Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Hapo ukiwa Muislamu halafu Mzanzibari cha kwanza unapewa posho ya kuwa na hizo qualifications [emoji16]
 
Labda tuulize...

Manajaza hizo taarifa kwa ajili ya kumbukumbu za kiofisi, au kuna watu mnakaribia kustaafu hivyo ni uhakiki wa taarifa, au ni kwa ajili ya mambo ya uhamisho?

Hebu weka wazi
 
Tuna balansi udini kwenye teuzi...........na labda wanataka kuwasomesha namba sukuma gang.
 
Hii ni Hamisha magoli watu wacheze mpira uwanja mwingine !! Badala ya kujadili issues za maana zilizopo na zinazolitesa taifa kama ufisadi na ufujaji wa Mali za umma mnakubali kuhamishiwa magoli muanze kuzungumzia vitu vya kufikirika ambavyo havina umuhimu wowote ! Hizi taarifa za dini yako au kabila yako zipo siku zote kwenye baadhi ya nyaraka tangu zamani ni formalities tu za kumtambua mhusika vizuri, that's it !
 
Kwenye rekodi za serikali huwa hakuna dini wala kabila la mtu. Nyerere aliondoa hiyo zamani sana wakati taifa bado ni changa, na hata marais waislamu Mwinyi na Kikwete hawakuirudisha. Sasa tumepata mwislamu kamili ndiye anayeyaleta. Katika teuzi wake naona kipengele cha dini kimekuwa ni cha muhimu sana kwake; na ili kukihalalisha ndiyo maana ameunganisha na ukabila akianzia na kurudisha uchifu.

View attachment 2095774


Tulia wewe kijana mdogo huna unalojua . Serikali ya nyerere ndio ilianzisha kuchukua taarifa za dini na kabila kwenye taarifa za kitaasisi hospitali, polisi, magereza hata kwenye fomu za kujiunga na utumishi wa umma
 
Vyeti vya kuzaliwa vyenyewe havina kipengele cha dini wala kabila..
Huko juu jamani kuweni makini sana
 
Bado hakuna justification yoyote hapo. Kuna mambo ni ya kitaifa au ya kibinaadamu zaidi kuliko ki kabila. Hicho mnachoita "tabia za kikabila" ni matokeo ya kimazingira zaidi na wala siyo genes hivyo huathiriwa zaidi na mazingira anayoishi kuliko kabila lake. Haya ni miongoni mwa masalia ya ukoloni kama yale ya binaadam alikuwa nyani. Hizi ni sawa na stori za kuamini eti kuna makabila ni malaya kuliko mengine: siyo kweli. Much as satisfaction level au sababu za sex almost sawa, ni mazingira tu aliyoishi mtu ndiyo hutoa tafsiri ya jambo flani litendeke vipi au alipe value gani kiasi mtu huyo akiishi mazingira mengine tabia hiyo hubadilika. Infact, kuendelea kuwepo kwa vijitabia vya hovyo vinavyonasibishwa na ukabila ni matokeo ya elimu mbovu inayoshindwa kuleta "convergence" kwenye hayo mambo ya msingi. Mhehe aliyezaliwa au aliyeishi na kusomea Texas definitely hatakuwa sawa na mhehe aliyeishi huko Mufindi. Then essence ya kabila kwenye tabia inatoka wapi hapa!

Mfano mwingine, jamii inamuona mmasai kama ni mtu mshamba, duni, anayefaa kuishi porini tu na mifugo yake. Is that true? Je hakuna wamasai wengine ambao kwa kupata Elimu, au exposure au kuishi na jamii/ mazingira mengine wamekuwa tofauti na mfumo wa asili waliouzoea.

Ukabila ni jambo ambalo halina afya yoyote na popote kwenye society ya Tanzania au jamii iliyostaarabika.
Binafsi naumia sana na haya mambo.
Naona hatari kweli.
 
Taarifa za dini ya mtu ni muhimu. Labda hatujakaa tufikiri vizuri tu.Mfano, watumishi wanakufa kila leo na wanahitaji huduma kwa mujibu wa dini zao. Kama serikali haina taarifa sahihi itawahudumiaje hawa watu?
 
Tulia wewe kijana mdogo huna unalojua . Serikali ya nyerere ndio ilianzisha kuchukua taarifa za dini na kabila kwenye taarifa za kitaasisi hospitali, polisi, magereza hata kwenye fomu za kujiunga na utumishi wa umma
Haya yanatakiwa yafutwe kabisa.
Hayajengi.
 
Taarifa za dini ya mtu ni muhimu. Labda hatujakaa tufikiri vizuri tu.Mfano, watumishi wanakufa kila leo na wanahitaji huduma kwa mujibu wa dini zao. Kama serikali haina taarifa sahihi itawahudumiaje hawa watu?
Kwa hiyo mnataka ili kufanya mazishi?
 
Na Kabila?? Mnapenga nini, kuongea kikabila, au kutambika maofisini!
Wakati wa kuandika proposal ndii uta ona umuhimu wake. Kuna makabila yana tamaduni fulani ambazo hazipo pengine
 
Mimi Bora wale rushwa watakavyo, ila wasiguse kabisa hii misingi midogo midogo inayofanya tuendelee kujiona wamoja.

Naumia siwezi hata kuelezea.
Mambo haya ni kinyume na misingi iliyoasisi taifa hili hayaruhusiwi popote pale hata kufanywa na mjumbe wa nyumba kumi;
  • Kuruudisha uchifu ambao waasisi walithibisha kwa vitendo haufai kwa mustakabali wa taifa.
  • Kurudisha utegemezi kwa mabepari ambao ni kinyume na misingi ya kujitegemea, hata kama hilo la kujitegemea ni la propaganda zaidi kuliko utekelezaji wake, sio vema kulikana hadharani mchana kwwupe.
  • Kurudisha huo ukabila na udini na uzanzibari, hata kama hausemwi lakini tunaona.
Mwalimu na Karume na wazee wenzao hawakuwa wajinga hata kama wakati wao wengi hawakuwa na elimu, wewe huwezi kuwazidi wazee wale, na akili yao ilikuwa haijachafuliwa na pollution yoyote iwe ya kimaadili ama ya vyakula, leo hii kwa sababu hatunauangalizi mkali wa misingi yetu kanaweza kuibuka kajinga fulani katika mfumo wa utawala kuanzia ngazi ya chini hata ya taifa , kalikofanya ufuska wakutosha kwa pollution za western cultures, akili yenyewe mbovu, kakaja kupinga mambo mazito kama hayo, yaani kamtu kama hako kanataka kaumbe taifa lake kenyewe na ss ndio katufanye watoto wake, kutoka kwa baba wa taifa ambae ss ni watoto wake tangu mwanzo,
 
Back
Top Bottom