Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Halafu Roman Catholic ni kwaajili ya Italy tu.Mmakonde,Mmachinga,Mmsai,Mchagga au Mnyakyusa na Catholic wapi na wapi !.Umewahi kuona au kusikia Pope Mwafrika au Mungu wa wa Catholic ni Mungu kwaajili ya wazungu pekee yake.
Sio kweli. "Katoliki" ni dhehebu katika imani ya kikristo lenye kutawala duniani kote. Katika mataifa yote ulimwenguni kuna waamini wa imani ya kikristo kupitia dhehebu hili.

By "Roman Catholic" means that catholicism is originally initiatied in Rome (Italy) and later did spread across the world.

Hivyobasi: Roman Catholic: Ukatoliki/mkatoliki wa asili ya Rome, Italy. Na kwa wengineo tuna Tanzanian catholics, Greek catholics, Polish catholics, Ugandan catholics nk.
 
Ibada ya sanamu ni ile ya kuipigia magoti sanamu ya bikira maria huku ukijua ile ni sanamu haioni wala kusikia huo ni utaahira kabisa
Kunakutengeneza sanamu na kuziabudu.
Mungu alikataa kutengeneza samu na kuziabudu. Ndiyo maana hapo chini alimwamuru Musa atengeneze nyoka sanamu ya nyoka wa shaba. Ili atakaemuangalia kwa Imani atapona. Hii haikuwa na maana ya Kuwa walikuwa wanaabudu na kusujudu Sanamu ya Nyoka wa shaba.

Hesabu 21:8-9
[8]Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.
[9]Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

Pia Mungu alimwamuru Mussa atengeneze sanamu za Makerubi(Malaika) na kuziweka mahara Patakatifu PA Patakatifu lilipokaa Sanduku la Agano. Je Mungu alikuwa anavunja Amri yake aliyoitoa mwenyewe ya kutengeneza sanamu???. Jibu ni laaa Bali hataki kuabudu sanamu siyo kutengeneza tu.
Wakatolic hatuabudu sanamu Ila tunasanamu mbalimbali katika kanisa Kama ilivyo sanamu katika Sanduku la Agano la Mussa.

Kutoka 25:18-20
[18]Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku.
[19]Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.
[20]Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema.


Tumekatazwa kuabudu sanamu na kuzisujudia ndivyo amri ya kwanza ya Mungu inamaana Usiabudu miungu mwingine. Miungu mingine ndiyo sanamu, na vitu vingine vinavyopewa Nafasi ya Mungu. Na wakatolic hatuzipi sanamu Nafasi ya Mungu wetu.

Kwa kufundishwa kwa kupotoshwa.
Tumsifu Yesu Kristo.
 
Eeh Yani petro mwanafunzi wa Yesu unasema ndio alikua papa?

Aisee Yaani Yesu ndio alikuja duniani kutoka mbinguni kuja kuwaambia mkaanzishe kanisa litakaloitwa katoliki?


Aisee si comment tena

hatari sana hii
Unafahamu history ya Ukristo ulivyoanza??. Ulianzishwa lini na Nani?. Viongozi wa awali wa Ukristo ni akina Nani??? na walikuwa wapi wakati wanaanzisha ukristo????. Ukifahamu majibu ya maswali hayo huwezi piga kelele sana
 
Waumini wake ni sehemu ya taasisi kwa hiyo hawana muda wa kuanza kujibizana na walokole ni kupoteza energy.
Waseme nini hao RC na ukweli uko wazi??? Yesu Mzungu Kamwe haji ng'ooo!! mtasubiri sana!! Waafrica wa leo wamejanjaruka hee!! acha kabisa!!...tena wamesomaaaa!! kuliko wazungu!! yaani akili sasa hivi tunazo tuna wahesabia tu!!

Islam, RC Vatican yooote ile!!, Anglicans nk!! hao baba ndo walishadadia biashara ya utumwa!! na weusi hawakuruhusiwa kusali sababu watajijua kuwa wao ndo kabila teule la Mungu, tena mkauzwa hasa! sababu ya kumuudhi Mungu!

hayoo hayo!! wenye rangi na sura ya yesu!! ndo wabaguzi hatare, watengeneza dhana za kuulia watu na wakoloni wabaya!! watibuaji wa amani Duniani!! km leo Ukrain!! kifupi wanajua kuwa sisi weusi sasa hivi tunajua uongo wao!..ili wao wale!!

hao hao ndo wakoloni Mambo leo!! ni aibu sana tena ya kudhalilika mnoo!! Mwafrica mweusi kuabudu kanisa la wakoloni!! wabaguzi mpaka leo! yaa sasa hivi ukienda vatican hawakuchangamkii!! wanaona ni Jibwa Jeusi tu!! lina anika umaskini! Lipo hapa ajili ya shida tu!

