Watu wengi hawafanikiwi Kimaombi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kukosea hii sehemu ndogo sana ila muhimu mno

Kuhusu kusoma Bibilia hapo sijakuelewa maana tunachanganya kati ya vitu vya kubarikiwa na vitu vya kuwajibikia.
Kumuabudu Mungu ni wajibu sio ombi na kama unataka kubarikiwa ni lazima umtafute Mungu kwa bidii
Mithali 8:17
Lazima ujue mifumo ambayo Mungu anatoa baraka na mafanikio watu wengi wanaenda kanisani lakini hawajui mifumo sababu hawasomi biblia
 
Unajua kabisa hadi sasa (2024) idadi ya Watu wote tuliopo Duniani ni Bilioni 8 na Milioni 200 halafu bado ukiwa Unasali ama Chumbani Kwako au Kanisani au Msikitini unamuorodheshea Mwenyezi Mungu lundo la mahitaji ukidhani atakuwa na muda wa Kukujibu yote.

Kuanzia sasa GENTAMYCINE nakufundisha jinsi ya Kusali kwa Mwenyezi Mungu na aweze Kukusikia na hata Kukubariki kwa haraka pia....

Jitahidi kila Siku kuomba Kitu kimoja tu unachoona ni cha muhimu Kwako na ukiona amekibariki na umekipata unaweza ukaongeza na kingine na uendelee hivyo hivyo utaona utakavyobarikiwa haraka.

Utakuta Mtu mmoja ndani ya Siku anaomba Mwenyezi Mungu ampe Kazi, Gari, Nyumba, Mke, Shamba na mengineyo akidhani Mungu ana muda wa kutosha Kumsikiliza Yeye tu na kuwaacha Wengine Bilioni 8 na Milioni 200 waliopo Duniani.
Unafikiria/unamchukulia Mwenye Mungu na kama binadamu!
Kama wq mwanzo wetu katka kuumbwa (Adam) na wa mwisho wetu tutamuomba kwa wakati mmoja maombi (mahitaji) ya idadi ya wingi wetu basi jua kuwa Mwenyezi Mungu atatusikia sote na akitaka atatujibu sote na hatopungukiwa na chochote ktk ufalme wake!
 
Kumuabudu Mungu ni wajibu sio ombi na kama unataka kubarikiwa ni lazima umtafute Mungu kwa bidii
Mithali 8:17
Lazima ujue mifumo ambayo Mungu anatoa baraka na mafanikio watu wengi wanaenda kanisani lakini hawajui mifumo sababu hawasomi biblia

Sawa tuendelee kusoma neno Kwa bidii ili Mungu akaitakase mioyo yetu.
 
Du, Una uwelewa mdogo Sana wa Mungu.

Mungu huyuhuyu alieumba Galaxy 2 trillion, na kila galaxy kuna ma billion ya nyota, na baadhi ya nyota ni kubwa kuliko dunia yetu ashindwe kujibu Vimaombi vyako 10.

Vizuizi vikubwa vya maombi:
1) Uovu: Mungu hawasikilizi waovu
2) ULEGEVU: Watu wengi hawaombi kwa bidii
Point namba mbili naikataa. Point namba moja ndo sababu.

Mungu ni Baba Yetu Mwema. Tukifunze kuongea naye kama Nabii Eliya Alivyoongea naye.

Mungu hataki uombe kama yale manabii ya baali.

Ongea na Mungu kama Baba Yako Mwema.
 
Ni muhimu zaidi kabla ya kuomba ujipatanishe na kujitakasa kwa toba kwa Mungu, kwa mawazo, maneno na matendo,

ili hatimae roho mtakatifu afanye makao ndani yako, na kuhuisha nafsi yako ili iwe rahisi kwako kuskia na kutambua sauti ya wito wa Mungu kwenye maisha yako.,
Ooh hallelujah..

Na kwenye maombi ya mahitaji yako kwa Mungu,
Ni vema na muhimu zaidi kuonyesha dhamira ya matumizi ya unachoomba endapo utapewa; kama je, kitakua Baraka na Neema kwako na wengine, au kitakua ni anasa, kero na usumbufu kwa wengine?

Maana kuna mtu anaomba Mungu ampatie gari kwajili ya kuzunguka kwenye mabaa mjini kufanya ufuska na kusumbua wake wa wenyewe...

Mungu akufanikishe katika Mahitaji yako Aimen 🐒
Wewe unayefurahia na kuhubiri kuumizwa Kwa watu Huwa unafanya hivi? Na je unajua kwamba Kila dhambi italipwa?
Wewe upotoshaye ukweli kwa manufaa ya watawala wanaodhulumu Haki na Haki ya kuishi unayafanya haya? Na kama unayafanya haya je unajua ya kwamba Mungu hadhihakiwi? Kwamba unaomba Msamaha halafu unarudia Yale yale?
 
Du, Una uwelewa mdogo Sana wa Mungu.

Mungu huyuhuyu alieumba Galaxy 2 trillion, na kila galaxy kuna ma billion ya nyota, na baadhi ya nyota ni kubwa kuliko dunia yetu ashindwe kujibu Vimaombi vyako 10.

