Watumishi wengi wa Serikali hawana tija. Mishahara inapotea bure

Ndio hivyo serikali itoe chakula na chai ili wtumishi wasitoke kwenda kufanya hivyo vitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu wanafunzi mnawaambia wachange kwa ajili ya chakula wakati hawana mishahara. Wafanyakazi unaiambia serikali iwape chai na chakula wakati wanalipwa.
Naona kichwa kinatumika kufuga nywele tuu.
 
Ni kweli kama ulivyosema

Ila Kuna wengine wako bize na wanafanya kazi Hadi unamwenea huruma
 
Hasa hasa halmshauri huko

Kuna siku nilipita halmshauri moja idara ya kilimo na misitu nikakuta wamekaa juu ya meza za ofisi wanapiga stori.
 
Watumishi wa miaka gani na wanaofanya kazi gani unaowazungumzia? Maana watumishi wa serikali wapo kada tofauti tofauti.
 
Huo siyo wivu tena bali ni umaskini wa akili au mawazo.

Hivi mbobevu wa kazi tena ana elimu ya PhD au MA utamsimamia vipi kazi akae muda wote tu ofisini ilihali anataka afanye kwa usahihi hata kama ni masaa ma6 tu kwa siku kashamaliza kazi alipostahili na kupumzisha ubongo ili baadaye akitoka aendelee na mishe zake nyingine nnje ya kazi?

Dr hufanya kazi kimasaa wala siyo sawa na wafanyakazi wa elimu za diploma n.k.

Pia kadri ya cheo kinavyozidi kupanda tokana na elimu au uzoefu wa maarifa bora ya kazi ndivyo mrundikano wa kazi hupungua.

Ieleweke kazi nyepesi nyepesi na mishahara minono ni za wasomi na ni kinyume na ambao wana elimu za kawaida au hawakusoma kabisa.
 
1. Hili ni miongoni mwa tatizo, hakuna KPI kwa watumishi wengi ambazo ni vigezo vya kuassess kazi

2. Mikataba ya ajira ni permanent and pensionable ( wewe unategemea nini, watu wanakuwa very relaxed) lau ajira zingekuwa fixed contracts with possibility of extention subject to your performance discipline kwenye kazi ingeongezeka

3. Rewards and benefits haziendani na utendaji wako wa kazi au those relevant merits. Mtu anaona hata akijitesa ni kazi bure.

4. Hakuna ufatiliaji wa karibu kwenye majukumu. Hakuna performance evaluation

5. Uvivu tu wa watumishi wengi sector ya ummaa.


Wengine waongezee.....
 
Hii cancer haiwez pona,
Tuendelee kumuombea mgojgwa tu aside.
 
Mleta mada ana point ila sasa baadhi yetu tunajibu kwa kebehi any way ndo uhuru wa mawazo wenyewe kwa hisani ya Jamii forum wacha niendelee.
Kwa hakika Kuna watumishi wengi mno katika idara mbalimbali wanalipwa mishahara bila tija kwa taifa.Mfano what is the return to our nation to the so called TAKUKURU, Kuna walimu mijini wanagawana topic za kufundisha hawa nao wanalipwa mishahara sawa na mtu anayefundisha vipindi zaidi ya 30 per week.Lkn pia kuna watu wanapelekwa halmshauri kufanya kazi za maofisa hawana hata barua ya karibu mkuu tamisemi.Kifupi mleta mada umesema Ukweli lkn kwa sababu Kuna watu pia ni wanufaika watakataa mno.
 
Of course, kama hivyo ndivyo maana yake huwezi kukopi kila kitu kutoka Ulaya.
 
yaani watu wa private wanavyoisema hiyo KPI utadhani ni kitu cha ajabu,,,utadhani ni magenious balaa ,, utadhani sio wavivu na wanawaona watumishi wa serikali ni vilaza balaa,,,,,mafanikio ya sekta binafsi ni yapi (mbona mara nyingi wanatangaza kujiendesha kwa hasara pamoja na hizo KPI )...serikali inatoa huduma kwa asilimia kubwa haifanyi biashara....nenda baadhi ya taasisi za serikali watu wanapiga kazi sana tu......
 
Maswali mengi ya nini? toa solution na wewe
Solution Ni kuwa na Watumishi wanaotosha.

Baada ya Hapo, kila mtumishi apewe haki yake kama mshahara, extra duty, sehemu ya kuishi, nauli au usafiri, na chakula wakati wa kazi.

Mshahara uwe classified katika mafungu, Mshahara, extra duty, nyumba, matibabu ( housing allowance ) n.k

KILA mtu akishapata haki yake, then una haki ya kumdai na wewe UTUMISHI ULIOTUKUKA.

Vinginevyo ASHUGHULIKIWE.
 
Extra duty hulipwa na BAJETI husika ya kituo acha kuchoronga; Kama hawakuweka vifungu Ni lao... Watu wanajilipa kila kukicha
Hapa tunazungumzia UTUMISHI wa UMMA.

Kwa Mfano: WEO/VEO, Mwalimu wana FUNGU lipi ?
 
Wafanyakazi wa kada zifuatazo hawawezi kuwa na ratiba ya namna hii na ikitokea wakafanya hivyo, chances ni kwamba mhusika atafukuzwa kazi ndani ya mwezi mmoja. Kada ambazo hawawezi kuwa na ratiba za namna hii ni:
1. ASKARI POLISI USALAMA WA RAIA
2. WALIMU KUANZIA NGAZI YA CHEKECHEA HADI SEKONDARI (HIGH SCHOOL)
3. MADAKTARI WA BINADAMU
Hawa watu hawawezi kuwa na ratiba ya nmana hii,, na ukizingatia kuwa kundi namba 1 na namba 3, ndiyo pekee wana ratiba ya Masaa 24, ukiongezea na JWTZ
 
Ni kweli kabisa !!
 
Ndio hivyo serikali itoe chakula na chai ili wtumishi wasitoke kwenda kufanya hivyo vitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kufanya hivyo, kutafanya mzunguko wa fedha kwenda kwa wananchi kusinyaa. Hilo jambo si zuri kwa mstakabali wa ustawi wa jamii. Hata hivyo, maeneo maalumu kulingana na unyeti wa kazi hilo wazo linakubalika.
 
Wakuu wa idara na viongozi wengine wa juu wanalipwa parefu sn pamoja na kupewa vyote ulivyovitaja wanafanya nini sasa cha maana zaidi ya majungu na kujipendekeza? mfumo mzima ufumuliwe tuanze upya kwa mikataba na watu wawajibike haswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…