Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Imani sahihi ni kumuabudu Mungu katika roho na kweli huku ukijiepusha na ibada za sanamu.

Kuwa na masanamu yaliyojaa makanisani mwenu ni ibada ya kishetani.

Kumuamini Mariam ni ibada ya kishetani. Mariam anaitwa Malkia wa Mvinguni katika Ukatoliki. Hii title ya Malkia wa Ulimwengu imekatazwa kutumika katika Biblia.

Yeremia 7:18
[18]Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.

Vile vile ukisoma Yeremia 44 :17-19

17 Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. 18Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa. 19 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimwandalia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mimiminiko, waume zetu wasipokuwapo?

Hizo ndizo ibada za sanamu zinazokatazwa.
Nasikia wakatoliki ndio wametengeneza hiyo biblia unayo refer. Thibitisha mtumishi.
 
never, Mungu hayupo kila mahali. Mungu anakaa mahali patakatifu. sasa kwa mfano, Mungu atakuwepoje katoliki wakati mnakataa kumpoke Roho kwa kujazwa na kunena kwa lugha, mnakataa uponyaji, badala ya kuomba kwa Jina la Yesu mnaomba kwa maria na wafu wengine? Mungu hayupo kwenye michanganyo kama hiyo ya dini. kumbuka, walipo wawili watatu wamekusanyika kwa Jina langu, mimi nipo papopapo katikati yao, the phrase "kwa Jina langu"ni muhimu sana. ninyi mnakutanika kwa majina ya wafu waliokufa na hawana lolote, mnakutanika kwa majina ya kina yosefu, kina Maria n.k, sio kwa Jina la Yesu. ndio maana Mung hayupo katikati yenu na hamtakuja kumwona mtakuwa mnamsikia tu.
Ukizungumzia wafu,ukumbuke hata Yesu alikufa.Sasa sijui utakunywa mchuzi wa maharage pekee au utabugia na maharage kabisa?
 
Kuabudu masanamu inahitaji uvumilivu sana
Ni nani aliyekudanganya Wakatoliki wanaabudu sanamu?

Kwa nini muwawekee watu maneno mdomoni?

Hebu pandisheni mizuka na muongee maneno yenu ya uongouongo.Eti...kundaraa bashartaayaaa kurduuum...!

Uongo mtupu kujidai mnanena kwa lugha.😂😂😂😂
 
Hapo ndipo umuhimu wa kuongozwa na Roho Mtakatifu unapoonekana.
Labda nikuulize swali.
Bikira Maria hakuna na watoto wengine wa kumlea Hadi akabidhiwe Yohana?

Angalizo.
Naomba hili swali lisijibiwe na Mkatoliki.
Naomba niongezee maneno baadhi kwnye swali lako ili ajibu vizuri zaidi..... '' bikra Maria hakuwa na watoto wengine mpk amkabidhi kwa Yohana ilihali pia mumewe Yusufu alikuwa bado yu hai? chapwa24
 
Nakusoma mkuu. Kanisa katoliki lina neema kubwa kwa maana ndo aliliacha Yesu. Tupo duniani na tumepewa kuchagua wema na ubaya tuko huru, kanisa aliliacha Yesu likiwa katika misingi lakini lilipita ktk changamoto nyiiingi saana mkuu watakatifu walikua wakiuwawa na serikali ya Kirumi na mwishowe wakasalenda zikaingizwa tamaduni za Kirumi katika kanisa mfano masanamu n.k na dola ya Kirumi ikalichukua kanisa rasmi na kulieneza duniani. Akina Mt Paulo na akina Mt Petro hawakuliacha kanisa na masanamu asee. Waliuwawa saana watakatifu na ma kaizari wa kirumi wew tafuta historia ndugu. Kaisari ambaye hakuuwa watakatifu ni Kaisari Kostantino tuu tena yeye ktk kipindi chake ndo aliweka tamaduni za Kirumi kanisani na mitanguso ikafuata mwisho ibada za wafu na kusali rozali mambo ambayo akina Luka hawakuyaacha. Utasema ni Roho mt ndo anamodify church that is not true, Roho Mt ni nafsi kamili ya Mungu na Mungu ni Mungu mwenye wivu hawezi kubali sanamu la Maria lipigiwe magoti katka ibada halafu watu wajifichamo waseme eti tunapiga magoti kuheshimu tuu wakati ni Jpili na watu wapo ibadani wanaabudu/wanasali
Walau nakushukuru Kwa kukiri kwamba Kanisa Katoliki ndilo alilolianzisha Yesu.
 
