Aisee...kuna siku niko nyumbani kama saa tano asubui mara msg inaingia ktk simu yangu akinipa salamu nikaamua kuipiga koz ilikuwa ngeni. Aliyepokea ni mtu ninaemfahamu kabisaa koz nilisoma nae chuo na tulikaa next door hostel pia nilifanya nae assignment inshort ni mtu tunaefahamiana vuzuri.
Akaniambia fanya uje Victoria hapa mbele ya makumbusho, nikamwambia kuna nini akaniambia kuna fursa ya kujiajiri anataka tujiajiri Mimi na yeye.
Nikakubali nikijua kuwa kweli ni fursa tena tutafanya mm na yeye wazo lililo nijia kichwani ni frame tuweke Tigo pesa na vinywaji and the like.
Kufika akanielekeza jengo la ACACIA nikafika pale nikasema hili jengo ni jipya au kuna kazi humu
Alipo fika baada ya salam tukaingia ndani ya jengo kisha akaniuliza
"ulisha panda jengo zuri kama hili"
(sasa nikajiuliza inamaana huyu jamaa anamaanisha nini )
Taa ikawaka kichwani
Nikamuuliza
"Fursa inahusu nini" akasema
" subiri utaelewa tuu"
Nikakumbuka kuna upumbavu wa GNLD, F,LIVING nk.
Tukaingia ndani kila mtu yupo kimya, wanasubiri semina ianze, koz nilikuta projector , laptop mezani, na viti vipo kipresentation style.
Hapo nikasema
"I'M DONE"
Nikawanataka kutoka lakini jamaa ananisihi kuwa just nisikie then kufanyia kazi ni option yangu . Tulibishana sana, mara simu yangu ikaita, hapo nikasema moyoni hii ndo kwaheri .
Ghafla jamaa akaniambia ongelea hapahapa ndani.
Heeee...nikasema these people are trained well duuu..
Nikafosi kutoka jamaa huyo nyuma, basi akanisihi sana . Mara semina imeanza story ni hizo hizo, sijui mil 4 kwa mwezi, Mara ulaya anayepresent hajui kitu chochote kuhusu presentation yaan tunalishwa upepo wa mafanikio tuu.
Tulipotoka nikamuuliza semina gani bila malipo akasema eti Mimi ndo nna shida, nikachoka sana.
Tukatembea mpka moroko kupanda mwendokasi eti ananitanguliza nimkatie teketi nikasema huyu anijui kumbe , kama biashara inalipa Mbona hela hana.
Tukaingia kusubiri gari yaani. Kila anayemuona anataka kumuuzia bidhaa sijui kutengeneza netweki yaani tabu tupu.
NILICHOJIFUNZA
Tatizo la ajira ni shida sana, pia watu wamechanganyikiwa na mafanikio thus fall for everything yaani kuamini kile wanachoaminishwa wale jamaa ni upumbavu mtupu
Nilpoteza buku tatu ya nauli for nothing