Wauza mchele, weka changamoto zenu hapa tusaidiane kuzitatua

Kwahiyo huko uliko mpunga unapatikana kwa wingi kwasasahivi?
Wingi wa Mpunga ni hela yako tu ila kipindi kizuri ni pale wakulima wakiwa wanavuna. Kwa sasa kipindi cha mavuno kwa Ifakara kimeelekea mwishoni maana wakulima wengi walishapiga mpunga upo ndani, hivyo upatikanaji wake si kwa wingi sana kama ilivyokuwa kuanzia June-August.
 
Kwa mfano nikinunua mchele mashineni afu naupaki tu baada ya muda ntapata matajiri wa kuninunulia mchele huo ukiwa hapohapo mashineni bila ya mimi kuusafirisha mpk dar au kwengineko panapo masoko
 
Kwa mfano nikinunua mchele mashineni afu naupaki tu baada ya muda ntapata matajiri wa kuninunulia mchele huo ukiwa hapohapo mashineni bila ya mimi kuusafirisha mpk dar au kwengineko panapo masoko
Unapata kaka
 
Kwa sasa kuna mgomo wa wanunuzi juu ya ushuru kuwa hii serikali sijui tunaelekea wapi kutoka kwenye 2000 kwa gunia mpaka 4500 inaelekea 5000 saivi
Hizi pesa wanazochukua zinatumia vipi katika kuboresha chochote kile kwenye mzunguko wa hiyo biashara? Yaani gunia 10 ushuru Tsh 50,000? Hela ambayo mfanyabiashara mwenyewe anaihitaji sana tu.


Ama kweli ukiweza kukwepa kodi, basi utajiri unakufuata, maana ukikwepa ushuru wa magunia 100 tu (5000*200) tayari unafaida ya 1,000,000 sokoni kabla hata ya kuuza.
 
Wewe ni mwenyeji wa Ifakara au upo Dar?
Kwa mzigo huo gari uhakika. Gharama kwa gunia la kilo mia ni 12000.
Usafiri 9000
Ushuru 2500
Kupakia 500
Hapo umesahau pesa ya kushushia gunia, maana kama kupandisha tu ni Tsh500 unadhani litashishwa bure..?
 
Hii pesa ya ushuru wa gunia mbona ni kubwa hivyo..?

Mkuu hiyo ndo serikali yetu ya saivi ni maumivu matupu niliacha 4500 nimerudi dsm kuusafirisha zanzibar nimepata soko soon narudi tena shamba
 
Mchele wa huku mbingu hauna rangi sana ila ni mtamu hauna mfano kiufupi ardhi ya kule ni nzuri
 
Ambaye yuko tayari kwenda kufanya survey aje pm tuarange twende lini maana soon naenda kufata mzigo kwa awamu ya mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…