dini tuliletewa potofu ... wengine hatutaki kukubali tumepotoshwa eti unatetea dini. Jamani tumekua watu wazima na kule kubatizwa utotoni haikuwa ubatizo. Ubatizo ni pale unapoelewa na kukubali kwa hiari YAKO. Ndio maana Yahsua alibatizwa ukubwani, na kwa kuzamishwa...

Hivi mtawa ambae ameishi kuendana na sheria... akifariki atakuwa mtakatifu wa kuabudiwa na kuaminika amekaa karibu na Mungu kutuombea? Jamani mantiki wapi? Maria wa biblia alikuwa kama mfano wa huyu mtawa - binadamu alieishi vizuri mbele ya Mungu... yaani wale tunawaita walokole siku hizi.

HAPA CHINI NI AMRI ZA MUNGU KUTOKA BIBLIANI

Exodus (Kutoka) 20:3-17

3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.

4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

6 nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

7 Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.

8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;

10 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.

... SASA kweli, kama sote wakristo biblia ni moja, mwenzangu mkatoliki kweli huoni mstari wa 3 - 5 unatuambia rozari, sanamu za maria, uabudu wa maria hauendani na ukristo halisia??? mstari wa 8 - 10 hamuoni sabato ilikuwa ni amri ya kutobadilishwa ?
Sijaona kwenye hili andiko wanapokutaza kusali Rozari wala kumtumia Bikira Maria atuombee Kwa Mwanae.
Ninachokiona hapo ni Kuabudi miungu.
Yaani hairuhusiwi kukipa kiumbe chochote hadhi ya Mungu kama walivyofanya waisrael walipochonga Sanamu ya ndama na kusema ndio Mungu wao aliyewatoa utumwani misri.
 
Dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Mungu
Mungu sio maskini msimshushe Mungu wetu hata sehemu ya kumuabudu lazima iendane na utajiri wake
Unadharau makanisa ya mabati, hujui ibada unaweza fanya hata chini ya mti. Nani alikudanganya Mungu anapatikana kwenye makanisa ya maghorofa tu.
 
Siyadharau. Mungu anakuumba na akili timamu kabisa. Unaweza kujenga nyumba ya kuishi, unaweka fence, na kufuga mpaka mbwa kukulinda, lakini ibada unaona ukaifanye kwenye kanisa la mabati machakavu?

Watu mnapenda kufanya utani sana na imani.
Asante rafiki
 
Hapana mkuu ubatizo kwa Kiebrania maana yake ni kuzamisha. Sasa ukibatiza kwa kikombe maana yake hujazamisha mwili. Hata Yesu alizamishwa mwili katika maji na Yohane mbatizaji.
We anzisha uzi mwingine sio kudanganya watu hapa
Kwanza lugha ya hivo vitabu vilikuwa ni vya kiebrania au unakariri tu
 
Imani sahihi ni kumuabudu Mungu katika roho na kweli huku ukijiepusha na ibada za sanamu.

Kuwa na masanamu yaliyojaa makanisani mwenu ni ibada ya kishetani.

Kumuamini Mariam ni ibada ya kishetani. Mariam anaitwa Malkia wa Mvinguni katika Ukatoliki. Hii title ya Malkia wa Ulimwengu imekatazwa kutumika katika Biblia.

Yeremia 7:18
[18]Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.

Vile vile ukisoma Yeremia 44 :17-19

17 Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. 18Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa. 19 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimwandalia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mimiminiko, waume zetu wasipokuwapo?

Hizo ndizo ibada za sanamu zinazokatazwa.
Hata imani yako ni potofu according to imani zingine
 
Dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Mungu
Mungu sio maskini msimshushe Mungu wetu hata sehemu ya kumuabudu lazima iendane na utajiri wake
Je wewe kuna kanisa hata moja zuri ulilojenga ukakabidhi watu wakaanza kuabudu?
 
