Watu watatu wafikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita

Watu watatu wafikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita

Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao wa sasa Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.
Twenty years, kwa hiyo waliua wakiwa na miaka 14, 12 na mwingine 10?
Duh....
 
Polisi akili zao sometimes ni shida sana.

Sasa hao watahukumiwa kwa kufata sheria kua ni watoto au watu wazima??
 
Ni vile tu hapa tz mitandao ya kijamii imejazwa na posts za kijingajinga ndo zinazotrend.

Ila hii habari ni kioja cha mwaka ingetrend hatari. Hawa polisi wangenyooshwa na hii mitandao ya kijamii ila ndo ivo huko insta, fb na kwingineko ni upuuzi wa harmo na kajala tu
 
mbona hii habari ina ukakasi mwingi ?
kumbe ukiua bado mtoto unasubiria ukue ndio ukamatwe ?
 
Soma vizuri yaliyoandikwa. Mwandishi amesema kabisa umri wa watuhumiwa wakati wa tukio ulikuwa kadha wa kadha.
Wabongo kwa kudandia story juu juu hawajambo.
Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.

Jitahidi kusoma between the line kiongozi wangu. Nadhani hakuna utata wa aina yoyote katika hili. Maana yake ni kwamba, chukua umri wa kila mtugumiwa kwa wakati huu, kisha jumlisha miaka 20 ili upate umri halisi wa sasa wa kila mtuhumiwa.
Kuna mdau ameshawajibu hapo juu. Mtoa mada hakuandika hivyo mwanzoni! Baada ya kumshangaa, ndiyo aka edit. Kwa hiyo kama ni kukurupuka, basi alikuwa Mtoa mada, na siyo sisi.
 
Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.

Mna haraka sana au hamjasoma mada?
Ali edit baadaye! Ila mwanzo hakuandika hivyo.
 
Waliojaribu kumuua Lissu tutaharibu makaburi yao kama wamekufa.
kwani alikufa? angekufa ndiyo mngeharibu hayo makaburi sasa hajafa na hataki kuja kushtaki amekaa tu mhuko kwa bwana zake nani afanye uchunguzi wakati yeye hayupo?
 
kwani alikufa? angekufa ndiyo mngeharibu hayo makaburi sasa hajafa na hataki kuja kushtaki amekaa tu mhuko kwa bwana zake nani afanye uchunguzi wakati yeye hayupo?
Mwandiko huwakilisha uhalisia wa mwandikaji.
Usipo uthamini uhai wa mwenzako juwa hata uhai wa kizazi chako hauuthamini. Tunaishi kwa kutegemeana,hakuna mkamilifu. Tuishi tukiamini kesho yetu ni leo maana yajayo hatuyajui.
 
Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.

Mna haraka sana au hamjasoma mada?
Wewe ndio hujasoma, wamesema huo ndio umri wao wa sasa, soma tena
 
Kesi za aina hiyo zipo nyingi sana mtwara wakishafanya uhalifu wao wanakimbilia nchi jirani ya Msumbiji.
 
Au mimi sikuelewa awali?
Screenshot_20220419-182517.png
 
Watoto wa miaka kumi na nne,kumi na tatu miaka 20 iliyopita walikuwa kidogo wana miili unaweza kusema ni sawa tu na watoto wa form 3 miaka hii hivyo akili ya kutenda jinai hiyo wanaweza kuwa nayo na hata akili ya kusema tufiche mwili wanaweza kuwa nayo vilevile,miaka ya 80 tukiwa bado wadogo kuna mtoto mwenzetu mtaani alimpiga teke la tumbo mwenzie na kumuua tukiwa tunacheza tu kiutaniutani hivyo labda tusikie mazingira ya kifo yalikuwaje kwa wenzetu
...Swala la kuwa na mwili Ni asili tu Kuna madogo was miaka 2004,2005 na 2006 ukiambiwa ndo miaka waliyozaliwa na miili yao unaweza ukabisha
 
Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao wa sasa kuwa ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.
Walitenda kosa wakiwa watoto na hawakujulikana wala siri kufichuka!!!
34-20=14
32-20=12
30-20=10
 
Back
Top Bottom