Wazazi acheni uhuni na visingizio, toeni urithi kwa watoto. Elimu sio urithi!

Kwahiyo tukikosa ada watoto wabaki
 
Asia iliyoendelea Kama UEA, Qatar, Baadhi ya Maeneo ya India, Iran n.k
Mfumo wa serkali zao hauna ubabaishaji, na kukosa mielekeo kama nchi haina dira maalum nchi matamko kwa kila anayeshikilia dola usitegemee kuendelea
 
Mfumo wa serkali zao hauna ubabaishaji, na kukosa mielekeo kama nchi haina dira maalum nchi matamko kwa kila anayeshikilia dola usitegemee kuendelea


😀😀😀

Nchi inajengwa na Nani Sheikhe!

Sasa Kama Viongozi wa nchi wengi wao ni wazazi wahuni unategemea nini Boss.

Nashukuru unaanza kunielewa
 
Mzazi jukumu lake ni kukutengenezea mazingira ww utoboe tobo la mafanikio iwe kupitia elimu au namna yoyote ile. Jukumu la wewe kurithi mali lipo tu kama wataziacha basi utarithi, lakini wakikuacha bila mbinu za kumaintain utarudi mavumbini tu. Na hapa ndiyo wahenga walitengeneza msemo wa elimu ni urithi tosha lakini hawakumaanisha huna haki ya kurithi.
 
Mzazi halazimiki kwa namna yoyote ile kugawanya mali zake kama urithi. Hakuna sheria inayomlazimisha kugawa mali kwa watoto wake kama haridhishwi na mwenendo wa zao lao. Mali zilizochumwa na wanandoa ni mali ya wanandoa hadi hapo watakapoamua kuwagawia mali watoto kwa hiali, lakini sio lazima!.
 
Nimesoma hii hoja ya mtoa mada, nikatumia dakika kadhaa kufikiria matajiri na marafiki wenye ukwasi nachelea kusema Yupo sahihi. mtachukia tu ni hali ya kibinadamu ila hoja yake ina mashiko.
Baada ya kumaliza masomo ni rahisi mno kufanikiwa kimaisha kwa mtoto aliekabidhiwa mali ukilinganisha na yule ambaye ndio inabidi aanze kutafuta.. Endapo huyu wa pili hatogundua hilo na kuacha urithi wa mali kwa mwanae.. basi mwanae atapita njia ile ile ya mahangaiko baada ya kumaliza kusoma, kwa namna hii umasikini ni ngumu kutoweka kwenye huo uzao.
 
Tatizo wengi wenu hamna mawazo ya Kifalme mna mawazo ya kitumwa.
 
Wengine hatukusumbuka kungoja urithi. Kumbuka urithi unaweza usiwepo. Wengine wamezaliwa masikini, badala ya kuhangaika apate chake, akae kugombania kihamba na nduguze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…