Watu wengi sana wanatamani biashara ya madini wanapowaona matajiri lakini wanafichwa mengi, hii ni biashara katili sana

Watu wengi sana wanatamani biashara ya madini wanapowaona matajiri lakini wanafichwa mengi, hii ni biashara katili sana

Hayo yoote uliyoandika ndio sababu ya kuwepo wenye nacho na wasiokua nacho. Kumiliki kunahitaji roho ngumu, wenye roho nyepesi, wanatafuta hela za kula
 
Nani? Mirembe? Yule Dada alikuwa mfanyakazi wa GGM wala hafanyi biashara ya madini na kifo chake hakihusiani hata na madini ni upuuzi wao tu wale.
Naona hata hujui , uliza kuna tajiri ambaye alitokea Dar kwao ni huko , fuatilia
 
Biashara gani yenye guarantee ili kila mtu afanye hiyo awe tajiri?

Toa majina matatu tu ya watu waliofanyiwa umafia na kuuwawa Geita au Chunya? Sio Mererani. Hii lazima iwe credible source sio story zenu za vijiweni za hearsay.

Kama uchawi unafanya kazi kwanini wasichimbe dar hadi waende sehemu zenye hayo madini?

Miafrika mnapenda sana kuamini ujinga.
Shida sio waafrika tu bali hata wachina na wajapani nishawahi kuona wanafanya mila kwenye miradi wanayofanya waulize wakazi wa mtambaswala wakati linajengwa daraja watakusimulia mambo yaliyokifanyika pale au hata hapo wakati wanajenga daraja la rufiji....tatizo wabongo wengi hawajui hata huko ulaya na Asia Kuna waganga wa kienyeji
 
Watu weusi na ndumba Pete na kidole Ila wamachimboni wamezidi
 
Sasa wewe unayejua humtaji si uchuro huo!
Nimeshakuambia wanakufa ,ni mwajka juzi tu hapa..Yaani utajiwe mpoaka jina 😀 😀 na hao wakaofukiwa na maduara nao nikutajie majina
 
Shida sio waafrika tu bali hata wachina na wajapani nishawahi kuona wanafanya mila kwenye miradi wanayofanya waulize wakazi wa mtambaswala wakati linajengwa daraja watakusimulia mambo yaliyokifanyika pale au hata hapo wakati wanajenga daraja la rufiji....tatizo wabongo wengi hawajui hata huko ulaya na Asia Kuna waganga wa kienyeji

Hizi story zenu za kusadikika zisizo na uthibitisho wa aina yeyote ule ni ujinga. Mimi nimewahi kwenda mbinguni na kurudi. Huwezi bisha maana hukuwepo na sina chochote kile kama kithibiti. Ukiwa zwazwa utaamini. That's how crazy your story sounds.
 
Hiyo ni miiko waliyokariri wachimbaji wengi hasa hawa wachimbaji wadogo wasiokutumia vifaa maalum vya kudetect madini yalipo.
Wengi wao hujikuta wanachimba kwa kubahatisha. Hivyo hukata tamaa mapema hasa pale kina cha kuyafikia madini kinapokuwa mbali.
Halafu kingine kinacho sababisha waendekeze hizo norms ni vile wachimbaji wengi wao ni wale wasiokuwa na exposure, wengi std VII na wengine hawajasoma kabisa. So jamii kama hii ni rahisi kushawishika na kujiingiza kwenye ushirikina. Make unakuta wanakomaa kuchimba huku mifukoni hawana kitu. So wanaopt kutumia ushirikina kwa kuamini kwamba kafara itavuta madini haraka.

Halafu ifahamike kwamba kwenye sekta ya wachimbaji madini wadogo kuna madaraja pia.
Wapo wachimbaji wanaozama maduarani, wapo wawezeshaji kwajili ya kugharamia wachimbaji kabla duara halijatua, wapo wanunuzi wa mawe ya madini, wapo makota/madigala kwajili ya kununua dhahabu na wa mwisho kabisa ni wale wanaoozesha ule udongo baada ya kuchenjuliwa na mercury ambao hawa hupeleka kifusi plant.
 
Hakuna ukweli wowote kuhusu ndumba kuwa itakufanya upate dhahabu bali ni imani potofu tu za watu.Ili uwe na uhakika wa dhahabu lazima ufanyike utafiti wa kitaalamu kwenye eneo unalotaka kuwekeza ili ujue kama kuna dhahabu au hakuna.
 
Huwezi kunishawishi nikakubaliana na wewe kwamba mtu mwenye rundo la kifusi anaepeleka plant eti atategemea ndumba ili apate madini mengi.
Hiyo ni big NO coz provided mwamba umesoma PPM za kutosha, huyo lazima apige hela ndefu tu.

So ukosefu wa mitaji ndo hupelekea watu waamini katika ushirikina.
Pia mnunuzi wa madini hahitaji kuamini ktk ushirikina ndo apate shehena kubwa ya dhahabu isipokuwa mtaji mkubwa ndo utamuwezesha kupata shehena kubwa na hatimae atauza na kupata faida kubwa.

So wanao hangaika na ulozi huko migodini ni wale wanaohusika direct na uchimbaji pasipo kuwa na vifaa vya kitaalam.
 
Hii haijatengenezwa kuzima mjadala wa Documentary ya bbc ???
Nyashindwa KUELEWA
 
Hizi story zenu za kusadikika zisizo na uthibitisho wa aina yeyote ule ni ujinga. Mimi nimewahi kwenda mbinguni na kurudi. Huwezi bisha maana hukuwepo na sina chochote kile kama kithibiti. Ukiwa zwazwa utaamini. That's how crazy your story sounds.
Weww ni mkristo?
 
Back
Top Bottom