Mambo mawili hapo nayaona juu ya fikra za wazazi kuhusu mtoto wa kike:
1. Kwamba, wazazi wengine huamini mtoto wa kike ni wa kuolewa tu, haijalishi kasoma saana au kiasi chake. Hii hupelekea kila hatua ya masomo anayohitimu kuonekana hatua inayofuata ni kuolewa.
2. Kwamba, baadhi ya wazazi huona mtoto wa kike kama kitega uchumi; kwamba kuolewa kwake kutachangia pato katika familia.
3. Kwamba, pengine ni aibu mtoto wa kike akizalia nyumbani.
Nashukuru Mungu, nina mabinti wawili, wamehitimu chuo, bado nawahudumia kimaisha na ninawatafutia kazi. Kamwe sijawahi na sitawauliza ni lini wataolewa. Nyumba nawalipia na 'pocket money' nawapa kila mwezi. Faraja yangu ni kuwaona wakifanikiwa kuanza maisha kivyao na kujitegemea.