Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

dini tuliletewa potofu ... wengine hatutaki kukubali tumepotoshwa eti unatetea dini. Jamani tumekua watu wazima na kule kubatizwa utotoni haikuwa ubatizo. Ubatizo ni pale unapoelewa na kukubali kwa hiari YAKO. Ndio maana Yahsua alibatizwa ukubwani, na kwa kuzamishwa...

Hivi mtawa ambae ameishi kuendana na sheria... akifariki atakuwa mtakatifu wa kuabudiwa na kuaminika amekaa karibu na Mungu kutuombea? Jamani mantiki wapi? Maria wa biblia alikuwa kama mfano wa huyu mtawa - binadamu alieishi vizuri mbele ya Mungu... yaani wale tunawaita walokole siku hizi.

HAPA CHINI NI AMRI ZA MUNGU KUTOKA BIBLIANI

Exodus (Kutoka) 20:3-17

3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.

4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

6 nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

7 Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.

8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;

10 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.

... SASA kweli, kama sote wakristo biblia ni moja, mwenzangu mkatoliki kweli huoni mstari wa 3 - 5 unatuambia rozari, sanamu za maria, uabudu wa maria hauendani na ukristo halisia??? mstari wa 8 - 10 hamuoni sabato ilikuwa ni amri ya kutobadilishwa ?
 
Mmh kanisa la kwanza ni Katoliki mkuu hata mimi najua, lakini halikua hivi lilovyo sasa hapo mwanzoni kuna mabadiliko mengi ambayo hadi akina Padri Martin Luther walihoji nafikiri unakumbuka
Kwaiyo unataka kusema Roho Mtakatifu hajui kazi yake anabaisha tu Maana yake kila siku amtokee mtu aanzishe kanisa lake

Mt 16:18 SUV

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

Kanisa ni moja tu
 
Mkuu hujanielewa, muda wa watakatifu kutawala bado mkuu. Badoo mkuu..baaado. Hadi Yesu aje mara ya pili ndo watakatifu watatawala pamoja nae. Game badoo hilii, hadi arudi kuwahukumu wazima na wafu ndo tutatawala pamoja nae au umesahau ile sala ya kuhukumu wazima na wafu hahaaa. Akina mtakatifu mashahidi wa Uganda hawana msaada wowote na maombi yetu Bro wame chill tuu. Ni jina la Yesu tuu. Vamiwa na pepo halafu uite shahidi wa Uganda akusaidie wapi na wapi. Lakini kwa triki ya shetani unaweza kuita mt shahidi wa Uganda na pepo litoke ili uamini shahidi na uzidi kupotea
Naona sasa unajitungia vifungu vya kwako
 
Zilongwa mbali zitendwa mbali sasa kama wao waliamua kitabu kipi kiwepo kipi kisiwepo sasa wangeshindwa kubadilisha

Bado ukaona haitoshi unatumia kitabu hiko hiko ambao ni zao lao kuwasema

Nakusihi tafuta chako afu uje hapa
Kipindi hicho kanisa lilikua bado la moto hivyo maandiko hayakubadilishwa, mitanguso ndo ilikuja kuharibu mengi saana. Tizama hata ubatizo wa Kikombe kanisani badala ya ubatizo wa maji mengi mkuu ni kitu ambacho kilibadilishwa na hawa makasisi wetu wa kanisa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kwani kuna uhalali wowote wakubatizwa na maji mengi kama vipi anzisha uzi mwingine
 
Yesu aliwatuma mkabatize kwa maji mengi????.

Na kuna watu walibatizwa nyumbani kwao sasa sijui kulikuwa na mito
 
Kipindi hicho kanisa lilikua bado la moto hivyo maandiko hayakubadilishwa, mitanguso ndo ilikuja kuharibu mengi saana. Tizama hata ubatizo wa Kikombe kanisani badala ya ubatizo wa maji mengi mkuu ni kitu ambacho kilibadilishwa na hawa makasisi wetu wa kanisa
Kanisa ni Moja tu
Naye Roho mtakatifu kazi yake ni kukarabati

Mt 16:18 SUV

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
 
Kwaiyo unataka kusema Roho Mtakatifu hajui kazi yake anabaisha tu Maana yake kila siku amtokee mtu aanzishe kanisa lake

Mt 16:18 SUV

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

Kanisa ni moja tu
Nakusoma mkuu. Kanisa katoliki lina neema kubwa kwa maana ndo aliliacha Yesu.

Tupo duniani na tumepewa kuchagua wema na ubaya tuko huru, kanisa aliliacha Yesu likiwa katika misingi lakini lilipita ktk changamoto nyiiingi saana mkuu watakatifu walikua wakiuwawa na serikali ya Kirumi na mwishowe wakasalenda zikaingizwa tamaduni za Kirumi katika kanisa mfano masanamu n.k na dola ya Kirumi ikalichukua kanisa rasmi na kulieneza duniani.

Akina Mt Paulo na akina Mt Petro hawakuliacha kanisa na masanamu asee. Waliuwawa saana watakatifu na ma kaizari wa kirumi wew tafuta historia ndugu.