Kule Vatican Makasisi, Mapadre, Ma-sisister weusi wana kazi sana kwa ku dharauliwa kule!! km una damu ya kichifu bin kimapinduzi kamwe huwezi kanyaga Vatican au kufanya ile kazi!.....na ndo maana wengi wanaofanya zile kazi ni wale wenye damu za kimaskini sana!

tena na elimu nusu sana ya kukaririshwa na wao!! km padre karugendo na marehehmu Rugambwa!! Nyerere mtoto wa chief alikataa katakata!! lkn alikufa akimalizia research yake kwao!!

Babu zetu wa kale! na baba zetu hatu walaumu kiviile sababu wao hawakujua kuhusu hili!! lkn kijana/Mtu mzima wa kuanzia miaka 70 kuja huku nikikukuta kanisani tena RC ntacheka mpaka nijambe kifukuto!!...Km umesoma nakuua maksudi!!

Wasomi huru gerezani hawaendi kanisani km Sarungi ni Msabato yule Mzee!!lkn ukimwambia hizo habari hakuelewi!! zamani za ujima nilidhani wana kiburi tu! kuuumbe mie ndo nilikuwa huru gerezani!!

Mtu mweusi kwenda kusali kanisa la RC ni udhalili wa hali ya juuu sana!! tena uliopitiliza kabisaaa! Baadhi ya weusi wa kule USAwakikuona unaenda huko sali?? hee! wana kuchinja live! ukienda kusali huko!!

eti nao hao wazungu wenyeji wa Vatican wanawachukia wayahudi Wazungu!! kisa ni etiiii!!.... walimuua na kumkana Yesu wa Nazareth basi nachekaaaga mpaka nayamba kifukuto karibia kupasuka!...ni udhalili mweusi kuabudu mzungu hadi leo!!

wao walipiga mahesbau kuwa!! Mweusi atajanjaruka baada ya miaka mitano tu ya uhuru yaani 1970 huko!!....ili wabadirishe mipago yao ya ukimadehehebu, ili bbadae huko yawe ni Mashirika ya Misaada!! Mweee!! lkn wapi ndo kwaaanza wanabatizwa! mpaka leo!

Niseme tu yesu mzungu haji ng'ooo mtasubiri sana!! ....kuuumbe wenzenu yYesu wao kapita hivi kawabeba!
 
Nilibahatika kusoma katekisimu kubwa ya wakatolic ikanifanya kuapa sitatoka katolic
Ukiona mtu anakimbia Kanisa ujue ni ubinafsi wa kibinadamu tu, anahisi yeye ni bora kiroho. Most of them are poorly Catechised.

Baada ya kipaimara haujawekwa mfumo bora wa mafundisho mapana ya Kanisa. Lakini pia kuongeza ukaribu kati ya waamini na makuhani wao ili mtu anapopata tatizo iwe rahisi kumfikia kuhani. Hii imeboreka sana siku hizi hasa pia social media zimesaidia sana.

Otherwise bado ni wajibu wa kwanza kiroho ni muumini mwenyewe kutafuta uso wa Mungu na kuitafuta kweli. Siku hizi hakuna tena kisingizio, kila kitu kipo mitandaoni, site za Kanisa zipo nyingi, njia za kujifunza ni bidii yako maana ufalme wa Mungu utatekwa na wenye nguvu! Ukilegea usilaumu mtu, siku ukipata wimbi unaanza kuhaa kwenye makanisa kama kwa waganga wa kienyeji.
 
Halafu Roman Catholic ni kwaajili ya Italy tu.Mmakonde,Mmachinga,Mmsai,Mchagga au Mnyakyusa na Catholic wapi na wapi !.Umewahi kuona au kusikia Pope Mwafrika au Mungu wa wa Catholic ni Mungu kwaajili ya wazungu pekee yake.
Soma list ya mapapa (pope) utaona wapo waafrika zaidi ya 5 tangu kanisa katoliki lianze
Usiwe mvivu kusoma na kuchunguza mambo kwa kina.
 
Kanisa Katoliki lilianzishwa na Mitume Kwa Maelekezo ya Yesu.
Mtume Petro ndie Papa wa Kwanza na alifia na Kuzikwa Vatican yalipo makao makuu ya Kanisa.
Hakika[emoji1488][emoji1488][emoji1488][emoji1488][emoji1488][emoji1488]
 
Tunautakatifuza ulimwengu, hatuna muda wa kunyangana waamini. Wanawarubuni kwa kuliponda Kanisa alafu after sometimes wanarudi! Wanabaki ambao ngome ya uongo juu ya mafundisho ya Kanisa imegandamana nao!

Mkuu mtazamo ilikuaje kanisa katoliki likaanzisha ubatizo wa kunyunyiza maji tofauti na ilivyokuwa kwenye kanisa la mwanzo ambapo maandiko ya biblia yanaeleza kuhusu ilivyokuwa inafanywa kwa kuzamisha kwenye maji mengi. Nini asili ya hii aina ya ubatizo?
 
