Upo sahihi mkuu kuna uwezekano mimi ni mjinga.
Mkuu mimi nimezaliwa na wazazi wanaoabudu kanisa la Roma kwa hiyo kama ni kutumia assets za kiroma basi ndo zimenikuza na kunifikisha hapa nilipo.
Nimezaliwa katika hospital ya Huruma inamilikiwa na shirika la Roman Catholic la ma sister wa st Joseph Rombo.
Nimesoma shule ya st Ritaliza primary school Kilimanjaro.
Secondary nikasoma st Amedeus Kilema Kilimanjaro mpaka advance.
Chuo kikuu nikasoma The Catholic University of Health and Allied Sciences - Bugando (CUHAS-BUGANDO)
Kituo changu cha kazi ni Consolata Hospital Ikonda-Makete.
Mke wangu na yeye alilelewa kituo cha watoto yatima St.Francis Boma Hai.
Kanisa la Roma ni zaidi ya kusali. Ni sehemu ya maisha ya waumini wake.
Kanisa la Roma halina ule utaratibu wa maombi na kununua mafuta.ila ukiumwa utaelekezwa hospital. Na kanisa hili lina hospital za kisasa nchi nzima. Ni kanisa linalosimamia misingi ya sayansi kuliko unavyoweza kufikiria.
Kanisa la Roma pia linaamini sana katika elimu. Kanisa hili limeweza ku survive miaka yote hii kwa sababu ya kuwekeza katika elimu. Ndo maana inavyuo mbalimbali nchi nzima
SAUT, ST.JOHN DODOMA ETC.
Kanisa hili pia halipo nyuma katika financial institutions lina MKOMBOZI BANK.
Kanisa Catholic halikusimamii wewe kwenda mbinguni tu ila linahitaji pia kuhakikisha unapata mahitaji yako muhimu kwa ubora kabisa.
View attachment 2148261