Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Ukristo ni mali ya Mwenyezi Mungu. Kabla ya wakatoliki ukristo ulikuwepo. Hizo unazoziita tamaduni za kale baadhi wanazo wayahudi hadi wa leo na wao hawamuamini Yesu kama mmoja wa watakatifu,pasaka na Christmas kwao ni siku za kawaida
Sitetei ukatoliki ila 99% ya ishu za kikristo ziliwekwa na wakatoliki nao walizitoa kwenye tamaduni za jamii za kale. Kwahiyo kwa ujumla ukristo ni mali ya wakatoliki labda niconclude hivyo
 
Hujawahi jibu kwa nini unabusu na kusujudu kuelekea jiwe, embu jibu
Nimeshajibu zaidi ya mara moja. Rejea utaona majibu.

Na hadithi ya swahaba Umar bin Khatwab nilikuwekea.
 
Unaweka maandiko kihuni na nusu nusu, nithibitishie kama hao walikuwa Waislamu.

Kingine onyesha katika hayo maneno ya Ibn Abbas wapi kawataja Waislamu ?
Suleiman Alie tajwa na Allah alikuwa muislamu au dini gani?

Koran 34:13. Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na masanamu.

Ibn Abbas, Koran 34:13 They made for him what he willed: synagogues and statues of angels, prophets and other righteous servants so that people look at them and follow their example of worshipping Allah,

Watu walikuwa wanaenda kwenye synagogue alizojenga Suleiman walikuwa dini gani?

Kisai njoo ujibu acha kujifanya hujaona maswali
 
Ukristo ni mali ya Mwenyezi Mungu. Kabla ya wakatoliki ukristo ulikuwepo. Hizo unazoziita tamaduni za kale baadhi wanazo wayahudi hadi wa leo na wao hawamuamini Yesu kama mmoja wa watakatifu,pasaka na Christmas kwao ni siku za kawaida
Nenda trace history ya kanisa lako, usipokutana na catholic basics ujue siyo ukristo.
 
Nimeshajibu zaidi ya mara moja. Rejea utaona majibu.

Na hadithi ya swahaba Umar bin Khatwab nilikuwekea.
Umar alipingana na Muhammad , Umar alilidharau jiwe , kwa hiyo unataka tumfuate Umar na tumpinge muhammad,

Ni vizuri ukajibu kwa nini unabusu jiwe nipo nasubiria majibu
 
Hapa ndipo mleta mada atakapopata majibu huwa mnajiona wamiliki wa madhehebu yote. Poleni sana
Nenda trace history ya kanisa lako, usipokutana na catholic basics ujue siyo ukristo.
 
Imani sahihi ni kumuabudu Mungu katika roho na kweli huku ukijiepusha na ibada za sanamu.

Kuwa na masanamu yaliyojaa makanisani mwenu ni ibada ya kishetani.

Kumuamini Mariam ni ibada ya kishetani. Mariam anaitwa Malkia wa Mvinguni katika Ukatoliki. Hii title ya Malkia wa Ulimwengu imekatazwa kutumika katika Biblia.

Yeremia 7:18
[18]Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.

Vile vile ukisoma Yeremia 44 :17-19

17 Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. 18Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa. 19 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimwandalia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mimiminiko, waume zetu wasipokuwapo?

Hizo ndizo ibada za sanamu zinazokatazwa.
Tatizo mnahisi tu au mnaaminishwa bila kujua ukweli. Ili kuelewa kuabudu sanamu ni nini ni lazima uelewe maana ya kuabudu kwanza kama hujui hilo basi usianze kupayuka payuka kuwa wakatoliki wanaabudu sanamu.

Kuwepo kwa picha, na sanamu kwenye kanisa hakumaanishi wakatoliki wanaabudu hivo vitu. (Tafuta kujua maana ya neno/tendo la kuabudu litakusaidia kwenye kumwelewa Mungu)
 
Mkuu hizo sherehe mbona hazina ukatoliki ndani yake. Yesu kristo sio mali ya wakatoliki pekee. Mwenyezi Mungu ni wa wote. Valentine ni udabwi udabwi tu wa kuongeza ka kibwagizi katika maisha.

Ungetaja sherehe za watakatifu wa kikatoliki zinazovamiwa na madhehebu mengine hapo ungeeleweka
Unafurahisha Sana[emoji23], tarehe 14/2 ni sikukuu ya mtakatifu Valentino au St. Valentine .....we mwenyewe si unaona dini zote zinasherehekea hiyo siku
 
Mkuu kama unakubali hizo ibada za kale basi chinjeni kabisa kondoo kanisani mteketeze kwa moto. Ndivyo ibada za kale waliruhusiwa
Hakuna andiko lolote katika agano Jipya linalosema pakiwepo na Sanamu Kanisa I ni ibada ya Sanamu.
Mungu Hana shida na Sanamu wala haziogopi.
 
