Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Hakuna lolote la maana linalopatikana kwa kulamba michirizi ya michuzi vidoleni ama masalia ya chakula zaidi ya uchafu.Picha linaanza, nimeenda ukweni kanda ya ziwa kulipa mahari. Siku hiyo walichinja Ng'ombe na msosi ulikuwa wa kutosha. Muda wa kula nakumbuka sisi tuliwekwa sehemu moja na wenyeji wetu wawili ili tusiwe wapweke, daah walivyokuwa wanalamba vidole wale mabwana hadi nikaghairi kula. Wenyewe wanasema kuwa haitakiwi mkono ubaki na mabaki ya chakula, kwahiyo wanalamba mikono haswa ili kuisafisha huku wanaendelea kula, pia hawajui kula sehemu moja. Muda huu atamega tonge upande huu, ila tonge la pili litamegwa upande ule na tonge la tatu litamegwa katikati. Nikamtumia meseji waif afanye mchakato aniletee chakula cha peke yangu,kweli kikaletwa nikala. Japo maneo ya chichini yaliongeleka kuwa sipendi kula sahani moja na wenyeji.
Baada ya kuwa mwenyeji hii kanda kwa takribani miaka minne ndo nimegundua kuwa ile siku ya mahari haikuwa bahati mbaya, watu wengi huku kuanzia Simiyu, Shinyanga, Mwanza hadi mara wapo hivyo. Kukuta mtu anakula huku anajichokonoa meno kwa vidole mbele za watu ni kawaida, kula na kukibehulia chakula ni kawaida, kula huku analamba vidole vyote vitano ni kawaida sana, Kula chakula bila kuchagua upande ndo kabisa hawa jamaa ni mafundi, wanadonoa chakula kama kuku.Inatia hasira sana na inakera kushuhudia watu wa namna hii.
Angalau kidogo kwa waliosoma soma na wale wenye exposure ya kusafiri sehemu mbalimbali ndo wanaunafuu.
USHAURI:Wazazi wa kanda ya ziwa wafundisheni vijana wenu ustaarabu wakati wa kula.
Kuna mashemeji zangu walikuja kunitembelea ila nikawaambia waziwazi kuwa sipendi kumuona mtu anakula hovyo kama mbwa hapa nyumbani kwangu.Walienda kusimulia huko walipotoka kuwa nina roho mbaya ila mimi sijali.
Utakuta mtu mzima akila hata kama yuko peke yake lakini analamba vidole!
Unashangaa, kuna nini cha kushibisha anachoweza kulamba na kikakidhi zaidi ya matonge makubwa makubwa aliyobwia?
Nadhani "elimu ya meza" ifundishwe na mashuleni pia, wasiachiwe wazazi pekee.
Angalau hii elimu hutolewa majeshini pekee lakini hustaarabisha sana watu, sasa sijui hawa vijana wetu wa "mujibu" kama elimu hii hufundishwa!
Hakuna kero kubwa inayoteremsha hadhi ya mtu kama kula kijinga jinga bila staha!
Unawezaje mtu mwenye akili zako timamu, ukaanza kula njiani huku unatembea!
Kuna mengi ya kujifunza kuhusu ulaji.
Sote twaweza kuwa na dosari, lakini kula kwa kutafuna kwa sauti..."nyam nyam nyam".. huku ukitoa toa mate ni ushenzi mwingine unaofanywa na watu wasiostaarabika!