Wazazi mmekuwaje?

Wazazi mmekuwaje?

Nadhani ndiyo maana kashusha andiko hili.

Kwa wenye D mbili+... hii ni siredi ya kimkakati.

She is bright. She trying to keep her essence and value. Sio kila mtu akajianike kule 'love connect' na bango kuuubwa, nah!

Ephen, soon utaolewa na utapata mume. 😎

-Kaveli-


Ndo maana comment ya kwanza nimemwambia Una akili Sana

Anafanya mawindo kimya kimya
 
Habari!

Nilipomaliza chuo nilipatwa na mkasa. Ile nimemaliza tu mitihani nikamtaarifu mama, tukaongea tu vizuri kwa muda mfupi chumbani kwake, sasa wakati natoka nje akaniuliza swali 'kwahiyo ushapata mtu wa kukuoa?' moyo ulishtuka halafu chap nikaendelea na safari hapo nikajifanya sijamsikia.

Ikawa wimbo anaoupenda 'ushapata wa kukuoa? Nikawa namwambia sipo tayari kwa sasa nikimjibu hivyo anaanza kutoa risala 'unajua inabidi uolewe mimi najisikia vibaya kukuona tu hapa nyumbani'

Siku moja nikamwambia mimi sijapata hata wa kunioa, akasema 'uzuri wote huo hakuna aliyesema anataka kukuoa' ilibidi tu nicheke mimi nilikuwa nishasoma akili yake kwamba uoga wa maisha unamsumbua.

Ishapita miaka 3 tokea kisa hiki kitokea, juzi nikasema acha niwaulize wenzangu kama wanakutana na maswahibu kama yangu sababu huu wimbo mama yangu bado anauimba.

Rafiki yangu FLORA
Yeye aliniambia alivyomaliza Mitihani alichelewa kurudi nyumbani kwa miezi kadhaa, sasa kuna siku akaumwa akalazwa mama yake alivyoenda hospital akamkuta Flora yupo na boyfriend wake ila huyo bf akawapisha waongee.

Mama yake akamuuliza 'huyo kijana ni nani' Flora akamjibu ni rafiki yake.
Mama yake akamwambia bills ni kiasi gani ili alipie! Flora akamwambia 'rafiki yangu ameshalipia' mama yake akaguna.

Sasa Flora alivyorudi kwao, mama yake akaanza kuimba nyimbo kila mara 'Yule rafiki yako yuko wapi akuoe kuliko kushinda ndani kila siku' Flora akaishia tu kucheka.

Rafiki yangu REBECCA
Yeye alikuwa anabanwa sana, ni wale watoto geti kali. Alivyomaliza chuo kuna siku akamuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumsalimia rafiki yake. Mama yake hakumuuliza maswali mengi kama alivyokua anafanya hapo awali.

Jioni mapema Rebecca aliporudi mama yake akamwambia 'Mbona umerudi mapema' akamjibu nilienda kumuona tu mara moja. Mama yake akamwambia 'Ebu tembeatembea wachumba wakuone sio kujifungia tu ndani'

Ila ameniambia huo wimbo mama yake aliuacha baada ya yeye kupata kazi.

Rafiki yangu ASHA
Huyu ndiye amenichekesha sana, anasema tulivyomaliza chuo baba yake akawa anamwambia 'fanya uolewe sitaki kukuona nyumbani kwangu'

Kuna siku akaenda kazini kwa baba yake akamkuta yupo na wanaume wengine akawasalimia.
Kijana mmoja akamwambia mzee wake kwamba hakujua kama ana binti mkubwa vile! Mzee wake akajibu 'Huyu ni binti yangu kamaliza chuo mwaka huu na bado hajaolewa' wote wakaishia kucheka.

Haikupita miezi mingi baba yake akamletea mchumba, ubani ukachomwa sasa hivi yupo kwenye ndoa.

Nilichokiona wazazi wengi ambao hawajajipata kazi wanayotupa watoto wa kike ni kuolewa tena kama mtoto hajapata kazi ya kufanya.

Ila ukiwa na kazi nzuri unapata pesa, hii risala ya kuolewa hawatoi hata ukifikisha miaka 40.

Sasa sijui wa kulaumiwa ni CCM, wazazi wetu au sisi watoto.
Ngoja namba ziendelee kusoma. Utakuja kufungua uzi tu wa kusema siku zinayoyoma.

Unafikiri wazazi wako hawakutakii mema? Kwanza inakuaje una marafiki wote hawaolewi?
 
Mzee wa kububujikwa machozi n wengine ambao mmeonesha interest kwa mwandishi wa hili bandiko.

Niwaambie tu huyu mtoto yupo booked 🙏🏽
 
Singo maza hawana shida Sana mkuu ukimpenda mtoto wake tayari ushampata
Haya ndio mambo mimi nayaweza sasa , mambo ya baby leo nina hamu na pizza 🍕 mimi siyawezi mkuu.
1720095510387.jpg
 
Mabinti wote niliograduate nao chuo na kuolewa haraka wanaishi maisha duni. Cha ajabu wote walikuwa watumishi na watu wa imani, kasoro gumegume mmoja aliolewa na mzungu kibabu ana miaka kama 65 wako Marekani kwa sasa.

Hao walioolewa hawajapata kazi hadi sasa, na maisha sio mazuri kivile ukizingatia elimu yao hawajaitumia ama kuajiriwa ama kujiajiri. Kuna ambao nina ushahidi wanajutia na mwingine nimemchangia gharama za hospitali.

Mtu kamaliza chuo hajaenda intervie yoyote, hajaajiriwa au kujiajiri. Huyo mbio kafunga ndoa. Hapo ana honeymoon, akitoka analea mume, akitoka anapewa mimba, analea mimba, anajifungua, analea kichanga. Baada ya hapo tiyari hatakiwi kukaa mbali na mtoto, hawezi tena kuwa free kwenda interview siku ya interview mtoto anaamka anaharisha.

Unakuta hamna hamna miaka miwili imekatika wapo tu hamna hatua wamefanya. Familia changa inakula hela balaa, gharama za maisha zimepanda. Mke elimu anayo ila kazi hana.

Nashauri binti ukimaliza chuo focus kwanza kuwa na chochote cha kuingiza kitu. Ajiriwa kwanza, hivi nani atakuajiri private sector ukiwa na mtoto wa miezi 6 kila siku una dharura? Alafu entry level opportunities zina mizunguko mingi huiwezi ukiwa na ndoa changa na watoto wadogo.
Kazi za serikali chache. Unless uhakikishe unayeolewa naye anaweza cover kila kitu, mna nyumba na bima na cashflow ya kueleweka.
Wanaingia ndoani ili kurahisisha maisha mkuu..

Mzigo wote anampa mume.
 
Back
Top Bottom