Tatizo serikalini hakuna targets kwa mfanyakazi na hawafanyiwi tathmini kwakua hawasign KPI na ndio wanakwamisha sana Taifa hizi performance na mafanikio tunayoona kwenye sekta binafsi wafanyakazi wake wana sifa sawa kabisa na hawa waserikali ni kwakua wamesoma vyuo hivi hivi lakini utamaduni wakifanya kazi kwa malengo ndio unawatofautisha
You are right..
Lakini pia kuna utofauti Mkubwa wa challenges & motivation factors kati ya mfanyakazi wa sekta binafsi na ya umma...
Hebu twende na mifano michache. Hapa tuna mfanyakazi (askari) wa kikosi cha Zimamoto. Gari la maji ya kuzimia moto liko pale. Kunatokea emergency ya moto somewhere near where you are living. Wafanyakazi wapo lakini vitendea kazi hakuna. Gari halina mafuta ya kuliendesha. Au haliwezi kabisa kutembea kwa sababu halijawa serviced kwa muda mrefu. Ukiuliza unaambiwa hakuna fedha ya mafuta wala service kwa sababu serikali haijatoa hela....!!!
Katika mazingira haya mfanyakazi akilala tu kazini au akienda kutafuta chakula kwa masaa 6 utamshangalia nini? Na hata ukimpa KPI bila vitendea kazi utapata matokeo gani...?
Aidha, katika sekta ya umma ni ngumu sana kuwa na wafanyakazi wenye moyo wa kujituma kwenye public sector kama kunakuwa na utofauti mkubwa wa viwango vya madaraja ya malipo kwa watu walio na kiwango sawa cha elimu tofauti ikiwa ni huyu ni mwalimu, mwingine askari na mwingine daktari nk nk...
Nenda kwa wanasiasa kuanzia ngazi ya mawaziri, wakuu wa idara, maDC, MaRC, wabunge nk nk yaani wamejipangia mishahara na marupurupu makubwa kiasi cha mara 100 au hata 200 cha kiwango cha mshahara wa mwalimu Grade A au Nesi mwenye stashahada...
Na wakati mwingine huyu mbunge au DC au RC anazidiwa kwa mbali sana kielimu na hawa ambao anawasimamia na kuwatungia sheria na sera mbalimbali....
Kinachotakiwa siyo hiki cha kulalamika. Ni kufanyika kwa mageuzi makubwa ktk sekta ya utumishi wa umma. Kusiwe na tofauti kubwa kivile kwa malipo kama ilivyo sasa, kwamba kuna mwingine analipwa 400,000 kwa mwezi na kuna wengine wanavuta hadi 30,000,000....!!
This is completely not fair at all. Katika mazingira haya lazima tu kuwe migogoro mingi msingi wake ukiwa ni tofauti ya kimaslahi miongoni mwa watumishi wa umma...