Hakuna andiko lolote katika agano Jipya linalosema pakiwepo na Sanamu Kanisa I ni ibada ya Sanamu.
Mungu Hana shida na Sanamu wala haziogopi.
Mkuu au haujui sanamu ni kitu gani au ni mpaka yachongwe na wamakonde ndo muite sanamu.

1 Corinthians 10:14
[14]Wherefore, my dearly beloved, flee from idolatry.

Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.
 
Kanisa la Roma lina miaka 2000 toka limeanzishwa.
Hivi mtu mwenye umrinwa miaka 2000 atabishana nini na mtu aliyeanzisha karne ya 20?

Kanisa la Roma limewekeza kwenye
elimu ndo maana wana shule na vyuo vikuu vya kutosha nchi nzima.
Afya
Kanisa la Roma lina hospital na dispensary nchi nzima.

Fedha
Kanisa la Roma lina Mkombozi bank.
Kanisa la Roma ni taasisi imara na kongwe kabisa.

Waumini wake ni sehemu ya taasisi kwa hiyo hawana muda wa kuanza kujibizana na walokole ni kupoteza energy.
Very poor reasoning capacity.
 
Hakuna andiko lolote katika agano Jipya linalosema pakiwepo na Sanamu Kanisa I ni ibada ya Sanamu.
Mungu Hana shida na Sanamu wala haziogopi.
Mnayapigia magoti na kuyabusu hayo manasesere kanisani
 
Unafahamu history ya Ukristo ulivyoanza??. Ulianzishwa lini na Nani?. Viongozi wa awali wa Ukristo ni akina Nani??? na walikuwa wapi wakati wanaanzisha ukristo????. Ukifahamu majibu ya maswali hayo huwezi piga kelele sana
Mnachekeshaga sana.
 
Wakatoliki wengi huwa wana akili.

Ila wa kwenye huu uzi ni wakatoliki wasiotumia akili kabisa duniani.

Eti Biblia ni mali yenu? Na ukristo ni mali yenu?

Kauli za kijinga kabisa kuwahi kuonekana tangu jamiiforums izaliwe.

Nimewadharau sana nyie jamaa. Tubuni sasa muache huo ufala

Acha kulialia mlamu, kama sio mali yao sema basi ni mali ya nani sio kukimbilia kutia huruma….. hizo 'tuition centers' zenu zote zimechukua [zimekopi] notisi kwa katoliki.
 
Ibada ya Sanamu ni Kuabudi kitu chochote na kukipa nafasi ya Mungu.
Au Kwa lugha nyepesi ni kutokutii maagizo ya Mungu na kujifanyia mambo yakupendezayo wewe mwenyewe.

Anayefikiri uwepo wa Picha Kanisani ndio ibada ya Sanamu Bado ana safari ndefu sana kumjua Mungu.

Wakolosai 3:5.
Basi, ueni chochote kilicho ndani yenu ambacho ni cha kidunia:
Uasherati,
uchafu,
shauku,
tamaa mbaya na
uchu

ambao ni kuabudu sanamu.

Kwa sababu ya mambo hayo hasira ya Mungu huwajia wote wote.
Exodus 20:4-5
[4]
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
[5]
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
 
Kumbe unajua kuwa tulikatazwa kuabudu sanamu.
Pia kanisa katoliki haliabudu sanamu au wewe umeona wapi linaabudu sanamu
Mkuu twende kanisa la mt Yosefu pale posta kesho tutajionea kwa macho ibada za sanamu
 
Waislamu walikuwa wanayaangalia masanamu ya malaika , mitume na watumishi watiifu ili wamuabudu allah
Koran 34:13. Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na masanamu, ...........
Ibn Abbas, Koran 34:13 They made for him what he willed: synagogues and statues of angels, prophets and other righteous servants so that people look at them and follow their example of worshipping Allah,

Haya masanamu allah aliyaweka kwenye msikiti wa suleimani wake , je unaweza kuniambia lini allah alikuja kukataza kuweka masanamu msikitini?
We kafiri kama kawaida yako kuchafua mada. Hapa wanazungumzia kuhusu Catholic church. Anzisha uzi mwingine tukujibu. Bila kusahau lile swali ambalo ulishindwa kujibu kuhusu ujinga wa Mungu anayezungumzia paulo

1 Wakorintho

25 Kwa maana huu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, na ’udhaifu’ wa Mungu una nguvu ipitayo nguvu ya wanadamu.
 
Exodus 20:4-5
[4]
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
[5]
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Umeshaelezwa sana tu kuwa kuwepo na sanamu katika kanisa haimaanishi kuwa vinasujudiwa ila sijui unataka nini?

Tumeshakupa mifano kadhaa kwenye hekalu kulikuwa na sanamu mbona Mungu aliyabariki hayo mahekalu wewe ni nani ambaye unamzidi Mungu
 
Back
Top Bottom