Nakusoma mkuu. Kanisa katoliki lina neema kubwa kwa maana ndo aliliacha Yesu. Tupo duniani na tumepewa kuchagua wema na ubaya tuko huru, kanisa aliliacha Yesu likiwa katika misingi lakini lilipita ktk changamoto nyiiingi saana mkuu watakatifu walikua wakiuwawa na serikali ya Kirumi na mwishowe wakasalenda zikaingizwa tamaduni za Kirumi katika kanisa mfano masanamu n.k na dola ya Kirumi ikalichukua kanisa rasmi na kulieneza duniani. Akina Mt Paulo na akina Mt Petro hawakuliacha kanisa na masanamu asee. Waliuwawa saana watakatifu na ma kaizari wa kirumi wew tafuta historia ndugu. Kaisari ambaye hakuuwa watakatifu ni Kaisari Kostantino tuu tena yeye ktk kipindi chake ndo aliweka tamaduni za Kirumi kanisani na mitanguso ikafuata mwisho ibada za wafu na kusali rozali mambo ambayo akina Luka hawakuyaacha. Utasema ni Roho mt ndo anamodify church that is not true, Roho Mt ni nafsi kamili ya Mungu na Mungu ni Mungu mwenye wivu hawezi kubali sanamu la Maria lipigiwe magoti katka ibada halafu watu wajifichamo waseme eti tunapiga magoti kuheshimu tuu wakati ni Jpili na watu wapo ibadani wanaabudu/wanasali
Kuwepo kwa sanamu katika nyumba za ibada kulianza hata kabla ya kuja kwa Yesu
Rejea waamuzi 17&18

Haya rejea tena[emoji116][emoji116][emoji116]

18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :18-22.)“

Ukipata mda tena rejea tena wakati sulemani alipokuwa akijenga hekalu mbona masanamu yalikuwepo 2Nyak 3&4

Na wakati wa kubariki hilo Hekalu, Mungu alilibariki likiwa na sanamu humo ndani
 
Watakwambia hiyo ilikuwa agano la kale.
Kwamba agano la kale Mungu alikuwa anakubali Sanamu ziabudiwe.
Ndio maana wakatoliki wanawapuuza na kuamua kukaa kimya.
 
Wasabato wao mafundisho yao makuu ni kumpinga papa na kumuita mnyawa wa chapa 666
Habari za wakati huu wapendwa
Katika dini zote au madhehebu yote au makanisa yote hakuna kanisa au waumini ambao wanaongoza kupigwa vita na kusemwa vibaya kama wakatoliki.

Ukienda kwenye mikusanyiko ya waislamu wanaopondwa ni wakatoliki ukienda kwenye mikutano ya injili ya walokole wanaopondwa na kusimangwa ni wakatoliki lakini huwezi kusikia wakijibizana na mtu.

Tangu nizaliwe hadi sasa sijawahi kusikia wala kuona wakatoliki wameandaa mkutano wa injili kuponda au kusimanga dini kinzani au dhehebu kinzani.

Isipokuwa wao mafundisho yao kwa watoto wa kimunio ya kwanza na kipaimara yamejikita katika kuufahamu ukatoliki na kuuelewa vizuri ndio maana ukikuta mkatoliki ameiva kabisa kwenye mafundisho huwezi ukamkuta anatetereshwa kwa mambo ya kijinga.

Wakatoliki wengi wao wamepewa mioyo ya uvumilivu ndio maana wanasimangwa sana kuhusu ubaya madhaifu yao lakini bado wapo imara na wameendelea kushikilia imani yao.

Huwezi ukakuta wakatoliki wanashawishi watu wahamie dini yao kwa kuwaambia madhaifu ya dini kinzani huwezi kukuta wakatoliki wapo mtaani wanahubiri au kwenye mabasi kisha kuwaambia watu watoe sadaka huwezi kukuta hiyo.

