Watu wote mnaomuamini Mungu mje, nina swali kwenu 😢

Watu wote mnaomuamini Mungu mje, nina swali kwenu 😢

Mungu ni nguvu zote na Mungu ni kila kitu.

Mungu ni nguvu, na hutoa nguvu zake kwa watu wake . Mungu hutoa provision ya watoto wote kuwa salama
Sasa kama mungu ni mwenye nguvu zote na hutoa provision ya watoto wote kuwa salama kwa nini watoto wa Gaza hawajawa salama??
 
Haijalishi wewe ni muislamu au mkristo, kama una imani yoyote inayoamini kwenye "Mungu" nina maswali hapo chini kwa ajili yako.
  1. Kwanini Mungu anaruhusu watoto wazaliwe na changamoto za kiafya ambazo hazina tiba na zitawatesa watoto mpaka wanapokufa wakiwa bado watoto wachanga au wadogo? (cancer za watoto, matatizo ya moyo, ubongo, upumuaji etc.)

  2. Kwanini mungu wako anaruhusu ujauzito utungwe, mtoto akue mpaka akaribie kuzaliwa halafu afie tumboni?

  3. Naomba kueleweshwa; kwanini Mungu wako muweza yote, anaruhusu vifo vya watoto wasio na hatia? Na, ni nini sababu ya kuwaumba watoto wakiwa na mapungufu ambayo anajua yatakatisha uhai wao?

    SABABU YA KULETA HUU UZI:
    Nimeumia 😭, mtu wangu wa karibu amepoteza watoto wawil mapacha; mmoja amefia tumboni, mwingine amezaliwa na uvimbe kichwani, amemaliza siku tano amefariki. Inaniwia vigumu kuamini kwamba kuna sababu yoyote hawa watoto walistahili hayo waliyoyapitia.

    View attachment 3588755

    Naomba utumie lugha nyepesi na unifundishe, kama kuna Mungu kwanini anaruhusu mambo ya kikatili namna hii?

    Asante na Alamsiki!

Kwa kuwa Suala lako linahusiana na imani ya dini...
Kama huwa ni muumini wa dini yoyote inayo amini uwepo wa Mungu mmoja mwenye mamlaka yote; Nakushauri ukaulize maswali yako kwa kiongozi wako wa dini.
Na hata kama huamini kwenye dini, nakushauri ukaulize kiongozi yeyote wa dini aliyeko karibu na wewe (Sheikh au Mchungaji) kwani suala lako linahitaji elibu bobezi ya dini......
 
Rudi kasome kitabu chako vizuri, hakuna dhambi isiyompelekea mtu moton. Kulingana na kitabu chako ukiacha kumkufuru roho Mtakatifu dhambi nyingine zote ni sawa.
Kurudi kusoma nasoma vizuri. Ila hakuna mwandamu asie na dhambi na kama hakuna mwanadamu asie na dhambi ( anakosa ukamilifu ) na kama ni hivyo wote wangeenda motoni. Kwenda motoni au mbiguni ni swala jingine . Kafanye utafiti kwa habari ya dhambi na utendaji wa dhambi na ujue stage ipi dhambi inasababisha hukumu ya moto.
 
Sasa kama mungu ni mwenye nguvu zote na hutoa provision ya watoto wote kuwa salama kwa nini watoto wa Gaza hawajawa salama??
Rudia kusoma nilicho andika nadikiri husomi na kutafakari ninacho andika, kila kiti nimeelezea tayari
 
Kama huwa unakwenda Msikitini au Kanisani
Kaulize maswali yako kwa kiongozi wako wa dini
Kwa kuwa Suala lako linahusiana na dini; nakushauri ukaulize kiongozi yeyote wa dini aliyeko karibu na wewe (Sheikh au Mchungaji). Na hii ni kama huamini kwenye uwepo wa dini
Unaogopa nini?
Usitake kuficha mambo ya dini kama Bangi, wacha majadiliano ya wazi yafanyike popote.
 
Haijalishi wewe ni muislamu au mkristo, kama una imani yoyote inayoamini kwenye "Mungu" nina maswali hapo chini kwa ajili yako.
  1. Kwanini Mungu anaruhusu watoto wazaliwe na changamoto za kiafya ambazo hazina tiba na zitawatesa watoto mpaka wanapokufa wakiwa bado watoto wachanga au wadogo? (cancer za watoto, matatizo ya moyo, ubongo, upumuaji etc.)

  2. Kwanini mungu wako anaruhusu ujauzito utungwe, mtoto akue mpaka akaribie kuzaliwa halafu afie tumboni?

  3. Naomba kueleweshwa; kwanini Mungu wako muweza yote, anaruhusu vifo vya watoto wasio na hatia? Na, ni nini sababu ya kuwaumba watoto wakiwa na mapungufu ambayo anajua yatakatisha uhai wao?

