Watu wakimya (introverts) mnapataje marafiki wa kawaida ukubwani?

Watu wakimya (introverts) mnapataje marafiki wa kawaida ukubwani?

Wanashindwa kutofautisha kuishi na watu vizuri na kujichanganya na watu,
Mimi hii nyumba ninayoishi sikuwahi kugombana na mtu, naishi nao vizuri tu ndo maana wanajitahidi kuweka ukaribu na mimi au kujenga mazoea na mimi sema mtu mwenyewe sasa nikitoka kwenda kazini na jioni nikirudi ndani, ila mtu akiniuliza jambo namjibu vizuri tu, akiwa na shida namsikiliza kisha nafanya mambo yangu

Kifupi huwa naishi nao vizuri inafikia kipindi vibinti vya humu ndani vinajaribu kunizoea lakini wapi sizoeleki
Huyu ndio introvert sasa

Mkuu huyu ndio mimi
 
Nadhani pia introverts wengi tunaroho nyepesi as ni rahisi kuumizwa, so kuavoid maumivu ya kila siku unaamua kujiweka pembeni

Pia hatupendi drama [emoji1787]

Ila ukibahatika kupata introvert friend ni kama umeokota dodo[emoji3][emoji38] tuko peace na very social katika small limited circle [emoji817]

Haya introverts tujuane tuanze kubond tuache kukaa counter wenyewe[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Umenena nilivyo

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Hulka moja wapo ya watu wakimya (introverts) ni ugumu wa kujichanganya na kuzoeana na watu wapya. Hii inapelekea wengi wanajikuta hawana marafiki ukitoa watu wachache wale waliofahamiana wakati wa chuo/sekondari, biashara/kazini. Siku zinavyosonga na wanavyozidi kukukua kimaisha "cycle" ya marafiki alionao inazidi kupungua. Anabakiwa na zaidi familia tu na rafiki mmoja au wawili.

Anajikuta imefika weekend mtu anatamani kujiachia kidogo na kubadili mawazo ila akiangalia hana watu wa kujumuika nao. Akiingia bar/mgahawa anakuta majamaa wamekaa kwenye meza kwa vikundi, inabidi aidha akae meza yake mwenyewe au akae counter...lakini anakosa ile ladha ya urafiki na uhusiano walionayo wengine kwenye maisha ambapo hubadilishana mawazo na kupeana changamoto chanya za kimaisha.

Kwa upande mwingine wanakuwa ni watu wanaojitegemea (independent) kifikra na kwa mambo mengi hufanya maamuzi na kuendesha maisha bila kutegemea ushauri au mawazo ya wengine. Pia kutokana na kutokuwa na watu wengi huwa hawana zile drama/changamoto za marafiki.

Faida za marafiki ni nyingi kuliko hasara, hebu introverts toeni mbinu za kupata marafiki wapya ukubwani.
Upweke ndo utaniua hii hali inagoma kabisa kunitoka[emoji24]

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Upweke mbaya sana sijui hii hali nitaishinda vipi nikitaka kuzieana na mtu naona kama ataniona nina shobo kwake na kiherehere naamua kumpotezea I'm too judgemental na nina reach conclusion kichwani kabla sijafanya kitu
 
Nimetoka kupata dawa za Impiramine kwenye hospitali moja kubwa hapa DSM.

Sielewi ni Introvert au ni nini. Nina loneliness moja ya kufa hata kufanya majukumu yangu sitaki kabisa. I hope it won't get worse.

I don't want to be an Introvert. It hurts.
 
Usitumie dawa mkuu zitakufanya uwe tegemezi kwazo
 
Hulka moja wapo ya watu wakimya (introverts) ni ugumu wa kujichanganya na kuzoeana na watu wapya. Hii inapelekea wengi wanajikuta hawana marafiki ukitoa watu wachache wale waliofahamiana wakati wa chuo/sekondari, biashara/kazini. Siku zinavyosonga na wanavyozidi kukukua kimaisha "cycle" ya marafiki alionao inazidi kupungua. Anabakiwa na zaidi familia tu na rafiki mmoja au wawili.

Anajikuta imefika weekend mtu anatamani kujiachia kidogo na kubadili mawazo ila akiangalia hana watu wa kujumuika nao. Akiingia bar/mgahawa anakuta majamaa wamekaa kwenye meza kwa vikundi, inabidi aidha akae meza yake mwenyewe au akae counter...lakini anakosa ile ladha ya urafiki na uhusiano walionayo wengine kwenye maisha ambapo hubadilishana mawazo na kupeana changamoto chanya za kimaisha.

