denis fourplux
JF-Expert Member
- Aug 17, 2017
- 1,049
- 1,385
Musoma wajuaji wengi ila wajanja wa maisha wachache, nimekaa musoma miaka kadhaa na Tarime pia, kwa miji ya Mara bora Tarime kuna aina fulani ya maisha kwa mtu mwenye kuitaji kutoka wajita wa musoma maneno mengi sana..
Kuna mmoja niliwai kumtoa jino katika gym ya pale pembeni ya uwanja wa karume.. nilikuwa mgeni kule ila kwa sababu napenda mazoezi nikaulizia nikaelekezwa mahala pa gym.. nimefika siku ya kwanza, pili ya tatu jamaa akaanza kuwa anafuatilia maisha yangu... alifikiri siwezi mfanya kitu nilimpa ngumi moja jino likadondoka mpk leo sitasahau hakuna aliyethubutu kunisogelea maana inaelekea yeye ndo alikuwa nunda pale.
Nilikaa miaka 2 hivi nikahamishwa kikazi. Ila wasichana tu wa kule mwanaume unatongozwa kabisa kulikuwa na hotel moja hivi kubwa tu ipo pembezoni mwa ziwa nimeishau jina, nimekula sana samaki pale na pombe sana. Matajiri wa pale ni akina matayo, hussein sokoni, ila wana maisha ya kishamba sana aise. Mitaa naikumbuka kamyonge, umoja, makoko nk, jamaa, zangu walikuwa huyu aliyegombea ubunge, akina Bailes na wengine nimewasahau. Ila sijawai kutamani kurudi kule.
Mkuu unaongelea bailesi wa mtaa wa makongoro pale kwenye kona.
Na apo pembeni ya karume palikua panaitwa Dayosisi kituo cha matumain michezo kama yote