    SABABU YA KULETA HUU UZI:
    Nimeumia [emoji24], mtu wangu wa karibu amepoteza watoto wawil mapacha; mmoja amefia tumboni, mwingine amezaliwa na uvimbe kichwani, amemaliza siku tano amefariki. Inaniwia vigumu kuamini kwamba kuna sababu yoyote hawa watoto walistahili hayo waliyoyapitia.

    View attachment 3588755

    Naomba utumie lugha nyepesi na unifundishe, kama kuna Mungu kwanini anaruhusu mambo ya kikatili namna hii?

    Asante na Alamsiki!
Kila kitu kinapotokea mbele ya uso wa MUNGU,kuna sababu ambazo yeye mwenyewe ana mamlaka nazo na anazijua anafanya kwa sababu gani,pengine wazazi au viapo na maagano ya kafara za mababu
 
Unaogopa nini?
Usitake kuficha mambo ya dini kama Bangi, wacha majadiliano ya wazi yafanyike popote.

Nimeona huyu tatizo lake anatakiwa apate referral ili akakutane na madactari Bingwa wa Dini..
Sasa hapa jukwaani anaweza hata kupotoshwa zaidi
 
Kurudi kusoma nasoma vizuri. Ila hakuna mwandamu asie na dhambi na kama hakuna mwanadamu asie na dhambi ( anakosa ukamilifu ) na kama ni hivyo wote wangeenda motoni. Kwenda motoni au mbiguni ni swala jingine . Kafanye utafiti kwa habari ya dhambi na utendaji wa dhambi na ujue stage ipi dhambi inasababisha hukumu ya moto.
Kobas wao wamelitatua hili Tatizo au contradiction kwa kusema madhambi ya watu yatapimwa kwenye mzani upande unaozidia ndipo utakapoelekea huko, ndio maana wao wanakazana sana kuswali, kutoa sadaka, kuhiji, kufunga na kuzingatia kila kitu ikiwemo hata namna ya kuingia chooni.

Wagalatia wa makundi mengi hawana maelezo yoyote ya msingi na thabiti kuhusu dhambi na kuingia mbinguni, wengi wao wanaamini wataingia tu mbinguni kwa kuwa ni Wakristo au wamepata sacrament.
 
Kwa kuwa Suala lako linahusiana na imani ya dini...
Kama huwa ni muumini wa dini yoyote inayo amini uwepo wa Mungu mmoja mwenye mamlaka yote; Nakushauri ukaulize maswali yako kwa kiongozi wako wa dini.
Na hata kama huamini kwenye dini, nakushauri ukaulize kiongozi yeyote wa dini aliyeko karibu na wewe (Sheikh au Mchungaji) kwani suala lako linahitaji elibu bobezi ya dini......
Naamini hata humu jukwaani wapo viongozi wa dini na wale wenye elimu bobezi ya kiimani.

Mpaka hapa mjadala ulipofikia, nimejifunza mengi mapya.
 
Kila kitu kinapotokea mbele ya uso wa MUNGU,kuna sababu ambazo yeye mwenyewe ana mamlaka nazo na anazijua anafanya kwa sababu gani,pengine wazazi au viapo na maagano ya kafara za mababu
Kwanini Mungu anaruhusu maagano na kafara ziathiri viumbe wake wasio na hatia?

Kama wazazi walikosea, kwanini awaadhibu watoto na siyo wale waliokosea?
 
Kwanini Mungu anaruhusu watoto wazaliwe na changamoto za kiafya ambazo hazina tiba na zitawatesa watoto mpaka wanapokufa wakiwa bado watoto wachanga au wadogo? (cancer za watoto, matatizo ya moyo, ubongo, upumuaji etc.)
Hizo changamamoto anazozaliwa nazo mtoto asilimia kubwa zinasababishwa na mama mzazi wa mtoto kwa kutohudhuria kliniki ipasavyo kipindi cha ujauzito, kutofuata ushauri anaopewa na wataalamu wa afya , kutozingatia matumizi sahihi ya dawa anayopewa kipindi cha ujauzito.

Mfano wanapewa vidonge vya fefo ili vimsaidie aendelee kuwa na damu na pia kumsaidia mtoto asipate mgongo wazi (spinal bifida) au mtoto kuzaliwa na kichwa kikubwa (hydrocephalus) lakini utakuta huyu mama hazingatii.

Huyo mama anashauriwa asinywe pombe kipindi cha ujauzito lakini anakaidi, ana shauriwa kama ana kisukari ajitahidi atumie dawa zake za sukari vizuri lakini anapuuza matokeo yake anajifungua mtoto mwenye matatizo ya moyo mfano tetralogy of Fallot. Nk
 
Kobas wao wamelitatua hili Tatizo au contradiction kwa kusema madhambi ya watu yatapimwa kwenye mzani upande unaozidia ndio utapelekea huko, ndio maana wao wanakazana sana kuswali, kutoa sadaka, kuhiji na kuzingatia kila kitu ikiwemo hata namna ya kuingia chooni.