Kwa upande mwingine wanakuwa ni watu wanaojitegemea (independent) kifikra na kwa mambo mengi hufanya maamuzi na kuendesha maisha bila kutegemea ushauri au mawazo ya wengine. Pia kutokana na kutokuwa na watu wengi huwa hawana zile drama/changamoto za marafiki.

Faida za marafiki ni nyingi kuliko hasara, hebu introverts toeni mbinu za kupata marafiki wapya ukubwani.
Huu Uzi umenigusa sana , mkuu umeongea kana kwamba nimekueleza maisha yangu ukayaandika JF.Sasa nimejua Mimi ni introvert, tena kwelikweli. Mtihani zaidi ni kutongoza
 
Nimetoka kupata dawa za Impiramine kwenye hospitali moja kubwa hapa DSM.

Sielewi ni Introvert au ni nini. Nina loneliness moja ya kufa hata kufanya majukumu yangu sitaki kabisa. I hope it won't get worse.

I don't want to be an Introvert. It hurts.
Time heal.....upweke ndio tatizo letu kubwa sana,mimi binafsi nakutana na hiyo hali sana hasa wakati wa wikiend kama nikiwa niko mbali na familia
 
kama wewe ni introvert hauwezi kusumbuliwa na mawazo ya kuwa mpweke binafsi napenda sana kufanya mambo yangu mwenyewe lakini sina aibu wala uoga wa kuishi na watu tena kuna muda mimi ndio huwa naitwa nichangamshe genge la story , nikitoka hapo mazoea na urafiki wetu unabaki hapo hapo wachache sana kwenye hilo kundi wanaweza kufahamiana na mimi zaidi, sio kwamba nawabagua bali wengi hushindwa kuendana na namna ninavyoishi sina maisha ya kuishi kubembeleza kuzoeana au kuishi kinafiki, kuna wajamaa niliishi nao miaka 4 sijawai kiongozana nao zaidi ya salamu na mimi kusepa hawa jamaa walikuwa wanajishitukia wakiwa na mimi wanavaa hovyo nikiwa nao wanaanza kukuita boss mara punguza kidogo kupendeza , mbona unashindia nguo za kanisani , nikasema moyoni nyinyi mbona mimi sioni aibu kwamba nyinyi mnaishi lafu lakini nyinyi mnapenda kufuatilia mambo yangu na kujishitukia nikawafungia vioo kabisa.

aah you’re that guy in high school/ college
 
Daah kuna mshkaji alikua na tabia hizo za kikuda kuda (Mood swings) mara aongee, kesho anune aisee nilimchana nikamwambia sitakagi mazoea kabisa na washkaji wenye Hizi tabia za kama vile demu aliyeko period.

wengine wagonjwa inabid ufahamu hilo (bipolar)
 
People kuna tofaut kat ya kuwa social anxious, na kuwa introvert
Kuna aina ya introvert ambao ni anxous introvert,ambao wao ni vigumu sana kusocialize,wapo ambao wanaweza kusocialize kwa kiasi fulani ambao wapo kwenye kundi la social introvert,mimi binafsi najiona kwenye kundi la restrained introvert
 
Upweke mbaya sana sijui hii hali nitaishinda vipi nikitaka kuzieana na mtu naona kama ataniona nina shobo kwake na kiherehere naamua kumpotezea I'm too judgemental na nina reach conclusion kichwani kabla sijafanya kitu

Hii kitu nili experience unajua tatizo ni nini! Hapo kila mtu anabalance shobo hata huyo unaetaka kuongea nae utakuta na yeye anataka kuongea na wewe ila anaona kama atashoboka.

Chamsingi wewe anza utaona atakavyokupokea kwa shangwe, nimefanya hivyo siku hiz naongea na watu kibao, kudhani kuwa watakuona una shobo.. it’s all in your head mkuu sio kweli, tena utapewa sifa ya “fulan mcheshi lazima akusalimie” ... hivyo Yaani
 
Ni muhimu kujua haya mambo ya "personality" unakuta baadhi ya wazazi wasiojua mambo ya "introvert vs extrovert" wanaishia kuwakaripia baadhi ya watoto....

"hebu changamka wewe mbona umezubaa zubaa tu huchezi na wenzako kama fulani"

.....bila kujua pengine ni introvert na hawezi kabisa kuwa na "social interaction" hasa kwa watu ambao ni wapya na hawajazoea.

Introvert = draw energy from within themselves
Extrovert = draw energy from each other.
 
Back
Top Bottom