Sehemu bora kabisa musoma kuwahi kutokea ilikuwa diocese ya musoma( kituo cha matumaini ya vijana).
Kilikuwa kituo bora cha michezo na masomo, vyote vilitolewa bure kabisa kilikuwa kisima cha maarifa, kituo hiki cha kanisa romani cathoric baada tu ya kufungwa ndipo yalipoanza kuibuka makundi ya uharifu na wahuni
Pale ilikuwepo michezo ya aina zote unayoifahamu wewe, maktaba na madarasa ya kufundishia fani mbalimbali ikiwemo uchoraji n.k
Vijana na watu wote walikuwa wanakutana pale kushiriki michezo na masomo hivyo hapakuwa na makundi ya kihuni, zilikuwepo timu za mipira na michezo mingine pamoja na wasomi.
Sijaona kikiongelewa humu mkumbuke na mazuri, msikumbushane matukio ya wahuni tu.