Nilipokuwa mdogo niliamini Jeshi la Polisi ni taasisi inayo mulika kila mahali!
Niliamini Polisi ni Dubwana kuuubwaa lenye kuona yaliyopita, yaliyopo na yajayo!
Hii Imani ilinifanya nivimbe kichwa na kutembea kifua mbele!
Sikuogopa ujambazi kwasababu niliamini jeshi lipo!
Nilikatiza popote bila tahadhari nikiamini nyuma kuna jeshi!
Ilifika hatua nilikula vyakula hovyo kutoka kwa watu nisiowajua bila kuogopa kulishwa Sumu! Kwasababu niliamini JESHI LIPO! Niliamini kama chakula kina sumu basi jeshi lipo Litakagua sampuli! ...
BAADAE NILIKUJA KUGUNDUA NILIKUWA NAOTA NDOTO ZA MCHANA!
Niliwaza vile kwasababu ya utoto lakini baadae ndo nilikuja kuelewa kwamba!
1. Ulinzi uko mikononi mwako na Mungu wako, Polisi ni kivuli cha tatu ambacho hutegemea sana na hali ya hewa.
2. Nimekuja KUGUNDUA kwamba pamoja na sheria za zebra, Ninapovuka barabara lazima nijiridhishe pako salama kuvuka kwasababu ajali ikitokea upelelezi huja baadae
3. Kiufupi nimekuja KUGUNDUA kabla ya kulipa mzigo jeshi la Polisi lazima NIWAJIBIKE kwanza Mimi!
HOJA YANGU NI IPI HAPA
Kumekuwepo na matukio ya kikatili sana mtaani! Ambayo yanachangiwa kwa asilimia 70% na watu kutowajibika!
Mfano!
Wale wazazi wenye watoto!
Unapeleka watoto chuo hufuatilii mtoto analala wapi, anakula nini, anaishi na nani huko chuoni hujui!
Wakati mwingine hata ada hulipi lakini mtoto anaendelea kusoma huulizi nani kalipa ada!
Mtoto anarudi likizo nyumbani na vitu vya bei ie iPhone, laptop n.k nguo za gharama, Kama mzazi huulizi!
Mtoto anaondoka kurudi chuoni humpi nauli anaondoka kama alivyokuja!
HALAFU MWISHO WA SIKU Ukatili unaootokea kwa mwanao UNALILAUMU JESHI la Polisi! ( Ni sawa kulaumu lakini Wazazi tujiulize je tuliwajibika?)
Ulinzi unaanza na sisi ! Tutawalaumu bure Polisi siyo malaika!
Polisi hawana uwezo wa kupita kila nyumba kuwakumbusha mfunge milango!
Wajibu wa ulinzi ni sisi wenyewe, Haki ni kwa Mungu, Polisi ni sheria na sheria ni vielelezo!
Polisi wakikosa vielelezo ndo imekwisha hiyo!
Kuna watu huwa nawatania kwamba "Siyo kila aliyeajiri mlinzi anamaanisha ana ulinzi, Hapana! Walinzi waliowengi huko mtaani ni Vielelezo"
Kila mtu awajibike,
Mzazi wajibika, mwenyekiti wajibika, mchungaji wajibika, polisi ukipokea taarifa wajibika!
HAPO NDIPO ITALETA MAANA YA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAKE!