Wauzaji wa bidhaa za forever living mnaboa sana!

[emoji113] [emoji113]
 
Ha ha ha nlienda sio kwa uzumbukuku nop niliheshimu tu alienialika, plus simu za kila dakika nilivofika kabla sijaingia nikauliza sio mambo ya forever, hata yeye hajui anasema sidhani..... Kuja kuoneshwa bidhaa anatoa macho tu
chakula kilikwepo lakini?
 
Kuna demu mmoja sijui alipata wapi number zangu, akanitumia video yenye mb 150! sikuwa nafahamu lolote kuhusiana na hii ishu ya forever kaniambia maneno kibao ya michongo ya hela nikakubaliana nae kesho asubuhi tuonane tupige hela kumbe ningepigwa za uso!

Kesho yake asubuhi nikampigia mshkaji wangu simu anisindikize nikaonane na huyo demu nipige hela jamaa kaniambia hao ni matapeli!

Hapo ndiyo nikaanza kuwa wafuatilia nikatafuta thread zao hapa jf kuhusu hawa forever hawa jamaa ni wasumbufu balaa!
 
Yaani watanzania ndo wamewakata kwelikweli mbinu ya kwanza kutumia wasichana wakali pili kuonyesha mafanikio ya uongo si mnajua tena maskini kwa tamaa
Hahahahaaaa.....hiyo mbinu ya kwanza!!!. Kwahiyo mkuu unashaurije hapo? Waendelee na mbinu ya kwanza na kuitupa mbinu ya pili ..!
 
Aisee...kuna siku niko nyumbani kama saa tano asubui mara msg inaingia ktk simu yangu akinipa salamu nikaamua kuipiga koz ilikuwa ngeni. Aliyepokea ni mtu ninaemfahamu kabisaa koz nilisoma nae chuo na tulikaa next door hostel pia nilifanya nae assignment inshort ni mtu tunaefahamiana vuzuri.
Akaniambia fanya uje Victoria hapa mbele ya makumbusho, nikamwambia kuna nini akaniambia kuna fursa ya kujiajiri anataka tujiajiri Mimi na yeye.
Nikakubali nikijua kuwa kweli ni fursa tena tutafanya mm na yeye wazo lililo nijia kichwani ni frame tuweke Tigo pesa na vinywaji and the like.
Kufika akanielekeza jengo la ACACIA nikafika pale nikasema hili jengo ni jipya au kuna kazi humu

Alipo fika baada ya salam tukaingia ndani ya jengo kisha akaniuliza

"ulisha panda jengo zuri kama hili"

(sasa nikajiuliza inamaana huyu jamaa anamaanisha nini )

Taa ikawaka kichwani
Nikamuuliza

"Fursa inahusu nini" akasema
" subiri utaelewa tuu"
Nikakumbuka kuna upumbavu wa GNLD, F,LIVING nk.
Tukaingia ndani kila mtu yupo kimya, wanasubiri semina ianze, koz nilikuta projector , laptop mezani, na viti vipo kipresentation style.
Hapo nikasema
"I'M DONE"
Nikawanataka kutoka lakini jamaa ananisihi kuwa just nisikie then kufanyia kazi ni option yangu . Tulibishana sana, mara simu yangu ikaita, hapo nikasema moyoni hii ndo kwaheri .
Ghafla jamaa akaniambia ongelea hapahapa ndani.
Heeee...nikasema these people are trained well duuu..

Nikafosi kutoka jamaa huyo nyuma, basi akanisihi sana . Mara semina imeanza story ni hizo hizo, sijui mil 4 kwa mwezi, Mara ulaya anayepresent hajui kitu chochote kuhusu presentation yaan tunalishwa upepo wa mafanikio tuu.
Tulipotoka nikamuuliza semina gani bila malipo akasema eti Mimi ndo nna shida, nikachoka sana.
Tukatembea mpka moroko kupanda mwendokasi eti ananitanguliza nimkatie teketi nikasema huyu anijui kumbe , kama biashara inalipa Mbona hela hana.
Tukaingia kusubiri gari yaani. Kila anayemuona anataka kumuuzia bidhaa sijui kutengeneza netweki yaani tabu tupu.

