Wazazi acheni uhuni na visingizio, toeni urithi kwa watoto. Elimu sio urithi!

Nimecheka sana, mtu anauza gari ili anunue matairi ya gari😂
 
Tatizo wengi wenu hamna mawazo ya Kifalme mna mawazo ya kitumwa.
Unapoamua kuzaa ni wazi utazingatia suala la urithi, tatizo linakuja pale ambapo uliyemzaa haelekei wala hataki kuhangaika, mtoto anayedai urithi kwa nguvu kisa hakuomba kuzaliwa anapataje huo urithi?.
 
Wanasiasa ndio zao hizo, unafikiri zile tilion kadhaa ambazo hazionekaniki zimeibiwa kwa ajili gani?

Leo hii vijana wote wenye jina la JPM hawawezi kufa maskini sababu mzigo uliopigwa pasu umewaacha kila mmoja akiwa vizuri sana!
 
Hahahhaha mtoto huyo kiazi haswa sema una wajibu wa kummegea kipande chake akafie mbele.
 
Unakuta mzazi alifikia Ukurugenzi ila watoto hawana ajira
 
Wanasiasa ndio zao hizo, unafikiri zile tilion kadhaa ambazo hazionekaniki zimeibiwa kwa ajili gani?

Leo hii vijana wote wenye jina la JPM hawawezi kufa maskini sababu mzigo uliopigwa pasu umewaacha kila mmoja akiwa vizuri sana!

🤣🤣🤣🤣

Mwanasiasa anakuambia jiajiri alafu yeye na watoto wake wameajiriwa.

Mwanasiasa anakuambia elimu ndio Urithi hivyo uza hata Mali zao mtoto apate Elimu.

Wakati yeye anafanya kila mbinu apate Mali za kurithisha Watoto.
 
Muelekeo anautoa mzazi sio mtoto.
Swadakta!... Mzazi siku zote ana lengo la kumrithisha mtoto, hapa nina maana ya mtoto aliyezaliwa kufuatia mipango rasmi ya ndoa.

Katika makuzi mzazi atatekeleza vipengele viwili vya Mwanza ulivyoviainisha.

Changamoto itakuja kwenye hicho cha tatu, kijana akianza kusigana na wazazi wake na mbaya zaidi kudai apewe urithi.... Hakuna mahali popote mzazi atalazimika kutoa urithi.
 
Nimecheka sana, mtu anauza gari ili anunue matairi ya gari😂

Si ndio hapo sasa.

Elimu sio kitu cha kushikika, kipo akilini.

Ndio maana watu walipigania nchi zipate Uhuru wapate ardhi ya kuishi wao na kizazi Chao.

Nchi hii tumeirithi Kwa Wazee wetu.
Sasa katika level ya kifamilia lazima mzazi apiganie Uhuru wa familia na kizazi chake kipate ardhi na Maeneo ya kuendesha maisha yao
 
Kidini na kiroho analazimika.

Mtoto lazima apewe Urithi hata Kama ni mwehu kiasi gani.

Ni moja ya majukumu makuu ya Mzazi.

Wazazi wa kileo hasa waliozaliwa miaka ya 1950 ndio wameanza kucheza Rafu zao ndio maana hata heshima imeshuka.

Mungu kama Mzazi Mkuu ametuachia dunia Kama Urithi wetu Sisi Wanadamu.

Bila kujali tunaitumia vipi, bila kujali tunamkosea au hatumkosei.
Angekuwa Mungu mhuni tuu Kama angekuwa na mawazo ya kipumbavu ati asitoe Urithi kisa hatumtii au kufuata anachotaka.

Nafahamu wazazi wengi WA sikuhizi hawajafundwa tangu wakiwa wadogo, hivyo hawawezi elewa nazungumzia nini hapa
 
Unapoamua kuzaa ni wazi utazingatia suala la urithi, tatizo linakuja pale ambapo uliyemzaa haelekei wala hataki kuhangaika, mtoto anayedai urithi kwa nguvu kisa hakuomba kuzaliwa anapataje huo urithi?.
Tatizo hatulei watoto kama warithi.Mrithi anaandaliwa,mrithi sio tu mmiliki,mrithi anajukumu kubwa la kutunza na kuendeleza mali aliyorithi mpaka pale atakapo ikabidhi iyo mali kwa kizazi kinachofuata.
 
Hahahahah watoto wanabaguliwa sikuhizi!
 
Watoto wa kihindi na kiarabu kama Mutaleeb “sema tena” ni ma Don toka zama zile wanamiliki basi za SadiQ Line ila utajiri ulianzia kwa familia. Wamesoma shule tulizosoma sema tu exposure ya biashara walianzishiwa toka primary!

Wakaurithishwa mbinu sahizi wana pesa na kizazi kifuatacho pia kitakuwa na pesa zaidi! Siku wabongo wakijifunza kuwa pesa ndio huleta pesa ingine watajikomboa katika umaskini! Tuna la kujifunza toka uchagani 😅!

Maswala yale ya kujitutumua uonekane una hela ukoo mzima na kuvimba huku wanao unashindwa kuwapa njia nao watoboe ndio yale unakufa watu wanabaki dah baba yao alikuwa na pesa sana!
 
Sawa kinadharia ni hivyo! Lakini unadhani utekelezaji wake unawezekana?... Hata mahakama zinategemea kuwe na "testament" ...kama mzazi hakuacha urithi kwa makusudi unafanyaje?.

Hii changamoto ya urithi nimeiona Ulaya. Pamoja na kupanga uzazi mtoto anageuka kuwa tegemezi jumla, kisa? Hakuomba kuzaliwa na hivyo wewe mzazi jukumu lako ni kumtunza hâta kama ni mtu mzima. Wengine wanafikia hata kupanga mauaji ili wapate urithi.
 
Nimesomesha na ninasomesha wanangu kwa shida halafu niwaachie mashamba wao pesa zao kwanini wasinunulie mashamba kama wanataka? Au unataka wanangu pesa zao ziishie kwenye ulevi,ngono nk?
Mm sasa nakula bia tamu kwa kwenda mbele.
Akili za kijima hizi! Kwahio Mo Dewji hela na makampuni alioachiwa aendeshe na baba yake zile mali anatombea na kulewea bia?
 
Tatizo hatulei watoto kama warithi.Mrithi anaandaliwa,mrithi sio tu mmiliki,mrithi anajukumu kubwa la kutunza na kuendeleza mali aliyorithi mpaka pale atakapo ikabidhi iyo mali kwa kizazi kinachofuata.
Sasa unamuaandaaje mrithi wako kama sio kupitia malezi? Mpaka kufikia kuandika na kutoa urithi, kuna mchakato ambao maamuzi yake yako kwa mzazi kwa asilimia mia..
 
fanya kazi na wewe watoto wako uwape urithi acheni kupenda vya bure
 
Anafikiri williamson alikuja africa kwa miguu 😂😂😂 au kina Vasco Da Gama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…