Wazazi acheni uhuni na visingizio, toeni urithi kwa watoto. Elimu sio urithi!

Sio lazima kama mtaingia nazo kaburini ila kama mtaziacha ni lazima ziwe na address!
 
Hahahahahah hapa ndipo tofauti yetu na wale wazee walionunuaga viwanja kariakoo ilipo😅!

Sahizi kuna baadhi ya wasanii ambao baba zao walikuwa na mijengo kariakoo imagine pameshaota maghorofa! Watu walikamua million 600 mpaka Billion 1! Kuuziwa yale maeneo tu! Unakuta kiwanja babu alinunua shilling 20 tu zama hizo😅

Akili ya ku acquire mali kwa ajili ya future ya kizazi chako ni muhimu sana.
 
Kwa maisha ya sasa urithi wa mtoto ni kumpa kitu kinachoweza kumsaidia maishani...Elimi yetu bado ni changamoto kubwa sana...bado haijawekwa kwenye kiwango cha urithi
 
Mungu wa Isaka na Yakobo na akujaalie uyatimize maono yako. Urithi kwa vizazi vyetu ndo jambo muhimu. Na hongera kwa kuwa mmojawapo wa wachache tuliolielewa somo hili.
 
Jamii zingine zimetuzidi hili hasa waarabu, mtoto anapewa elimu kwanza ambayo itamuwezesha kurithi mali zilizopo mfano maduka na viwanda
waafrica ubinafsi umetuzidi.Ila kwa vitu ambavyo sijawahi kuwaza ni urithi aisee...hilo nilifuta siku nyingi sanaaa nilipogundua mwamba simuelewi.Vijana msiwaze urithi waza wewe utawapa nini wanao tena wakiwa na umri mdogo wa kuanzia 25-30 yrs wasiteseke kama wewe ulivyoteseka,finishi.Kwa hili mzee wa fasihi sikuungi mkono kaka
 
Sasa tumefikia patamu. Basi kinachotakiwa mzazi somesha watoto kimachalemachale kama haeleweki darasani mpe mtaji mapema ajiongeze usijekuishia kumaliza pesa kwenye ada alafu ukakosa kumpa mtaji
 
Wachaga wangekuwa na akili muflisi kama hizi wasingepiga hatua wanazopiga.Acha kudanganya watoto wa wenzio unawadekeza mno wewe.Yuko mmoja hapa ameshangaa eti utauzaje shamba kisa unasomesha mtoto akili muflisi kabisa hizi.Kuna mzee mmoja nilisoma na mtoto wake chuo kikuu dar aliuza gari ili mtoto wake akasome Marekani baada ya kufukuzwa mwaka ule wa 1990 mtoto kaenda Marekani akawa na akili za kupindukia wamarekani wakambakisha kule kwa sasa anafanya kazi shirika la NASA kamtumia baba yake magari kama siafu.Watu wanaofuga mang'ombe ndio wanakuwa na akili muflisi za kufikiria mambo ya kurithi mang'ombe makabila haya tunayajua wako nyuma sana kifikra japo wana utajiri wa asili.
Najua mtasema mbona MO na watoto wa Bakheresa wamerithi mali za baba zao ukweli hawakurithi ila baba zao wanawasomesha kwanza wasiwe mambulula kama huyu anayesema elimu sio urithi kisha wanarudi baba zao wanawaomba watumie elimu zao wawasaidie kwenye biashara zao kumbuka Dewji ana shahada ya uzamili au masters ya uchumi amesomea Marekani alivorudi mali za baba yake zikaendelea maradufu hakukaa kusubiri eti agawiwe chake ni umuflisi kiakili acheni kudanganya watu elimu ni kila kitu.
Ukitegemea eti upewe urithi akili inalala tafuta chako baba yako akigundua una akili sana atakupa vinavyofaa
Hawa wachunga ng'ombe wa hovyo sana
 


Kuna watu nchi hii wanaouana kisa Urithi Kama Wachaga??

Bahati nzuri nimeishi nao hivyo nawajua fika
 
Kuna watu nchi hii wanaouana kisa Urithi Kama Wachaga??

Bahati nzuri nimeishi nao hivyo nawajua fika
Hao watakuwa ni wachaga warombo maana katika wachaga ambao wana imani za kijinga sana ni kabila hilo ule mpaka wa Kenya umewapumbaza sana kila mtoto anafikiria kufungua duka na mambo ya ushirikina wachaga wengine wako poa sana
 
brother Heriel ngoja nikuchekeshe kidogo
Usikute ndio nyie mliomaliza chuo ajira hakuna sasa mnaanza kutuwazia sisi wazee tufe
mrithi hakika tatizo la ajira ni msumari wa mto inatia huruma
 
Na huyu yatima aliekulia kwa baba paroko urithi anapata wapi? au baba paroko anahusika.
 
Inaijua vizuri dhana ya urithi?,unayajua majukumu ya mrithi?,unajua kuwa mrithi anaandaliwa?,unajua kuwa Mali/utajiri wa kurithi ndio unaoweza kudumu kizazi hadi kizazi?,unajua utajiri wa kurithi ndio unaoweza kufuta umasikini wa familia/ukoo?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…