Uhakiki
JF-Expert Member
- May 18, 2017
- 7,288
- 7,704
Maendeleo ya teknolojia yamefanya wanaadamu kuwa katika hali ya kushindwa kukabiliana nayo. Matokeo yake, wengi wamekata tamaa. Kuanzia nchi za dunia ya kwanza hadi dunia ya tatu tabia na mitazamo ya wananchi wengi inafanana.Tunasikitisha sana... Imagine Pascal Mayalla mayala akapate kura moja...
Wanaadamu wengi wa sasa wanapenda masihara na vitu visivyoongeza tija katika maisha yao kama tulizo la usumbufu unaosababishwa na maendeleo ya kiteknolojia.
Ndio maana, mataifa yanayoelewa uhalisia huu. Haya mwachii mwananchi wa kawaida kuamua mambo yake binafsi achilia mbali mambo ya kitaifa.
Wajenzi jamii wanaelewa kizazi cha sasa kinapitia wakati mgumu pengine kuliko kizazi chochote kilichopita.
Mtoa mada kafika hatua mbaya kuelekea kujidhuru. 'Self denial' ni hatua ya mwisho kuelekea kujidhuru.
Nashauri mtoa mada anastahili kupewa huduma ya kisaikolojia mapema iwezekanavyo kabla hajaanza kushambulia mwili wake.