Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Amwaminiye yeye hatakufa bali ataishi milele
Wao wamepata nafasi ya kutawala pamoja naye Uf 20:4

Ndio hao ambao wanatuombea ambao Uf 6:9-11
 
Huyu mama mnajaribu tu kumshusha ila anadaraja lajuu sana, tunamwomba yeye kama daraja atuombee kwamwanae ukumbuke hata kula kana kwenye harusi walipoishiwa divai hawakumfata yesu mojakwamoja bali walimfata maria awaombee kwamwanae
Ni kweli mkuu, Mama Maria ana daraja. Lakini katika kusoma kwangu Biblia hakuna sehemu nimeona ikisema tupitishie maombi kwake. Labda kama una andiko lolote mkuu linalosema tupitishe maombi kwake tuwekee ili tujifunze mkuu, natanguliza shukurani
 
Ufunuo 20:4 BHN

Kisha nikaona viti vya enzi na watu walioketi juu yake; watu hao walipewa mamlaka ya hukumu. Niliona pia roho za wale waliokuwa wamenyongwa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawa hawakumwabudu yule mnyama na sanamu yake, wala hawakupigwa alama yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao. Walipata tena uhai, wakatawala pamoja na Kristo kwa miaka 1,000.
 
Asantee!!
Na huu ndio msingi na kanuni ya Imani ya Kanisa Katoliki. Ila kuna watu bado wanakwambia wakatoliki wanamkataa Roho Mtakatifu!!
 
Ni kweli mkuu, Mama Maria ana daraja. Lakini katika kusoma kwangu Biblia hakuna sehemu nimeona ikisema tupitishie maombi kwake. Labda kama una andiko lolote mkuu linalosema tupitishe maombi kwake tuwekee ili tujifunze mkuu, natanguliza shukurani
Mt. Bikira maria anatuombea sisi kama watakatifu wengine wanavyotuombea
 
Ni kweli mkuu, Mama Maria ana daraja. Lakini katika kusoma kwangu Biblia hakuna sehemu nimeona ikisema tupitishie maombi kwake. Labda kama una andiko lolote mkuu linalosema tupitishe maombi kwake tuwekee ili tujifunze mkuu, natanguliza shukurani
Hv unawezakunipa andiko lolote linalosema wachungaji wavae neckties?

Issue yamama maria nikwamba yeye ndio yuko karib mno yamwane huyo kristo nahata akiwa anakata roho msalaban alimkabidhi huyo mama kwawanafunz wake kinachofanyika kwaukatoliki nikumtumia mama kama mtu wakarib kutuombea kwamwanae ili atunganishe nae mitume wote walikua namama maria kipind wanamsubir roho mtakatifu aje
 
Kanisa la Roma limewekeza kwenye
elimu ndo maana wana shule na vyuo vikuu vya kutosha nchi nzima.
tena waliunda JESUITS kwa ajili ya kufundisha elimu potofu na kwa makusudi... ili kuingiza mila za kirumi ndani ya kanisa, kuficha ukweli, kupotosha ukweli na kuliteka kanisa la Mungu. Mfano mzuri, wapagani wanamuabudu ISHTAR (ASTHARTE) NA MTOTO (TAMMUZ) ... walipoamrishwa kubadili dini kuwa wakatoliki - waliingiza hii mila kanisani wakibadili majina ya sanamu ya ISHTAR na mtoto kuwa ya Maria na mtoto - na kuendeleza uabudu wao. Hakuna sehemu ambayo biblia inasema Maria aabudiwe. Kwa miaka 300+ baada ya Yahsua (Yesu) kuondoka na kabla katoliki kuundwa, mitume wala waumini hawakuwa na mila hii.

Chunguza vile ambavo amri 10 zimeandikwa bibliani na vile zimeandikwa na katekisimo... wakristo biblia ni moja - niaje

Mkoloni mwenyewe hapa Tanzania alitumia elimu kupotosha...
 
Amwaminiye yeye hatakufa bali ataishi milele
Wao wamepata nafasi ya kutawala pamoja naye Uf 20:4

Ndio hao ambao wanatuombea ambao Uf 6:9-11
Hahaa mkuu, kwani kuna ugumu gani wa kumuomba Yesu direct hadi upige kona nyiingi ambazo syo halali.

Mkuu kwa hiyo unafikiri akina mtakatifu Inyasi muda wao wa kutawala pamoja na Bwana ndo huu uliopo kulingana na hilo andiko? Duu muda bado hadi unyakuo utokee mkuu, waliolala wafufuke na walio hai pamoja kwenda kumlaki Bwana mawinguni ndipo hapo kuna kutawala pamoja na Bwana..Usiogope kupitisha maombi yako direct kwa Jesus.

Sasa ukivamiwa na wachawi usiku huu unafanyaje ..unaanza kumuomba mtakatifu mother Theresa akuombee kwa Yesu ili mchawi akuache hahaa badala ya kuliita tuu jina la Yesu.

Asante mkuu nimejifunza kitu kutoka kwako natumaini pia umejifunza kitu kutoka kwangu.
 
Wewe umeona wapi Bikira Maria anaabudiwa
 
Sasa kama nikiwaomba waniombee kuna shida gani maana wao wapo huko wanatawala pamoja na kristo
 
Kwa bahati nzuri upagani wao wameupenyeza mpaka kwenye biblia ambayo wewe unaringa nayo
 
Issue ya mavazi ni ndogo kwa muktadha huu, swala ni kwamba wapi katika biblia kuna maelekezo yasemayo Mama Maria huko aliko atuombee. Maelekezo niyajuayo ni kwa Jina la Yesu tuu. Karibu chief tujifunze maana elimu ni bahari
 
Panapofuka moshi pana moto - umeshawahi chunguza kwa nini wanasemwa sana? wanasemwa nini?