NILICHOJIFUNZA
Tatizo la ajira ni shida sana, pia watu wamechanganyikiwa na mafanikio thus fall for everything yaani kuamini kile wanachoaminishwa wale jamaa ni upumbavu mtupu
Nilpoteza buku tatu ya nauli for nothing
 

Mimi hao kitambo sana sikuhizi hata humu jf hawaji kujitetea
 
Kwamba nilitamani kuuza forever au sijakuelewa
Hizo promise alizokupa ndo zilikupinza bila kujali kama zilikuwa nda ya malengo yako mahususi au la. Sikulaumu maana wengi wetu tunakutwa na kadhia hizi. Mtu ukiambiwa kuna mtu anagawa hela mahali watu wanakimbilia huko bila kujiuliza kama ni sawa kugawiwa hela au sawa ni kutafuta za kwako ule jasho lako.
 

mimi waliniita mahali fulani kwa ajili ya semina nauliza semina ya nini naambiwa ni semina ya motivation & inspiration kufika bhana nikaona kuna tickets zimeandaliwa ambazo hazikutaja chochote kuhusu forever living zaidi ya picha za watu wamevaa suti nikajua yeeeess ndo penyewe hapa

akatokea jamaa mmoja akaongea takriban dakika 90 na wala hakuongea kitu chochote kuhusu forever living na kwa kweli aliongea vizuri sana kitu kimoja kilichonifanya nihisi kuna ulaghai ni kabla ya yeye kuanza kuongea aliweka speech ya nani sijui ambayo ilisaidia ku-brainwash watu na kuwaandaa kwa ajili ya kuikubali hiyo forever living

baada ya hizo dk 90 ndo akaanza kuleta masuala ya unene sijui na kuonyesha picha za sehemu za mwili wa binadamu zilizoathiriwa na magonjwa kama tezi dume nk halafu huyooo akafunua koba lake akatoa dawa za forever living aisee nilishikwa na hasira kali nikanyanyuka na kusepa muda huo huo
 
Mimi hao kitambo sana sikuhizi hata humu jf hawaji kujitetea
hawawezi kuja huku kujitetea mkuu lakini wanapita humu na wanasoma kila kitu kilichoandikwa maana ni wazuri sana wa kutumia social networks
 
ndo za mkuu! kuna jamaa mmoja eti alisema alikuwa mkuu wa customs bandari ila akaacha akajiunga na forever living
hahahaha kuna baba mtu mzima akaniita mahali nikajua jambo la mana mana enzi hizo nilikuwa natafuta ajira ama... kufika akaanza unishawishi nitafute laki 7 za kujiunga hahahah nilimnywea nia za fasta nikamblock papo hapo tehetehe
 
Aisee umekikumbusha kitu, hao jamaa wamaboa kinoma.

siku moja jamaa mmoja nae kanipigia simu akanambia wew ndo flani nikasema ndio, akanambia nimepewa namba yako na rafiki yako flani yupo iringa amenambia upo makini tunaweza kufanya biashara, akanamabia niende ofisini kwake kinondoni.

aisee nakumbuka siku hiyo nilikua nimebaki na buku tu nikatumia nauli kwenda ofisini kwake eti nafika pale ananambia upuuzi wa forever living.

mjiga yule chia hajanipa, nauli yangu alaf ananambia huo upuuzi.

yani hao jamaa wa forever wananikera sana aisee
 
"Huyu ni John Joseph Pombe Magufuli, amechunga ng'ombe na Mbuzi, akasoma shule za serikali huko Chato kutwa akitembea na miguu peku kwenda shule, leo amekuwa Rais wa Tanzania. Hata wewe unaweza kuwa rais wa Tanzania ukiweka nia." Huo ushawishi wanaopewa watu wa Forever unafanana na huu..
 
tehe tehe tehe tehe wanaboa kweli, tena sana mi mwenyewe walisha nichosha, eti kuna kongamano la wanawake hyatt hotel sijui,wageni kutoka wapi sijui,nikamwambia huyo anayenialika embu kuwa wazi huo mkutano unahusu nini,mimi sitoi mguu hadi nijui ni mkutano wa nini,alivyonitajia tu forever,nusu nimmeze coz alinizungusha hataki kusema khaaaaaa
 
Kuna mmoja nimekaa na yeye rum moja chuon alikuwa na ndoto ya kumilik gari na kwenda mbele du,,hadi leo nahisi kama anarud nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…