Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Mara ya mwisho kuonana nae ilikua ni Kitunda (Dar), alikua analima bustani ya mchicha. Nadhani ilikua 2016_ wakati huo Jack Pongo kaokoka hahaa. Hakuna marefu yasiyo na ncha!
Duchu alikua ananionea sana aisee kwa kisingizio cha baba angu kumwonea sana kipindi anasoma (baba angu alikua ni mwalimu mwisenge primary ) sasa kuna cku alinifukuza kutokea bwalo la police mpk makoko darajani ndo akanishika na kunichana na kiwembe mbavuni enzi hizo niko darasa la saba cku sita isahau asee ila baadae tulikuja kuwa marafiki wakubwa tu mpk alivyoingia jamaica mokers rasmi.
 
Huwa nikikaa na watu wa Arusha alafu wakaanza kuongelea ubabe wa huko kwao, huwa naishia kucheka tu. Musoma ilikua ni vita kamili.

Anyway, ulikua unateseka ukiwa maeneo gani hahaa?
Ni wachumba tu bado maana, kuhusu kundi kwa kundi kuuliana mtu ni swala la kawaida kabisa aisee ilikuwa noma, nimeweka sime mno kwenye modo au pemben ya mguu, aisee mpaka now nina harama ya mwana haramu mmoja ila nilichomtenda hatosahau nafikiri kila sehemu akifika anailizwa ulikuwaje...!?
 
Mie musoma nimeenda mara 2 tu, Ila sjawahi na stopapenda...Mji mbaya mno
 
Sehemu yenye vijana washamba na magrup yao ya kishamba kishamba .aani hawa vijana wa musoma wao wanaona mabifu ndiyo ujanja machoko sana
 
Daah kweli kabisa mkuu, na kuna kundi lilitwa Jamaica Mockers.
 
You're the best,buddie..
 
Musoma wajuaji wengi ila wajanja wa maisha wachache, nimekaa musoma miaka kadhaa na Tarime pia, kwa miji ya Mara bora Tarime kuna aina fulani ya maisha kwa mtu mwenye kuitaji kutoka wajita wa musoma maneno mengi sana..

Kuna mmoja niliwai kumtoa jino katika gym ya pale pembeni ya uwanja wa karume.. nilikuwa mgeni kule ila kwa sababu napenda mazoezi nikaulizia nikaelekezwa mahala pa gym.. nimefika siku ya kwanza, pili ya tatu jamaa akaanza kuwa anafuatilia maisha yangu... alifikiri siwezi mfanya kitu nilimpa ngumi moja jino likadondoka mpk leo sitasahau hakuna aliyethubutu kunisogelea maana inaelekea yeye ndo alikuwa nunda pale.

Nilikaa miaka 2 hivi nikahamishwa kikazi. Ila wasichana tu wa kule mwanaume unatongozwa kabisa kulikuwa na hotel moja hivi kubwa tu ipo pembezoni mwa ziwa nimeishau jina, nimekula sana samaki pale na pombe sana. Matajiri wa pale ni akina matayo, hussein sokoni, ila wana maisha ya kishamba sana aise. Mitaa naikumbuka kamyonge, umoja, makoko nk, jamaa, zangu walikuwa huyu aliyegombea ubunge, akina Bailes na wengine nimewasahau. Ila sijawai kutamani kurudi kule.
 
Hii thread imenikumbusha mbali nimewakumbuka marafik zangu..

ila sitamani kuja kuishi tena Musoma
 
Wanaotaman kuish kule ni watu wa hukohuko Kuna kaz niliwahi kuipiga chin kwasababu tu napachukia huko
 
Hivi kipindi hiki Esther Bulaya alikuwa kishazaliwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…