Ndivyo Mungu anavyosema kwa hekima yake maana inapoishia akili ya mwanadamu ndipo yeye huanza.Ikiwa sisi wanadamu tumepiga marufuku au tumeharamisha adhabu za ujumla "collective punishment" inakuaje mungu mkamilifu aione ni sawa??
Kuna haki gani kumuhukumu mtu kwa makosa ya mwingi? Common sense na logic sio kila mtu ahukumiwe na awajibishwe kwa kosa lake?!
🤣🤣Mwenyewe kachemka akamrusha Duniani😁😁😁Jamaa linanguvu sana! Kutoboa ngumu.
Jamaa kma alifanikiwa kushawishi robo tatu ya malaika mbinguni atakushindwa wewe ambae hata Mungu hujawahi kumuona? Kuna kitu hakikuwa sawa tu ndo maana jamaa akalianzisha hawezi kukurupuka tu. Ni vile hajawahi kupewa nafasi yakusema jambo kilitokea nini hadi akazinguana na muumba bali analishwa maneno tu mara alikuwa na wivu,mara alikuwa mjeuri mara alitaka kumpindua Mungu. Vitabu vyote vinamsema vibaya na kumchora vibaya hadi wanamuweka mapembe, vitabu vyote anaezungumza ni Mungu na manabii/ mitume wake.Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu na ninyi mkaao ndani yake. Ole wa nchi na bahari; kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu akiwa na ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache.
Ufunuo 12:12
Very sad,,,sijui kwanini anaruhusu haya…
Wanyama wanavyochinjwa na wanadamu yeye anaangalia tu🥹
Maumivu ya mda mrefu ni mateso sana. Kma ni mtu wako wa karibu inauma sana hasa kma mnafanya kila jambo na ugonjwa hauonekani ila mtu anaumwa sana na anaisha kila siku hadi hatua anarudi utotoni yaan hawezi kufanya kitu tena ni wakuhudumiwa.Pole sana 🫂 , mimi nina mawazo kama huyo kiongozi uliyemquote, nikipata terminal illness ambayo nina uhakika imefikia hatua isiyo na tiba, basi tayari nimeshajiandaa kujiondoa hapa duniani kwa haraka kadri itakavyowezekana.
Ni logical decison ambayo inamsave kila mtu kutoka kwenye unnecessary suffering.
Kama unaona hakuna maana ya kuwepo kiumbe chochote duniani ikiwa kila kitu kipo 100% basi bora binadamu wangekuwa wanaugua homa na mafua tu ila sio Malaria, HIV, TB, Cancer na vifo. Hata hivyo sio kweli kwamba hii ni fikra ya kawaida tu inayozunguka ulimwengu wote. Huu ni mtazamo wako wa dini yako tu.Hakuna Hali iliyokamilika, Kila Hali ina upungufu wake na uimara wake. Hakuna maana ya kuwepo kiumbe chochote duniani ikiwa Kila kitu Kipo 100%, hii ni fikra ya kawaida tu inayozunguka sayari na nyota zote za ulimwengu...
Kama aliweza kumfukuza Adam na Eva bustanini akawapa adhabu.. huyu akatafute kwa jasho, huyu akazae kwa uchungu. basi wacha tuendelee kunywa hicho kikombe, ukiachana na maswahibu ya ulimwengu wa giza wa kina Mshana
Ni wakati mbegu ya baba na yai la mama zinalandana ili kutengeneza kiumbe aliyekamilika mwenye 46 chromosomes, kuna tokea hitilafu kidogo kwenye Crossings kama ziki cross ndivyo sivyo.Mmh, endelea kiongozi, I'm listening
View attachment 3588984
Nakushauri pia ujiulize swali hili: Kwanini tulikubali kula tunda tulilokatazwa tusile?Haijalishi wewe ni muislamu au mkristo, kama una imani yoyote inayoamini kwenye "Mungu" nina maswali hapo chini kwa ajili yako.
- Kwanini Mungu anaruhusu watoto wazaliwe na changamoto za kiafya ambazo hazina tiba na zitawatesa watoto mpaka wanapokufa wakiwa bado watoto wachanga au wadogo? (cancer za watoto, matatizo ya moyo, ubongo, upumuaji etc.)
- Kwanini mungu wako anaruhusu ujauzito utungwe, mtoto akue mpaka akaribie kuzaliwa halafu afie tumboni?
- Naomba kueleweshwa; kwanini Mungu wako muweza yote, anaruhusu vifo vya watoto wasio na hatia? Na, ni nini sababu ya kuwaumba watoto wakiwa na mapungufu ambayo anajua yatakatisha uhai wao?
SABABU YA KULETA HUU UZI:
Nimeumia 😭, mtu wangu wa karibu amepoteza watoto wawil mapacha; mmoja amefia tumboni, mwingine amezaliwa na uvimbe kichwani, amemaliza siku tano amefariki. Inaniwia vigumu kuamini kwamba kuna sababu yoyote hawa watoto walistahili hayo waliyoyapitia.
View attachment 3588755
Naomba utumie lugha nyepesi na unifundishe, kama kuna Mungu kwanini anaruhusu mambo ya kikatili namna hii?
Asante na Alamsiki!