Hio siku hakuna dini inayosherehekea kwa misa kanisani kama Pasaka, Christmas,Mwaka mpya

. Hio ni siku ambayo guest houses,hotel na sehemu za starehe zinajaa kwa wapendanao,wazinzi wa kila aina
Unafurahisha Sana[emoji23], tarehe 14/2 ni sikukuu ya mtakatifu Valentino au St. Valentine .....we mwenyewe si unaona dini zote zinasherehekea hiyo siku
 
Habari za wakati huu wapendwa
Katika dini zote au madhehebu yote au makanisa yote hakuna kanisa au waumini ambao wanaongoza kupigwa vita na kusemwa vibaya kama wakatoliki.

Ukienda kwenye mikusanyiko ya waislamu wanaopondwa ni wakatoliki ukienda kwenye mikutano ya injili ya walokole wanaopondwa na kusimangwa ni wakatoliki lakini huwezi kusikia wakijibizana na mtu.

Tangu nizaliwe hadi sasa sijawahi kusikia wala kuona wakatoliki wameandaa mkutano wa injili kuponda au kusimanga dini kinzani au dhehebu kinzani.

Isipokuwa wao mafundisho yao kwa watoto wa kimunio ya kwanza na kipaimara yamejikita katika kuufahamu ukatoliki na kuuelewa vizuri ndio maana ukikuta mkatoliki ameiva kabisa kwenye mafundisho huwezi ukamkuta anatetereshwa kwa mambo ya kijinga.

Wakatoliki wengi wao wamepewa mioyo ya uvumilivu ndio maana wanasimangwa sana kuhusu ubaya madhaifu yao lakini bado wapo imara na wameendelea kushikilia imani yao.

Huwezi ukakuta wakatoliki wanashawishi watu wahamie dini yao kwa kuwaambia madhaifu ya dini kinzani huwezi kukuta wakatoliki wapo mtaani wanahubiri au kwenye mabasi kisha kuwaambia watu watoe sadaka huwezi kukuta hiyo.

Ushauri wangu kwa dini na madhehebu mengine ni bora katika mafundisho yenu mjikite katika kuwaambia watu mazuri ya dini na madhehebu yenu ili kama mtu akivutiwa na mafundisho yenu awafate bila kuchafua dini za wenzenu.

Maana unaweza ukachafua dini/dhehebu la mwenzio siku na lako likija kuchafuliwa usianze kupaniki na kuanza kuleta maandamano ya kufunga barabara kwa kusema dini /dhehebu lako limechafuliwa.

Najua yapo mengi sana yanaongelewa huko mtaani kila dhehebu likisema ubaya wa dhehebu kinzani na wote ni mashahidi.
Kama wote lengo letu kufinga mbinguni muache afike kwa njia anayotaka yeye usimpangie njia ya kupita afike mbinguni.

Nilichogundua asilimia kubwa wanaohubiri kwa kuwachafua wenzao anataka wapate waumini tu ili SADAKA ziongezeke hakuna kingine.

Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana, kwa sababu boss wao anaishi vatican na kanisa ni mali ya vatican.​

Nimeshajibu zaidi ya mara moja. Rejea utaona majibu.

Na hadithi ya swahaba Umar bin Khatwab nilikuwekea.
Umar sawa yupo juu Sana

Maana Kuna Verse kadhaa za Koran katunga yeye , ila hili la jiwe tunataka kutoka kwa muhammad kwa nini mnabusu jiwe ,

Umar swala la jiwe alipinga Sana na kutofautiana na Muhammad
 
Ibada ya Sanamu ni Kuabudi kitu chochote na kukipa nafasi ya Mungu.
Au Kwa lugha nyepesi ni kutokutii maagizo ya Mungu na kujifanyia mambo yakupendezayo wewe mwenyewe.

Anayefikiri uwepo wa Picha Kanisani ndio ibada ya Sanamu Bado ana safari ndefu sana kumjua Mungu.

Wakolosai 3:5.
Basi, ueni chochote kilicho ndani yenu ambacho ni cha kidunia:
Uasherati,
uchafu,
shauku,
tamaa mbaya na
uchu

ambao ni kuabudu sanamu.

Kwa sababu ya mambo hayo hasira ya Mungu huwajia wote wote.
 