Vizuizi vikubwa vya maombi:
1) Uovu: Mungu hawasikilizi waovu
2) ULEGEVU: Watu wengi hawaombi kwa bidii
Wewe ndio umeongea madini mkuu sio Kama huyo mpiga porojo
 
Unajua kabisa hadi sasa (2024) idadi ya Watu wote tuliopo Duniani ni Bilioni 8 na Milioni 200 halafu bado ukiwa Unasali ama Chumbani Kwako au Kanisani au Msikitini unamuorodheshea Mwenyezi Mungu lundo la mahitaji ukidhani atakuwa na muda wa Kukujibu yote.

Kuanzia sasa GENTAMYCINE nakufundisha jinsi ya Kusali kwa Mwenyezi Mungu na aweze Kukusikia na hata Kukubariki kwa haraka pia....

Jitahidi kila Siku kuomba Kitu kimoja tu unachoona ni cha muhimu Kwako na ukiona amekibariki na umekipata unaweza ukaongeza na kingine na uendelee hivyo hivyo utaona utakavyobarikiwa haraka.

Utakuta Mtu mmoja ndani ya Siku anaomba Mwenyezi Mungu ampe Kazi, Gari, Nyumba, Mke, Shamba na mengineyo akidhani Mungu ana muda wa kutosha Kumsikiliza Yeye tu na kuwaacha Wengine Bilioni 8 na Milioni 200 waliopo Duniani.
Bandiko lako linaonesha kuna miungu/ Miungu wengi sana, na wanazidiana uwezo.
 
Wewe unayefurahia na kuhubiri kuumizwa Kwa watu Huwa unafanya hivi? Na je unajua kwamba Kila dhambi italipwa?
Wewe upotoshaye ukweli kwa manufaa ya watawala wanaodhulumu Haki na Haki ya kuishi unayafanya haya? Na kama unayafanya haya je unajua ya kwamba Mungu hadhihakiwi? Kwamba unaomba Msamaha halafu unarudia Yale yale?
sina hakika kama wadau wamekuelewa gentleman,

Hata hivyo,
Nakuombea Baraka na Neema za Mungu, aondoe roho chafu ya hasira na ghadhabu, kwani hiyo ni dalili ya kiburi na kukata tamaa, Lakini pia ni chanzo cha kujitenga na kua mbali na Mungu.

Mungu akubariki na akufanikishe uondokane na roho ya uvivu 🐒
 
Kipi kiswahili fasaha kati ya,
1.Roho wa bwana au roho ya bwana.
2.Tuko mbele zako au tuko mbele yako.
Nieleweshini enyi walumbi.
Mungu katika dini inaeleza yupo katika nafsi 3 ....lakini katika imani Mungu ni mmoja (The creator). Chagua statement yako moja sahihi.
 
Ni wewe tu maombi yako yamejibiwa mapema hio haina maana wengine hawaombi au hawafanyi unavyovifanya wewe ni foleni tu ila wewe ndo umetangulia kujibiwa wengine tunasubiri
 
Huna uelewa juu ya MUNGU.
MUNGU hashindwi kusikia maombi kisa wingi wa wanadamu wanaomuomba, ubize wa MUNGU haupo kwa sababu ya wingi wa wanadamu duniani.

MUNGU ni mfumo uliokamilika ambao unashughulika na kuamua bila kujali idadi ya wahitaji. MUNGU ni nguvu na mamlaka inayokijua kila kiumbe kilichopo ulimwenguni kote.

Maombi kwa MUNGU yaanze na shukrani kwa wingi na Sifa za dhati.

Mtu aanze kwa kujitakasa ( Toba) na Kisha kushukuru kwa vingi ndipo aweke na ombi lake.

MUNGU anahitaji kutambuliwa kwa vingi anavyotufanyia maishani mwetu ingawa wengi wetu tunavichukulia vya kawaida.
 
Unajua kabisa hadi sasa (2024) idadi ya Watu wote tuliopo Duniani ni Bilioni 8 na Milioni 200 halafu bado ukiwa Unasali ama Chumbani Kwako au Kanisani au Msikitini unamuorodheshea Mwenyezi Mungu lundo la mahitaji ukidhani atakuwa na muda wa Kukujibu yote.

Kuanzia sasa GENTAMYCINE nakufundisha jinsi ya Kusali kwa Mwenyezi Mungu na aweze Kukusikia na hata Kukubariki kwa haraka pia....

Jitahidi kila Siku kuomba Kitu kimoja tu unachoona ni cha muhimu Kwako na ukiona amekibariki na umekipata unaweza ukaongeza na kingine na uendelee hivyo hivyo utaona utakavyobarikiwa haraka.

Utakuta Mtu mmoja ndani ya Siku anaomba Mwenyezi Mungu ampe Kazi, Gari, Nyumba, Mke, Shamba na mengineyo akidhani Mungu ana muda wa kutosha Kumsikiliza Yeye tu na kuwaacha Wengine Bilioni 8 na Milioni 200 waliopo Duniani.
,
 
Katoto kadogo hakaombi msaada wowote, kanajua wazazi wanajua wajibu wao. Sisi mbele ya Mungu ni zaidi ya hako katoto, anajua shida zetu, hakuna haja ya kujipendekeza. Kumbuka Mungu ni mweza ya yote.
 
Back
Top Bottom