hatuongei ili kuwakashifu, hatuongei ili kuwadharau, hatuongei ili kuwatukana, tunaongea ili kuwasaidia mfumbuke macho pengine mtaponya roho zenu.
1. Kanisa aliloanzisha Paulo/Pwetro au mitume wowote wale, halifanani kabisa na ukatoliki, kwasababu makanisa ya mitume yalitembea na Nguvu za Mungu. Yesu alipopaa aliwaelekeza wanafunzi wake kwamba enenedi mkawafanya mataifa yote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa JIna la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuri ninyi, na tazama mimi nipo pamoja nany hata ukamilifu wa dahari. mojawapo ya mafundisho ya Yesu ni kwamba, wakati wa kuhubiri injili tunatakiwa kuponya wagonjwa, kufufua wafu, kutakasa wenye ukoma, na tunatakiwa kufanya hivyo bure bila malipo.(ndio maana siku zote napinga wachungaji wanaotoza waumini ili wawaone au kuuza bidhaa kama njia ya kuwaona).
hakuna padre wala askofu wala papa wa kiroma mwenye uwezo wa kuponya wagonjwa, kufufua wafu au kutakasa wenye ukoma. hakuna padre wala yeyote wa aina hiyo anayetembea na Nguvu za Mungu kwasababu ili uwe nazo lazima ujazwe Roho Mtakatifu ambaye wakatoliki wanampinga, wanakataa kujazwa Roho na kunena kwa Lugha.
kanisa la kwanza, lilelile ambalo ndio kina Paulo na Petro walilijenga kule St.Peter Roma Italia, walizingatiwa uongozi wa Roho na kuomba kwa Jina la Yesu, hawajawahi kuomba kwa Maria au Mtakatifu yosefu n.k, pia katika vitabu vyote vya manabii mitume walifanya reference, hautakuja kukuta vitabu kama vya Maccabean n.k,