Ushauri wangu kwa dini na madhehebu mengine ni bora katika mafundisho yenu mjikite katika kuwaambia watu mazuri ya dini na madhehebu yenu ili kama mtu akivutiwa na mafundisho yenu awafate bila kuchafua dini za wenzenu.

Maana unaweza ukachafua dini/dhehebu la mwenzio siku na lako likija kuchafuliwa usianze kupaniki na kuanza kuleta maandamano ya kufunga barabara kwa kusema dini /dhehebu lako limechafuliwa.

Najua yapo mengi sana yanaongelewa huko mtaani kila dhehebu likisema ubaya wa dhehebu kinzani na wote ni mashahidi.
Kama wote lengo letu kufinga mbinguni muache afike kwa njia anayotaka yeye usimpangie njia ya kupita afike mbinguni.

Nilichogundua asilimia kubwa wanaohubiri kwa kuwachafua wenzao anataka wapate waumini tu ili SADAKA ziongezeke hakuna kingine.
 
tena waliunda JESUITS kwa ajili ya kufundisha elimu potofu na kwa makusudi... ili kuingiza mila za kirumi ndani ya kanisa, kuficha ukweli, kupotosha ukweli na kuliteka kanisa la Mungu. Mfano mzuri, wapagani wanamuabudu ISHTAR (ASTHARTE) NA MTOTO (TAMMUZ) ... walipoamrishwa kubadili dini kuwa wakatoliki - waliingiza hii mila kanisani wakibadili majina ya sanamu ya ISHTAR na mtoto kuwa ya Maria na mtoto - na kuendeleza uabudu wao. Hakuna sehemu ambayo biblia inasema Maria aabudiwe. Kwa miaka 300+ baada ya Yahsua (Yesu) kuondoka na kabla katoliki kuundwa, mitume wala waumini hawakuwa na mila hii.

Chunguza vile ambavo amri 10 zimeandikwa bibliani na vile zimeandikwa na katekisimo... wakristo biblia ni moja - niaje

Mkoloni mwenyewe hapa Tanzania alitumia elimu kupotosha...
Haya maneno tumeshaambiwa sana na walokole,wasabato lakini kwanini haya mantiki yoyote kwa wakatoliki?
Ni kwa sababu ya msingi imara wa imani uliojengwa kwenye mioyo yetu.
 
Ukizungumzia wafu,ukumbuke hata Yesu alikufa.Sasa sijui utakunywa mchuzi wa maharage pekee au utabugia na maharage kabisa?
Mkuu Yesu alikufa, akafufuka halafu akapaa mbinguni. Huyo Yesu alie katika wafu mpaka sasa siyo Yesu huyu tumzungumziaye Yesu Mnazareti
 
Walau nakushukuru Kwa kukiri kwamba Kanisa Katoliki ndilo alilolianzisha Yesu.
Hilo ni kweli na asiyekubali hilo ni kwamba tuu hajui. Ni kanisa la kwanza aliloliacha Yesu lakini lilipata mkengeuko
 
Waislamu siwezi kuwasemea lakini Wakristo wengine wanawashutumu Wakatoliki kwa sababu wanafundisha mambo ambayo ni unbiblical na mambo ambayo yalirithiwa kutoka katika desturi za Dini za Kipagani za Kirumi na Kiyunani
Mbona wao wakatolik hawawashutum hao wengn.. wako kimya tuu na wapole.. kwa akil ya kawaida unaona din ya kwel hapo ni ipi.. ile ya kusimanga wengne au?.. hahah.. ila pia akil.. wakatolik weng wana akil
 
Dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Mungu
Mungu sio maskini msimshushe Mungu wetu hata sehemu ya kumuabudu lazima iendane na utajiri wake
Mungu hana shida na utajiri wa mfuko wako, Mungu anachotazama haswa ni roho yako jinsi ilivyopondeka mbele zake.

Mahekalu makubwa na minara na nakshi za dhahabu siyo ishu saana kwake.

Unafikiri Nuhu alikua kwenye kanisa lenye mnara mkuubwa alipotoka kwenye gharika na akamfanyia Mungu ibada ya shukurani akatoa na sadaka? Building ni muhimu lakini siyo ishu saana
 
Back
Top Bottom