KERO Watumishi wapya wa Halmashauri ya Chunya hatujalipwa stahiki tezu
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Watumishi wapya tulioajiriwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya hatujalipwa stahiki zetu za kujikimu hadi sasa.

Pamoja na kufuatilia suala hilo, viongozi husika hawajatoa majibu ya wazi kuhusu sababu ya kuchelewa kwa malipo hayo wala lini watumishi tutalipwa.

Hali hiyo imeanza kuathiri morali na ari ya kazi miongoni mwetu, huku tukihitaji ufafanuzi na hatua za haraka kutoka kwa mamlaka husika.
 
KERO: FEDHA ZA KUJIKIMU – HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA

Naomba kuwasilisha kero ya watumishi wapya wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, hususani kada za afya, ambao hadi sasa hatujalipwa fedha zetu za kujikimu baada ya kuripoti vituoni miezi kadhaa nyuma.

Majibu tunayopata hayako wazi, wala hakuna taarifa ya uhakika kuhusu lini malipo yatafanyika.

Tunaomba mamlaka husika itoe ufafanuzi wa wazi kuhusu hatua iliyofikiwa na lini stahiki hizi zitalipwa.
 
Back
Top Bottom