gombana nje

Kisa kilikuwa nimeenda na mamanzi wawili halaf machalii wawili wanata eti wateke wee thubutuu ndio nilikuwa nimeiva kwenye Tae kwon do niliwaoshea kinoma aisee maboda wote walio kuwa pale waliniona kama vandame, mmoja nilimuacha amezimia na Mwingine alipanda piki piki akakimbia kinoma na nakamfata na piki piki langu huku maboda nyuma kama 25 wanafuatilia tukio kama sinema ya kihindi vile ni bahati sikumshika nikarudi nikachukua mamanzi wangu nikarudi tena ndani hiyo space 2000 hatari sana aisee,

Na wakati fulani Jamaica wananiwinda kinoma aisee...
 
Back
Top Bottom