KERO: FEDHA ZA KUJIKIMU – HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA
Naomba kuwasilisha kero ya watumishi wapya wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, hususani kada za afya, ambao hadi sasa hatujalipwa fedha zetu za kujikimu baada ya kuripoti vituoni miezi kadhaa nyuma.
Majibu tunayopata hayako wazi, wala hakuna taarifa ya uhakika kuhusu lini malipo yatafanyika.
Tunaomba mamlaka husika itoe ufafanuzi wa wazi kuhusu hatua iliyofikiwa na lini stahiki hizi zitalipwa.