Habarini za wakati huu wakuu..
Nimegundua kwamba watu wengi (siyo wote) wenye pesa/mafanikio ya kweli wako very humble. Hadi naanzisha huu uzi, yapo matukio mengi yamethibitisha conclusion hii.
Jana jioni nilienda Morena Hotel Dodoma kujipumzisha. Nikiwa pale nikakutana na rafiki yangu niliyepotezana naye muda mrefu. Akaomba ani-join kwenye meza yangu. Alikuwa anakunywa maji makubwa. Tukawa tunastorisha, akaniambia kwa sasa yeye ni Mhandisi binafsi, aliacha kazi Serikalini akaamua ajiajiri.
Tukiwa tunaendelea na story, nikapigiwa simu na business partner wangu, akaja kutu-join. Kwanza partner alipofika tu alikuwa kaning'iniza funguo za gari kwenye lux, alipofika mezani akazitoa kiunoni akazianika mezani, sambamba na iphone zake mbili. Nikamtambulisha story zikaendelea.
Story zikiendelea, partner akapigiwa simu na client ambaye tunamdai, badala ya kwenda kuzungumzia pembeni au kwa sauti ya chini akawa anapayuka kwa kutaja hadi kiasi cha pesa tunachomdai akidhani kwamba kama ni kiasi kingi kwetu basi ni kingi kwa kila mtu. Sikushangaa kwasababu nimeshamzoea, yeye ni mtu flani hivi (wakubwa mmenielewa).
Baada ya muda kidogo Mhandisi akaagiza Hennesy VSOP Cognac 700ml. Akatuambia na sisi tuagize. Mimi nimeacha pombe, nikaagiza grand malt na coke. Nikamuona partner ana wasiwasi, uso wake umesawajika, ni kama alikuwa anajiuliza kuhusu bill. Akaagiza Heineken, akaletewa 6! Bill ikaja, Mhandisi akalipa, alikataa kabisa kushea au sisi kulipa. Taratibuuu, partner akachukua funguo za gari na simu mezani akaweka mfukoni [emoji28]..
Mhandisi akanywa Hennesy kidogo tu, ingine akabeba, akaomba tuhame pale, partner naye akabeba Heineken zake.
Ile tunafika parking, Mhandisi anasukumu Toyota Land Cruiser V8 VXR nadhani ni ya 2021 ile, partner ana Toyota Vanguard yake, akawa mpole sana. Msiulize mimi naendesha nini [emoji3]...
Mhandisi akaomba tumfate nyuma. Break ya kwanza Bambalaga. Aisee partner alilewa mpaka anauliza pale tuko wapi!
Tukaagana usiku wa saa saba, tukabadilishana contacts. Leo saa tatu asubuhi Mhandisi kanipigia, kuna mradi "X" amepata tender hapa Dodoma. Anataka tuwe Wanasheria wake, yaani tufanye 'retainership agreement', na anatulipa kwa mwaka mzima, leo hiihii amesha-deposit malipo yetu yote ya mwaka in millions. Partner amebaki mdomo wazi!
Mhandisi ni mpole sana. Anachagua maneno ya kuzungumza. Hana mbwembwe yeye ni vitendo tu.
Hii siyo scenario ya kwanza, ziko nyingi sana.
Kwahiyo ukiona mtu anajisifia sana, anaonesha possessions zake hadharani ili kila mtu ajue, ujue hamna kitu hapo. Anafanya hivi ili kujilinda. Kuna kitu najifunza hata whatsap status za matajiri ni tofauti sana na za masikini. Wengine huwa hawapost kabisa au wanapost mara mojamoja, na wakipost hawawezi kupost fitina au majungu.
Hata humu JF, wadau ambao wako vizuri sana huwezi kuwaona ni wajuaji. Hata namna wanavyo-comment ni tofauti sana na masikini na waigizaji wa maisha.
Maisha ni safari ndefu, naendelea kujifunza..