Labda nikujuze kitu kimoja, ukifanya maamuzi ya pupa kwenye masuala ya mirathi inaleta shida kubwa, hilo la kwanza, la pili mimi sio mwanasheria sijui chochote kuhusu mambo ya mirathi na kwa sababu hiyo ndo maana wakawepo wanasheria. La nyongeza, binti yetu huyu elimu aliyonayo ni ndogo sana ukilinganisha na elimu yangu na ya mdogo wangu, na kuwa na elimu kubwa haimaanishi ndo kujua sheria, ndo maana unakuta mtu ni profesa lakini anakwambia ana mwanasheria wake. Nimeleta huu uzi kwa watu waliobobea kwenye masuala haya nipate moja mbili za kisheria. Maamuzi ya mihemko sio mazuri