Watu wakimya (introverts) mnapataje marafiki wa kawaida ukubwani?

Watu wakimya (introverts) mnapataje marafiki wa kawaida ukubwani?

Hii hali inanitesa sana tena sana kwenye nyumba tumepanga 9 ila sina namba ya hata 1 na nina mwaka mimi nilikua na marafiki 2 mmoja akanisaliti moja bado yupo tena mbali marafiki wangu ni sim na redio tv nilirudisha kwenye box maana niliona haina kazi kwangu yani mtu mwenye uwezo wa kituelewa watu kama sisi ni wachache sana. Duh natamani nikacheze bao lakini najikuta hata kuchangia siwez nikienda kwenye mpira nakua bubu nikienda sehemu kupata kinywaji nikikuta pana watu wengi hamna sehemu yakukaa peke yangu naondoka atakama nitapewa ofa nitaikataa kisiasa napenda kua peke yangu yani mm nizaidi na zaidi
Wewe ni muoga na hujiamini. Sio introvert!
 
Sio unajiona upo sawa, sema TUPO SAWA, mbona tunaishi fresh tu hatumkeri mtu,
Tena mimi nipo sawa tu, huwa sipendi tabia ya kubabaikia mtu, ishu zangu zote huwa nazimalizaga mwenyewe kibingwa tu
Kuna wapuuzi utasikia... "Siku ukipata tatizo watu watakuangalia tu kwa kuwa huna mazoea nao...", anasahau kuwa mwenye akili timamu na muungwana hahitaji umzoee au ujipendekeze kwake ili akupe msaada. Hao watu wa mpaka sijui akujue, mara mzoeane ndipo atoe msaada huwa washenzi tu kama washenzi wengine.
 
Siku zote huwa nakaa Mbali na Watu wanaoongea sana..!
Na wale wanaotaka kunizoea kwa haraka!

Nina Marafiki 2 tu....! Lakini rafiki zangu hao sio introverts!

Binafsi hata kuwa na Demu mpaka nitengeneze Urafiki kwanza...!!!

Napenda kujitegemea kifikra, kiuchumi na kila kitu!
Naweza kusema na Moyo wangu nikatatua matatizo ndani yangu!!!
 
Wanashindwa kutofautisha kuishi na watu vizuri na kujichanganya na watu,
Mimi hii nyumba ninayoishi sikuwahi kugombana na mtu, naishi nao vizuri tu ndo maana wanajitahidi kuweka ukaribu na mimi au kujenga mazoea na mimi sema mtu mwenyewe sasa nikitoka kwenda kazini na jioni nikirudi ndani, ila mtu akiniuliza jambo namjibu vizuri tu, akiwa na shida namsikiliza kisha nafanya mambo yangu

Kifupi huwa naishi nao vizuri inafikia kipindi vibinti vya humu ndani vinajaribu kunizoea lakini wapi sizoeleki
 
Ndiyo hao ukisikia issue zao za mademu unakataa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sasa mbona unatunanga mkuu?

Anyway mi watu wananishangaa tu mademu wanaowahofia wao mi ndo naruka nao
Siku kuna jamaa maeneo ya kazini aliniuliza kuhusu kuoa nikamjibu nitaoa akanikatalia akasema maliza ujana kwanza maana macho yako hayajatulia, nikakaa kimya
 
Unaendeleza ukorofi. Natural death - leukemia.
Naomba usichoke Mwalimu. Na mbona kuna tetesi kuwa ulipewa zawadi ya wine siku ya b/day party yako ambayo ilikuwa imepandikizwa leukemia, na ndio ambayo ilikuua? Tuweke wazi tafadhali.
 
Toka nizaliwe sijawahi kuwa na rafiki hata mmoja,na nafurahia maisha bila tabu yoyote.Napenda wakati wowote niwe peke yangu bila kelele.Naona kujichanganya na watu ni kujitafutia stress na hakuna umuhimu huo.
Social anxiety
 
Siku zote huwa nakaa Mbali na Watu wanaoongea sana..!
Na wale wanaotaka kunizoea kwa haraka!

Nina Marafiki 2 tu....! Lakini rafiki zangu hao sio introverts!

Binafsi hata kuwa na Demu mpaka nitengeneze Urafiki kwanza...!!!

Napenda kujitegemea kifikra, kiuchumi na kila kitu!
Naweza kusema na Moyo wangu nikatatua matatizo ndani yangu!!!
Hizi ndio tabia zetu halisi,sio kila mtu anaweza kuwa rafiki yako,tunajiamini kupita maelezo,inafikia watu wanasema ngoja tumuone akipata tatizo nani atamsaidia,likifika tatizo wanashangaa limepita na hakuna lililokupata,kumbe hawajui kuwa kiroho Introverts huwa anakuwa kila wakati ameshatengeneza solution kwa matatizo yake na hii ni kwasababu ya kujiamini sana...
 
Njna rafiki mmoja tu ambae ndie ndugu angu

Wengine wote wamebaki washkaji tu.
 
Back
Top Bottom