Wazazi wa Azory Gwanda watuma barua kwa Rais Samia Suluhu Hassani

Wazazi wa Azory Gwanda watuma barua kwa Rais Samia Suluhu Hassani

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
04 June 2021

Baada ya kauli za kupingana kati ya ile ya waziri Prof. Palamagamba Kabudi wa serikali ya Tanzania alipohojiwa na BBC Swahili na ya msemaji wa Mkuu serikali ya Tanzania Dr. Hassan Abbas kuhusu kutoweka kwa mwandishi wa habari Azory Gwanda hapo mwezi November 2017.

Msemaji wa serikali Dr. Hassan Abbas alisema serikali iliyokuwa chini ya hayati rais John Pombe Joseph Magufuli inafanya jitihada zote kujua kuhusu kutoweka kwa mwandishi Azory Gwanda.

Wazazi wa Azory Gwanda wameomba msaada wa serikali ya Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iendelee kufuatilia kujua taarifa kamili juu ya suala la kupotea mwandishi huyo wa Mwananchi Media Corporation ili ieleweke kilichompata mwandishi huyo ili wazazi na familia ya Azory Gwanda wafahamu yaliyomkuta kama bado yupo hai au amefariki .

Chanzo: CHADEMA MEDIA TV
PIA, SOMA:

- Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea siku 10 na hajulikani alipo

Kutoweka kwa huyu mwandishi kunatatanisha kwani hata haijulikani alikuwa akiandika au akitafuta taarifa juu ya kitu gani ambacho kingeweza kuwa ndiyo sababu ya kutoweka kwake.

Hivi huko Mwananchi nao hawajui alikuwa akishughulika na habari gani?

Je kwenye magazeti ni habari zipi alizokuwa anaziandika, ili tujaribu kuunganisha doti?.

Hii ni tofauti kabisa na kutoweka kwa Ben Saanane, ambaye habarizilizosababisha apotee zinajulikana wazi.
 
Wazazi wengine nao ni hovyo kabisa sasa hawa walikuwa wapi siku zote toka mwanao atoweke utafikiri huyo mtoto walimchuma mtini.

Wale wa Beny Saanane ndio kabisa hata habari hawana utafikiri walimtoa kafara mwanao. Hizo ndizo "Legacy" za huyu dikteta Magufuli, rais wa hovyo kuwahi kuonekana katika nchi hii.
 
Duh! Legacy ya mwendazake imejaa makandokando mengi sana. Damu za wapendwa wengi sana hapa nchini bado zinamlilia. Si Azory tu bali hata Ben Saanane na wengine ambao hawakuwa maarufu na kuweza kutambulika kama wale ndugu wengine wa MKIRU.
 
Wazazi wengine nao ni hovyo kabisa sasa hawa walikuwa wapi siku zote toka mwanao atoweke utafikiri huyo mtoto walimchuma mtini.

Wale wa Beny Saanane ndio kabisa hata habari hawana utafikiri walimtoa kafara mwanao. Hizo ndizo "Legacy" za huyu dikteta Magufuli, rais wa hovyo kuwahi kuonekana katika nchi hii.
Usikufuru. Wamelia sana kuomva sana, hadi balozi za nje wameenda kuomba msaada. Weka akiba maneno.
 
Wazazi wengine nao ni hovyo kabisa sasa hawa walikuwa wapi siku zote toka mwanao atoweke utafikiri huyo mtoto walimchuma mtini.

Wale wa Beny Saanane ndio kabisa hata habari hawana utafikiri walimtoa kafara mwanao. Hizo ndizo "Legacy" za huyu dikteta Magufuli, rais wa hovyo kuwahi kuonekana katika nchi hii.
Inaonekana Hufuatilii habari.
Washaongea na kumuomba JPM awasaidie kujua alipo mtoto wao,hawakukaa kimya.
Mke wa Azory naye kapiga Sana kelele kuhusu kupotea kwa mumewe.
 
Wazazi wengine nao ni hovyo kabisa sasa hawa walikuwa wapi siku zote toka mwanao atoweke utafikiri huyo mtoto walimchuma mtini.

Wale wa Beny Saanane ndio kabisa hata habari hawana utafikiri walimtoa kafara mwanao. Hizo ndizo "Legacy" za huyu dikteta Magufuli, rais wa hovyo kuwahi kuonekana katika nchi hii.
Ulitaka wamwombe muuaji msaada?
 
Back
Top Bottom