Watu wasiojulikana wampiga risasi na kumuua Alphonce Nyinzi M/Kiti wa Mtaa wa Bulale mkoani Mwanza

Wakuu.
Nilivyoongea na OCS Jana kumweleza kuna tukio LA mauaji haraka aliniuliza ni kwe mm ye mpesa? Hivi kauli hii ililenga nini!
 
Mkuu, jaribu kuipitia tena ,isome kwa uangalifu halafu rekebisha makosa madogo.
 
Mkuu ntamaholo.
Kwanini kudhalilisha taaluma za wengine. Mbona hatujasikia wananchi wakiombwa kufanya kazi ya Daktari kipindupindu kikiibuka? Kwanini polisi ambao wana intelijensia inayofanya kazi wakati wa shughuli za siasa?
Mkuu wewe utakuwa mchanga wa masuala haya. Sisi wakongwe tunajua. Ngoja nijaribu kukupa hints kidogo, i hope utanielewa.

1. Kwa mujibu wa sensa, tunakaribia mil 50. Na kwa mujibu wa taarifa za Polisi wenyewe, wanadai hawazidi 40,000 na hapo ni kuanzia ijp hadi aliyeko mafunzoni leo. Hivyo kila askari anahudumia watu 1250 kuhakikisha ulinzi na usalama wao. Hapo inajumuisha viongozi, walioko likizo, masomoni, wagonjwa na waliopata ulemavu wakitekeleza majukum ya kiulinzi. Kazi ni pevu.

International standard inataka kila askari kuhudumia 1:400, ni nchi chache sana zimefikia kiwango hicho.

2. Katiba ya jamhuri ya muungano ya JMT, inatamka wazi kuwa, ulinzi na usalama wa taifa hili, ni wajibu wa kila mwanachi. Kila mtu anahitaji kuwa salama na usalama ni zao letu sisi sote. Kama mimi nahitaji usalama, wewe huhitaji usalama, ni wajibu wangu kuhakikisha nawe unakuwa mwana usalama.

3. Sheria inayounda jeshi la polisi cap 322, pamoja na mambo mengine, ni kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

4. Sheria ya usalama wa taifa, kila mtu kwenye eneo lake ana wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama unashamiri.

5. Sheria ya tawala za mikoa/wilaya na serikali za mtaa, wajibu wa kila kiongozi kwenye Tamisemi, kazi yake ya kwanza ni kuhakikisha watu wako salama.

Kwa hiyo kutaka ulinzi na usalama kwa kutegemea Polisi, huku wanaohitaji usalama hawashiriki ni kujidanganya tu. Intelijensi ya polisi inahitaji wananchi ili ifanye kazi. Intelijensi ya tiss inahitaji wananchi ifanye kazi. Bila wananchi hakuna linalofanyika.

Wahalifu ni sehem ya jamii, na wanajamii wanawajua wahalifu. Polisi haiwezi kuota. Wananchi wawatumbue tu.

Kazi ya polisi ni profession lkn huwezi linganisha na udaktari. Hata hivyo, ili madaktari watekeleze wajibu wao ipasavyo, wanahitaji kusimamiwa na wananchi wenyewe au kupitia viongozi wao. La sivyo matatizo yaliyopo yangekuwa maradufu ya haya yaliyopo.

Sijui umenielewa? Uliza kama hujaelewa
 
Wakuu.
Nilivyoongea na OCS Jana kumweleza kuna tukio LA mauaji haraka aliniuliza ni kwe mm ye mpesa? Hivi kauli hii ililenga nini!
Kwanza andika vizuri, sarufi izingatiwe.

Pili ni kwa nia moja tu kwa uelewa wangu. Kila wahalifu huwa na namna wanavyotekeleza uhalifu wao. Alikuuliza kujua kama ni kwenye m pesa ili kujaribu kulinganisha mbinu zilizotumika na wahalifu wengine.

Ndio maana wengine jana hiyo tulikuuliza uidadavue habari yako ili mtendaji yeyote akiisoma apate pa kuanzia.

Usimwelewe vinginevyo OCS wako mkuu
 
hii nchi ulinzi upo kwa walinda vituo vya kura mengine hakuna, kipindi cha uchaguzi nchi ilikuwa na ulinzi mkali sana mpaka tukawa tunalala milango wazi na hakuna jambazi, mwizi au kibaka kukuvamia, uchaguzi umeisha na wale askari hatuwaoni tena
 
MAUAJI MWANZA:
Watu wasiojulikana wampiga risasi na kumuua M/Kiti wa Mtaa wa Bulale mkoani Mwanza Alphonce Nyinzi na kumjeruhi mama mmoja, polisi wathibitisha.
Source Mwananchi.
 
hii nchi ulinzi upo kwa walinda vituo vya kura mengine hakuna, kipindi cha uchaguzi nchi ilikuwa na ulinzi mkali sana mpaka tukawa tunalala milango wazi na hakuna jambazi, mwizi au kibaka kukuvamia, uchaguzi umeisha na wale askari hatuwaoni tena
Ulinzi ni garama. Kila mgambo alilamba 60,000/- kama vipi tuendelezeni tulipoachia
 
Kwan matukio yote yanafanywa kwa smg tuu hiyo ya smg ni moja ila point yake ya msingi ni kwa silaha zote zinazomilikiwa na sio smg tuu
 
Huez anzisha ulinzi shirikishi ikiwa jeshi LA polisi halitoi response kwa wakati na pia hawafanyi kazi kwa ufanisi wanapohitajika sasa hayo aliyoyasema mchangia wa mwanzo yote no muhimu
 
Dr Akili you are smart !
 
Kinachoendelea tukio LA mauaji mza.
Viongozi mbalimbali wa chama na serikali wamefika kutoa salam za pole.
Miongoni mwao ni mbunge wa Nyamagana, naibu meya wa jiji, Katibu wa ccm was wilaya za Nyamagana na Ilemela na Katibu was ccm mkoa.
Katibu wa mkoa amelitaka jeshi LA polisi kutoa taarifa ya walipofikia katika kufuatilia natukio ya mauaji ya wilayani Nyamagana
Pia jeshi LA polisi lifanye kazi yake ili kuwaondolea hofu wananchi wa Mza. Watu aamekuwa wakishi kwa hofu ya kupopilewa na wahalifu hivyo polisi wafanye kazi yao ipasavyo kuimarisha usalama.
Aidha Katibu huyo amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi ikiwa wanatofauti zozote.
Yaonekana Katibu anahisi mauaji haya yana mwelekeo huo.
Kadhalika ccm wameahidi kutoa gari LA kusafirisha mwili was marehemu kwenda inara wilayani kwimba kwa mazishi halo keshokutwa.
Imeelezwa kuwa uchunguzi wa Daktari umethibitidha kuwa marehemu ameuawa kwa kupigwa risasi moja iliuoingia kifuanj na kutokea ubavuni.
 
Tunaendelea kushuhudia mengi. Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wakiongozwa na mkuu was mkoa ndio inaingia.
 
Wakati Jana tulipokuwa tukihitaji msaada was polisi, baadhi ya wachaangiaji waludai wana raslimali chache ikiw ni pamoja na nagari. Vipi hi I kamati ifike hapa na msafara wa magari 11 na poisi juu. Hizi raslimali hupungua kwa wananchi wa kawaida pekee?
 
Haya mauji yatakuwa yanafanywa na raia wa nchi jirani wanaoachwa kuishi kama wazawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…