Wazazi tusiache kusomesha watoto wa kike

Wazazi tusiache kusomesha watoto wa kike

Kila mtu kwenye ndoa atakuwa busy kutafuta Mali yake alinde heshima yake
Hii mambo imeshaanza kukomaa kwenye societies zetu. Yani kila mtu anamwangalia mwenzake kimachale machale tu. Mungu atusaidie sana.
 
Screenshot_20230416-000300.png
 
Habari ndio hiyo, sasa hivi wanawake wasome wafuate ndoto zao wafanye kazi au biashara wanazozitaka, hakuna tena kufuata ndoto za mume

Kila mtu awe busy kutafuta pesa zake, mwanamke hata akiondoka asubuhi na kurudi usiku hatakiwi kuulizwa wala kulalamikiwa sababu naye anatafuta pesa zake, ili mwisho wa siku wakiachana naye awe na chake asidai cha mumewe

Na wanaume waache kelele za oo mke wangu hanipikii hanifulii hanipetipeti wala hanijali kama anavyowajali watoto, maana kumbuka naye yuko busy kama wewe anatafuta pesa zake, hapo ndoa ndio zitakuwa rahisi
Hapa umemaliza,lakini Kwa ku-summarise haha mawazo Yako, ni kwamba watu tusioane Kila mtu akomae kivyake ila Kwa kuongezea tu,mimba kanunueni maabara ili watoto wenu watumie majina yenu kabisa!
Wanaume tuishi kwa kununua uchi tu, kufanya maisha yawe mepesi ila yenye kuijenga taifa la hovyo kabisa!
Ni machaguo tu!
 
Habari ndio hiyo, sasa hivi wanawake wasome wafuate ndoto zao wafanye kazi au biashara wanazozitaka, hakuna tena kufuata ndoto za mume

Kila mtu awe busy kutafuta pesa zake, mwanamke hata akiondoka asubuhi na kurudi usiku hatakiwi kuulizwa wala kulalamikiwa sababu naye anatafuta pesa zake, ili mwisho wa siku wakiachana naye awe na chake asidai cha mumewe

Na wanaume waache kelele za oo mke wangu hanipikii hanifulii hanipetipeti wala hanijali kama anavyowajali watoto, maana kumbuka naye yuko busy kama wewe anatafuta pesa zake, hapo ndoa ndio zitakuwa rahisi
Mwanamke na mwanaume hawapo sawa atatoka kutafuta hela na mimba? Vipi kuhusu watoto na hiyo habari ya kutoka kurudi usiku?
 
Sasa nao si wanatafuta pesa zao ili mwisho wa siku wakiachana mwanamke awe na mali zake asidae za mumewe
Sijakataa kwenda kutafuta .Na tumbo lako la miezi 7 utaenda kutafuta nini na wapi?
 
Nadhani mmeona wenyewe mambo aliyofanya ASHRAF HAKIMI na wanaume pia baadhi ya wanawake wanavyofurahia alichokifanya.

Mwanaume anamdharau mwanamke anamthamini mama yake. Yaani anamthamini aliyemzaa anamdharau aliyemzalia, namaanisha anamdharau mama anamweshimu mama, nadhani mmenielewa.

Kiufupi si wanawake tu hawajui wanataka Nini bali hata baadhi ya wanaume hawajui wanataka Nini.

Tusomeshe wanetu wa kike wawe na Kazi zao Ili wawe na Kazi wakiolewa mabwana zao wakiwachoka na kuwapa talaka wasiangaike na kumdhalilishwa kama hivi anabaki na Kazi yake na watoto wake.

Wanaume mnachukulia poa hili lakini ndo linaenda kuharibu mfumo mzima wa maisha ya ndoa. Kila mtu kwenye ndoa atakuwa busy kutafuta Mali yake alinde heshima yake.

Wanawake watazaa watasomesha huku wao wakijua mwanangu hata akioa mke Mali hazimuhusu.😭😭😭😭😭 Ee Mwenyezi Mungu kitetee kizazi chako.

Dunia ndo inaharibika, yaliyotabiriwa yanatimia yote. Aisee upendo hakuna tena.
Mnaendekeza tamaa,kwani mke wa hakimi hana kazi,mali alikua nazo ila tamaa za kutaka zaidi zikamponza.

Unazaa na mtu watoto wawili mnalala mnaamka kumbe unawaza siku moja uende mahakamani udai talaka ili upate mali

Hakimi kaamsha akili za wanaume wengi zilizokua zimelala kizembe.mtanyooka tu

Wanawake matapeli hii ndio dawa yao sasa
 
Wanawake bhana.

Naona wengi humu wanaangalia upande wa yule mke, ila hawavai viatu vya Yule mama. ( Hapa inazua maswali mengi )

Sasa najiuliza je yule mama wa Hakim Ashraf yeye sio mwanamke?
 
Mleta mada usilolijua ni kama usiku wa giza...

Samir Nasri ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye alipoteza mali zake baada ya kutalikiana na mke wake wa zamani, Anara Atanes....

Emmanuel Eboue ni mchezaji wa soka wa zamani wa Ivory Coast ambaye alipoteza mali zake baada ya talaka yake na mkewe mwaka 2017.

Ray Parlour - Mchezaji wa zamani wa Arsenal ya Uingereza, ambaye alipoteza pauni milioni 2.5 za mali yake baada ya kutalikiana na mkewe.

David James - Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England, ambaye alilazimika kuuza nyumba yake baada ya kutalikiana na mkewe.

Ryan Giggs - Mchezaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Wales, ambaye alipoteza takribani pauni milioni 40 za mali yake baada ya kutalikiana na mkewe.
 
Sawa nimeelewa mkuu, tusomeshe tu watoto wawe na Kaz zao ambzo hata wasipopewa huduma na mwanaume ztawasitiri kidogo
 
Back
Top Bottom