Kwa nini unasema "tulikubali* ? Labda ungesema "walikubali". Hata hivyo hizo ni hadithi tena fiction tu za Wayahudi tu ambazo zinaaminiwa na kuchukuliwa kama ni uhalisia na kweli na Wakristo pamoja na Waislamu. Watu wengine kama Wahindu au Budha nao wana hadithi zao tofauti kabisa. Wanasayansi wao hhawamtambui Adam na Hawa, wanasema binadamu ni matokeo ya evolution.Nakushauri pia ujiulize swali hili: Kwanini tulikubali kula tunda tulilokatazwa tusile?
Niaminivyo mimi ni kwamba sisi wenyewe(uzao wa Adam na Hawa) ndio chanzo cha matatizo na mambo yote mabaya tunayoyaona leo. Tuliambiwa tukila tunda la katikati ya bustani tutakufa, tukakaidi, tukala. Hivyo sisi sote(including watoto) tunakula mshahara wa dhambi yetu ya kukataa kutii agizo la Mungu. Hata hivyo, ninaamini pia kila chenye mwanzo kina mwisho. Hivyo ninaungana na wenye imani kwamba dunia hii inakaribia mwisho, na siku moja tutaingia katika mbingu mpya na nchi mpya isiyokuwa na ubaya wala jambo lolote lenye kuleta huzuni. Tusubiri, muda utaongea
Kama kweli utakuwa na akili basi niambie ni kitu au Hali gani iko kamili asilimia Mia moja katika haya maisha?, nataka unijibu Hilo swali kama kweli wewe Una akili timamu na Nafikiri hujui maana ya dini.Kama unaona hakuna maana ya kuwepo kiumbe chochote duniani ikiwa kila kitu kipo 100% basi bora binadamu wangekuwa wanaugua homa na mafua tu ila sio Malaria, HIV, TB, Cancer na vifo. Hata hivyo sio kweli kwamba hii ni fikra ya kawaida tu inayozunguka ulimwengu wote. Huu ni mtazamo wako wa dini yako tu.
Hio kumfikiria kitofauti sasa ndio mjue hamko completed , mmefumbwa.Binadamu wameweza kumfikiria mungu alivyo, ndio maana kila jamii ina tafsiri yake ya mungu au mungu wao ni tofauti na wengine. Kwa mungu anayefikiriwa na Abrahamic religions ana tabia nyingi za kiume.
Kwanza kuwa kamili ni nini? Halafu kwa nini unaona hakuna maana ya kiumbe chochote kuwa kamili hapa duniani??Kama kweli utakuwa na akili basi niambie ni kitu au Hali gani iko kamili asilimia Mia moja katika haya maisha?, nataka unijibu Hilo swali kama kweli wewe Una akili timamu na Nafikiri hujui maana ya dini.
A lot of gibberish, it doesn't make any sense.Hio kumfikiria kitofauti sasa ndio mjue hamko completed , mmefumbwa.
Kumfikiria sawa basi hatwakuwa Mungu tena.
Hivi kwanini yoda asiwe binti wa zamani? Na binti wa zamani asiwe yoda?
Ni perspective yako, usitake watu wawe kama wewe au wafuate kile unachoons wewe.A lot of gibberish, it doesn't make any sense.
Chaijibu ni hili
Mungu ni nguvu si kiumbe .. Na hiyo nguvu hua haiingilii jambo bila kuamriwa ilifanye .. kwa mfano ilipaswa huyo mjamzito kwa ssaala aiamuru nguvu hiyo imjaalie watoto wenye afya na uzima inge tii .. ILA NGUVU HIYO KAMWE HAIWEZ KUBADILI UALI YA MTU BILA RUHUSA .. tujifunze kusali kwa iman yeyote tu .. ELEWA TU MUNGU NI NGUVU SI KIUMBE MFANO LAHISI CHUKULIAGA MUNGU NI SAWA NA MOTO .. moto unaweza ukautumia utakavyo ila moto kama moto wenyewe hauwez ukajiamria tu kua leo ngoja ukuchomee nyama choma au ngoja leo ukuchomee nyumba .. bali ww utakavyo utumia ndivyo utafanya ... Na mungu pia yupo hivyo...ni nguvu ipo tuli tu uibadili ww ikusaidie nn ?.
Hilo la uwezo ni la pili tuanze na la kwanza, kwanza.Kwahiyo Mungu hana uwezo wala mamlaka ya kufanya kiumbe kikazaliwa au kufa, right?
Jibu Hilo swali langu Kwanza maana ulinijibu mwanzo Kwa kuonyesha kuwa unajua majibu au ulikuwa hujui unachokiandika?... Sasa basi ngoja nkujibu kiufupi, Kamili ni Kutokuwa na upungufu wowote ule haijalishi ni muda gani utapita, ulisema huu ni mtazamo wa dini yangu, je unahisi huu ni mtazamo wa dini na si ukweli kuhusu maisha kama nilivyomjibu mtoa mada(hoja yangu iliakisi) kuwa haijalishi uko na Imani au mungu gani Hali hii ya Kutokuwa kamili itamkumba Kila mtu hivyo mtu asijihisi mnyonge au mbaya Kwa Hali kama hizo za kufiwa na watoto as long as unafanya kuokoa mengine ni nje ya uwezo wako na ndiyo kutokuwa kamili huko....Swali lako la pili ni kwamba, maana ipo kwenye Jambo lisilo kamili na ndio ili kitu kilete maana kinahitaji marekebisho Kila wakati (huu ni mtazamo changamshi).Kwanza kuwa kamili ni nini? Halafu kwa nini unaona hakuna maana ya kiumbe chochote kuwa kamili hapa duniani??