KERO Watumishi Ajira Mpya HALMASHAURI YA CHALINZE hatujapewa pesa ya kujikimu
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mtumishi wa ajira mpya kutoka Halmashauri ya Chalinze.

Yaani toka mwezi wa pili hatujapewa pesa za kujikimu na ilihali halmashauri nyingine za mkoa wa Pwani wameshalipwa.

Kila tukiuliza tunaambiwa tutalipwa tu, wanasema kama sio December 2025, basi April au June 2026.
 
Uongozi unatakiwa uwakopeshe halafu zikitoka watarudisha
 
WALIMU MNATUMIKA NA CCM KWA KILA JAMBO HAYO NDIO MATOKEO YAKE
 
Nendeni wote ofisi ya mkurugenzi hakikisheni mmekula msiondoke hapo siku nzima,akizingua nendeni ofisi ya mkuu wa wilaya msiondoke hadi mlipwe ikibidi kulala hapo.
 
Hii pesa mnaweza msipewe kabisa, Shida ya Pesa ya Kujolimu inalipwa na Halmasahuri sasa kama Halmashauri ni Maskini mpo wemgi sana au ina vipaumbele vingi andika maumivu tu!!


Kama mshahara mnapata shukuru Mungu tu
 
Mimi ni mtumishi wa ajira mpya kutoka Halmashauri ya Chalinze.

Yaani toka mwezi wa pili hatujapewa pesa za kujikimu na ilihali halmashauri nyingine za mkoa wa Pwani wameshalipwa.

Kila tukiuliza tunaambiwa tutalipwa tu, wanasema kama sio December 2025, basi April au June 2026.
Halmashauri kuna uchafu mwingi sana.

Pesa za kujikimu kwa ajira mpya na likizo ni kitendawili, mishahara midogo kama wafanyakazi wa Muhindi.

Ila nchi yetu ina utajiri hadi mabeberu wanatuonea wivu wanagawa pesa kwa wanaharakati waharibu amani yetu.

Na halmashauri inayolalamikiwa ni ya mbunge ambaye wizara yake inahusika na utumishi na utwala bora.
 
Ndio maana wanawadanganya na neno Amani bila Haki... endelea kusubiri
 
Tunaomba msaada kwa halmashauri ya chalinze, tumekuwa tukizungushwa sana kuhusu pesa ya kujikimu, watu tumeajiriwa toka mwezi wa pili lakini hadi sasa hatujalipwa na ilihali halmashauri nyingine zimeshalipwa.

Na tukifanya jitihada za kuuliza tunajibiwa subirini tu mtalipwa muda sio mrefu, mara waseme tutawalipa december au april au june.

Tusaidieni kupaza sauti tulipwe hizo pesa maana tuna maisha magumu.
 
mimi mwajiriwa mpya wa mwaka 2025 hadi sasa 2026 hatujalipwa hela ya kujikimu, na ilihali halmashauri nyingine wameshalipwa tumekuwa tukizungushwa sana hadi kwa mkurugenzi tumeuliza lakini hatulipwi,
Kama mnaweza kutusaidia tafadhali tunaomba msaada wenu.
Asante.
 
Ukishakua Halmashauri nakusihi sana tafuta mishe nyingine ya pembeni uwe unafanya kwa ajili ya kujiongezea kipato na usipende sana kazi. Fanya kazi kwa bidii ila usitoe maisha yako kwa ajili ya kazi.

Usikae kazini zaidi ya muda wa masaa ya kawaida. Nenda katafute mchongo hata kama ni boda weka uafisa wako pembeni.

Brace for impact cause kazi ndio kwanza imeanza.
 
Tulieni nchi ina amani. Au umetumwa na Mange Kimambi?
 
Maadili ya Utumishi wa Umma yanakuruhusu kulalamika mitandaoni? hujui kuwa hizo ni siri za ofisi ya umma?
 
Tunaomba mtusaidie kupaza sauti ili mamlaka ziweze kutulipa pesa zetu za kujikimu maana hatujapata hayo malipo toka mwaka 2025 mwezi wa 2, tunazungushwa tu.
 
Watumishi wa Halmashauri ya chalinze ajira ya 2025 hatujapewa pesa ya kujikimu hadi sasa, kila tukifatilia hatupati majibu yanayoeleweka. Tunaomba mtusaidie kupaza sauti na serikali itusaidie hili jambo tupate stahiki zetu.
 
Back
Top Bottom