Kaisari ambaye hakuuwa watakatifu ni Kaisari Kostantino tuu tena yeye ktk kipindi chake ndo aliweka tamaduni za Kirumi kanisani na mitanguso ikafuata mwisho ibada za wafu na kusali rozali mambo ambayo akina Luka hawakuyaacha.

Utasema ni Roho mt ndo anamodify church that is not true, Roho Mt ni nafsi kamili ya Mungu na Mungu ni Mungu mwenye wivu hawezi kubali sanamu la Maria lipigiwe magoti katka ibada halafu watu wajifichamo waseme eti tunapiga magoti kuheshimu tuu wakati ni Jpili na watu wapo ibadani wanaabudu/wanasali
 
Naukitaka kumuona mungu kwaharaka nenda kwazumaridi sie kwetu dini nizaidi yamiujiza ambayo ndio chambo yamanabii wauongo kuwateka mana wanajua mnapenda miujiza
ukweli ni kwamba, ipo miujiza ya kweli kabisa inayofanywa kwa JIna la Yesu sawaswa na maelekezo ya Yesu mwenyewe. vilevile ipo miujiza ya shetani ambaye siku zote huwa anajiedit ili afanya vitu vinavyofanana na vya kimungu ili kupotosha watu.

watu kama wewe wameshapotoshwa tayari na shetani na ameshafanikiwa kukudanganya kwamba, kwasababu wapo watu wa kishetani kama zumaridi na wengine kadhaa, basi miujiza sio ya muhimu na hakuna miujiza halali. dini ndio ya mhimu kwako.

jambo hili ni hatari sana kwenye ustawi wa ukristo duniani. na hata hivyo, kanisa katoliki haliamini matendo makuu ya Mungu, na hayajawahi kudhihirishwa na watu wa kanisa hilo.

kama Yesu aliponya, na sisi tunategemewa tuponye, unachoita wewe miujiza, kwa upande mwingine ni huduma ya Yesu mwenyewe. kwasababu kuna kufanya miujiza watu wamwamini Mungu hasa wale wenye imani haba, na kuna kufanya miujiza kama huduma ya kawaida kabisa ya Yesu hapa duniani ambayo poa alituachia waamini kwamba kwa Jina lake tutaponya wagonjwa, tutafufua wafu na kukemea pepo. katholic hata kukemea pepo hamuwezi sasa ni Yesu yupi mnayemwamini?

mwisho, kina zumaridi na wengine hao wote walishakuwa denounced na makanisa ya kilokole zamani sana, kwasababu wanafuata ushetani. na pia uwepo wa hao haumaanishi hakuna matendo makuu ya Mungu hapa duniani.

uwepo wa shetani haimaanishi Mungu hayupo.
 
Ila waumini wa free church yamasanja mna mbwembwe sana
free church ya masanja ni aina nyingine ya upotoshaji wa Neno la Mungu, shetani anaweka matawi mbalimbali hapa duniani, catholic na free church ni miongoni mwao. la mc kipilipili.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kwani kuna uhalali wowote wakubatizwa na maji mengi kama vipi anzisha uzi mwingine
Hapana mkuu ubatizo kwa Kiebrania maana yake ni kuzamisha. Sasa ukibatiza kwa kikombe maana yake hujazamisha mwili. Hata Yesu alizamishwa mwili katika maji na Yohane mbatizaji.
 
Kanisa ni Moja tu
Naye Roho mtakatifu kazi yake ni kukarabati

Mt 16:18 SUV

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Hata Mungu alipowaumba Adamu na Eva hakutaka wakengeuke lakini ni wao tuu ndo walikengeuka. Hata kanisa vivyo hivyo mkengeuko wake haupangwi na Mungu ni watu wenyewe kupigwa na nguvu za adui, Yesu aliliacha kanisa saafi chini ya Mt Petro lakini ndo hivyo tena mambo yashakua mengi
 
sahihi kabisa. na kama Mungu ni Roho, wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. ukimwabudu kimwili kamwe hautamwona kwasababu Mungu haonekani kimwili, na hata hivyo mwili ndio adui mkubwa wa roho.
there you are.

Yesu ndiye Bwana.
 
binafsi huwa nashangaa sana nikihudhuria misiba, padre au askofu akiwa pale mbele akianza kuhubiri, hakuna hata tone la nguvu za Mungu, hata harufu tu ya uwepo wa Mungu haipo, mahubiri makavuuuu yasiyookoa. kusali dini inahitaji uvumilivu sana na ni kifungo kikubwa mno.
Kwa hiyo unapendelea mapadre wawe wanapandisha mizuka wanapohubiri?Halafu na weye ukishikwa midadi ujitupe chini,kugalagala na kupiga mayowe ndiyo sala zinakuwa na Roho wa BWANA?Acheni utapeli huo!😂😂😂😂😂
 
Wa kwanza kujiona wapo karibu na Mungu ni walokole.Na kwa uchokozi hawajambo.Mara sanamu imefanya hivi mara vile.Hawatulii.Wanafuata akina ...!
 
Back
Top Bottom