Hawako kimya - wanatumia elimu na maandishi

Je hizi kesi nyingi za ulawiti wa watoto na wao kutoadhibiwa ... wasisemwe?

* Nakushaurini wenzangu mchunguze historia ya katoliki na matendo yake hapa duniani. Mara nyingi kufuata mkumbo kama kondoo kutakuingiza majangani. Sielewi kwa nini mwanadamu unabatizwa ukiwa mtoto huielewi wala kutambua dini afu ukikua huchunguzi unaumini nini? Hivi kama mkatoliki unatambua viongozi wa kanisa lako ndio waliobadili siku alioamrisha Mungu iwe sabato (jumamosi)? ... na kimaandishi wanatamba kwa hilo tokea enzi, kwa nini?

Mimi ni mrithi wa uLutheri kutoka kwa wazazi - nshabishana hoja kadhaa na wachungaji kwa sababu nako huku wanahitaji kusemwa na kusutwa. Kwa mfano mlipojitenga na kanisa mama kwa tabia mbali mbali ambazo hazikuwa za kibiblia - mbona mmeturudisha kwenye tabia hizo hizo

Naomba niwaulize wakristo wenzangu wakatoliki - kama sote tunatumia biblia ile ile kwa nini katekisimo iliandika amri 10 za Mungu na utofauti fulani kuhusiana na kuabudu sanamu nk? Mm najua kwa nini ila nangoja niwasikie nijifunze zaidi

La mwisho, nawaomba mzingatie lifuatalo - waumini sisi ni kondoo, mchungaji anapotupotosha dhambi kwake, tunapostuka tumepotoshwa ila tunaendeleza mila potofu - dhambi kwetu. Biblia pia inatuambia usichokujua hutahukumiwa, ukishakijua utahukumiwa wewe wala si mchungaji aliekupotosha.

Wengi sisi waumini hatujui mengi, na tunapojadiliana hapa tuwe na moyo huo. Sio kugombania uongo ama kitu ambacho hujakitambua ama kukielewa vizuri. Ogopa sana kuwa mbishi ukitumia elimu yao na uelewa finyu.

Wamefinya elimu ili usijitambue na utetee uovu dhidi ya dini yako mwenyewe.
 
Kwa bahati nzuri upagani wao wameupenyeza mpaka kwenye biblia ambayo wewe unaringa nayo
walichofanya sio sana kupenyeza uongo bibliani... wamepenyeza elimu inayokufanya ukubaliane na tafsiri zao za biblia. Bado unaweza soma biblia leo ukapata ukweli kuliko alivohubiri mchungaji aliejifunza uchungaji kwao.

Kumbuka miaka ya mwanzoni kanisa katoliki lilipiga marufuku muumini asie kiongozi kuwa na biblia. walikuwa hawajaunda Jesuits ama kujipanga mbinu za kudanganya umma - na hawakutaka wabishiwe wakihubiri uongo. Hii miaka walipenyeza mengi kwa jina la biblia na dini
 
Issue ya mavazi ni ndogo kwa muktadha huu, swala ni kwamba wapi katika biblia kuna maelekezo yasemayo Mama Maria huko aliko atuombee. Maelekezo niyajuayo ni kwa Jina la Yesu tuu. Karibu chief tujifunze maana elimu ni bahari
Si tumekupa vifungu kadhaa ambavyo vinaonesha kuwa watakatifu wanatuombea
 
Zilongwa mbali zitendwa mbali sasa kama wao waliamua kitabu kipi kiwepo kipi kisiwepo sasa wangeshindwa kubadilisha

Bado ukaona haitoshi unatumia kitabu hiko hiko ambao ni zao lao kuwasema

Nakusihi tafuta chako afu uje hapa
 
Sasa kama nikiwaomba waniombee kuna shida gani maana wao wapo huko wanatawala pamoja na kristo
Mkuu hujanielewa, muda wa watakatifu kutawala bado mkuu. Badoo mkuu..baaado. Hadi Yesu aje mara ya pili ndo watakatifu watatawala pamoja nae.

Game badoo hilii, hadi arudi kuwahukumu wazima na wafu ndo tutatawala pamoja nae au umesahau ile sala ya kuhukumu wazima na wafu hahaaa.

Akina mtakatifu mashahidi wa Uganda hawana msaada wowote na maombi yetu Bro wame chill tuu. Ni jina la Yesu tuu.

Vamiwa na pepo halafu uite shahidi wa Uganda akusaidie wapi na wapi.

Lakini kwa triki ya shetani unaweza kuita mt shahidi wa Uganda na pepo litoke ili uamini shahidi na uzidi kupotea
 
Kwa bahati nzuri upagani wao wameupenyeza mpaka kwenye biblia ambayo wewe unaringa nayo
Mmh kanisa la kwanza ni Katoliki mkuu hata mimi najua, lakini halikua hivi lilovyo sasa hapo mwanzoni kuna mabadiliko mengi ambayo hadi akina Padri Martin Luther walihoji nafikiri unakumbuka
 
Halafu Roman Catholic ni kwaajili ya Italy tu.Mmakonde,Mmachinga,Mmsai,Mchagga au Mnyakyusa na Catholic wapi na wapi !.Umewahi kuona au kusikia Pope Mwafrika au Mungu wa wa Catholic ni Mungu kwaajili ya wazungu pekee yake.
SASA hapa unamaanisha hata uislam mwisho makka na madina wengine wote wachawi Tu si ndio eehhh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…