Wagalatia wa makundi mengi hawana maelezo yoyote ya msingi kuhusu dhambi na kuingia mbinguni, wengi wao wanaamini wataingia tu mbinguni kwa kuwa ni Wakristo au wamepata sacrament.
Mkuu dhambi sio tiketi ya motoni. Hapa itakuja tuangalie dhambi ni nini ? Tusiweke dhambi in general hatupata picha pana, mfano dhambi isiyo sameheka inafanyake kazi , dhambi yenye kusamehe ikoje na dhambi katika maisha ya mtu ina atahari gani katika uhusiano wake na Mungu n.k tiachie hapa mada yenyewe sio mambo ya dini
 
Hivyo vifo vya watoto havina uhusiano wowote na hidden or unseen forces.

Ripoti aliyoitoa daktari baada ya hivyo vifo kutokea, hiyo ndiyo sababu iliyopelekea vyao kutokea, nothing else.
 
Kwanini mungu wako anaruhusu ujauzito utungwe, mtoto akue mpaka akaribie kuzaliwa halafu afie tumboni
Una maswali ya kipumbavu sana.

Mama anashauriwa na daktari kipindi cha ujauzito usilale mlalo huu lala hivi lakini mama anakaidi analala chali matokeo yake anakwenda ku compress abdominal aorta , anasababisha damu kutofika kwa mtoto vizuri mtoto anapata intrauterine fetal growth restriction (iufd) mtoto anafariki .
 
Naomba kueleweshwa; kwanini Mungu wako muweza yote, anaruhusu vifo vya watoto wasio na hatia? Na, ni nini sababu ya kuwaumba watoto wakiwa na mapungufu ambayo anajua yatakatisha uhai wao?
Hili nilishajibu hapo juu.

Uzembe wa mama kwa asilimia kunwa ndio chanzo.

Wiki karibia 40 za ujauzito lakini utakuta huyo mama hajawahi kuhudhuria kliniko hata mara moja.
 
Haijalishi wewe ni muislamu au mkristo, kama una imani yoyote inayoamini kwenye "Mungu" nina maswali hapo chini kwa ajili yako.
  1. Kwanini Mungu anaruhusu watoto wazaliwe na changamoto za kiafya ambazo hazina tiba na zitawatesa watoto mpaka wanapokufa wakiwa bado watoto wachanga au wadogo? (cancer za watoto, matatizo ya moyo, ubongo, upumuaji etc.)

  2. Kwanini mungu wako anaruhusu ujauzito utungwe, mtoto akue mpaka akaribie kuzaliwa halafu afie tumboni?

  3. Naomba kueleweshwa; kwanini Mungu wako muweza yote, anaruhusu vifo vya watoto wasio na hatia? Na, ni nini sababu ya kuwaumba watoto wakiwa na mapungufu ambayo anajua yatakatisha uhai wao?

    SABABU YA KULETA HUU UZI:
    Nimeumia 😭, mtu wangu wa karibu amepoteza watoto wawil mapacha; mmoja amefia tumboni, mwingine amezaliwa na uvimbe kichwani, amemaliza siku tano amefariki. Inaniwia vigumu kuamini kwamba kuna sababu yoyote hawa watoto walistahili hayo waliyoyapitia.

    View attachment 3588755

    Naomba utumie lugha nyepesi na unifundishe, kama kuna Mungu kwanini anaruhusu mambo ya kikatili namna hii?

    Asante na Alamsiki!
Yeye mwenyewe aliamuru watoto wasio na hatia wauwawe kwa kukatwa katwa kama nyama (1Sam 15:3). Pia aliwauwa mwenyewe watoto wasio na hata hadi watoto wa wafungwa kwa kosa farao ambaye ni yeye mwenyewe alikuwa anamshika mawazo yake kwa kumfanya awe mkaidi makusudi, na wengi wengine kwa maji katika gharika ya Nchi na moto katika kosa cha Lutu. In fact, nadharia kuwa Mungu wa kiyahudi (naamini ni tofauti kdg na Mungu wa Wakristo na yule wa Waislamu) anajali kuhusu uhai wa watoto sio kweli.
 
Rudia kusoma nilicho andika nadikiri husomi na kutafakari ninacho andika, kila kiti nimeelezea tayari
Sijaona chochote cha maana ulichoelezea zaidi ya kusema sijui zipo nguvu zina interest zinapambana na maneno mengine mengi mengi ambayo yote hayajibu swali langu nililouliza kwa nini watoto wa Gaza, DRC, Sudan na Ukraine wanauwawa ikiwa mambo yote anayopitia mwanadamu yanasababishwa na yaliyotendeka kwenye ulimwengu wa roho.

Nini hasa atakachokuwa ametenda mtoto ambaye hajui jema na baya na wala hajaomba kuletwa duniani katika ulimwengu wa kiroho unaousema hadi ifikie astahili kifo, kansa, kubakwa, kulawitiwa n.k??
 
Back
Top Bottom