Ukristo ni mali ya Mwenyezi Mungu. Kabla ya wakatoliki ukristo ulikuwepo. Hizo unazoziita tamaduni za kale baadhi wanazo wayahudi hadi wa leo na wao hawamuamini Yesu kama mmoja wa watakatifu,pasaka na Christmas kwao ni siku za kawaida
Haya basi tafuta kitabu chako mwenyewe ili ukitumie nasio kutumia biblia ambayo ni mali ya kanisa katoliki
 
Nakubaliana na wewe lakini tulikatazwa kuabudu sanamu kwa Musa katika amri kumi. Halafu kumbuka sisi ni wa agano jipya. Mwisho utasema sasa ni halali kufanya sadaka za kuteketeza leo kisa zamani zilifanywa
Kumbe unajua kuwa tulikatazwa kuabudu sanamu.

Pia kanisa katoliki haliabudu sanamu au wewe umeona wapi linaabudu sanamu
 
Unaweka maandiko kihuni na nusu nusu, nithibitishie kama hao walikuwa Waislamu.

Kingine onyesha katika hayo maneno ya Ibn Abbas wapi kawataja Waislamu ?
Ungejibu kwa nini Allah alituma majini yakatengeneza masanamu na yakaweka msikitini na kutengeneza pia mabeseni ya kutawazia

Koran 34:13. Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na masanamu, ...........
Ibn Abbas, Koran 34:13 They made for him what he willed: synagogues and statues of angels, prophets and other righteous servants so that people look at them and follow their example of worshipping Allah,

Na ujibu pia lini Allah alisema yasiwekwe tena na kwa nini?
 
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]Wapi imeandikwa hivyo
Ukitakwa iandikwe wapi
Ni kina nani walifanya kazi ya kuchagua baadhi ya vitabu ambavyo waliviweka humo kwenye biblia ambavyo wewe leo unatumia
 
Habari za wakati huu wapendwa
Katika dini zote au madhehebu yote au makanisa yote hakuna kanisa au waumini ambao wanaongoza kupigwa vita na kusemwa vibaya kama wakatoliki.

Ukienda kwenye mikusanyiko ya waislamu wanaopondwa ni wakatoliki ukienda kwenye mikutano ya injili ya walokole wanaopondwa na kusimangwa ni wakatoliki lakini huwezi kusikia wakijibizana na mtu.

Tangu nizaliwe hadi sasa sijawahi kusikia wala kuona wakatoliki wameandaa mkutano wa injili kuponda au kusimanga dini kinzani au dhehebu kinzani.

Isipokuwa wao mafundisho yao kwa watoto wa kimunio ya kwanza na kipaimara yamejikita katika kuufahamu ukatoliki na kuuelewa vizuri ndio maana ukikuta mkatoliki ameiva kabisa kwenye mafundisho huwezi ukamkuta anatetereshwa kwa mambo ya kijinga.

Wakatoliki wengi wao wamepewa mioyo ya uvumilivu ndio maana wanasimangwa sana kuhusu ubaya madhaifu yao lakini bado wapo imara na wameendelea kushikilia imani yao.

Huwezi ukakuta wakatoliki wanashawishi watu wahamie dini yao kwa kuwaambia madhaifu ya dini kinzani huwezi kukuta wakatoliki wapo mtaani wanahubiri au kwenye mabasi kisha kuwaambia watu watoe sadaka huwezi kukuta hiyo.

Ushauri wangu kwa dini na madhehebu mengine ni bora katika mafundisho yenu mjikite katika kuwaambia watu mazuri ya dini na madhehebu yenu ili kama mtu akivutiwa na mafundisho yenu awafate bila kuchafua dini za wenzenu.

Maana unaweza ukachafua dini/dhehebu la mwenzio siku na lako likija kuchafuliwa usianze kupaniki na kuanza kuleta maandamano ya kufunga barabara kwa kusema dini /dhehebu lako limechafuliwa.

Najua yapo mengi sana yanaongelewa huko mtaani kila dhehebu likisema ubaya wa dhehebu kinzani na wote ni mashahidi.
Kama wote lengo letu kufinga mbinguni muache afike kwa njia anayotaka yeye usimpangie njia ya kupita afike mbinguni.

Nilichogundua asilimia kubwa wanaohubiri kwa kuwachafua wenzao anataka wapate waumini tu ili SADAKA ziongezeke hakuna kingine.
Sasa wakatoliki si ndio hua wanajitapa kua wao ndio dini ya kwanza kuanzishwa na Mungu 😂😂,huku wakiwakejeli wenzao eti vidini vya juzijuzi..

Acha na wao wapigwe mambo tu kudaadeki zao
 
Back
Top Bottom