Mohammed wa 5
JF-Expert Member
- Jun 20, 2022
- 1,215
- 3,035
Maisha Yana Mambo mengi Sana. Mimi ni kijana wa kiume Nina miaka 29 nakaribia 30 soon,mtoto wa pili Kati ya watoto watano nimemaliza chuo mwaka 2019 sasa hivi nipo mtaani napiga harakati zangu Mungu anasaidia maisha yanasonga JAPO familia yetu inajiweza kipesa sitegemei hela za nyumbani... situmii kilevi chochote Wala sio mtu wa wanawake.
Shida yangu ni wazazi hasa mama yangu amekuwa mtu kunitilia mashaka kisa hajawahi kusikia Nina mwanamke Wala tokea nasoma sijawahi kuleta kesi nyumbani kuhusu wanawake. Mama yangu ni mama anayependa watoto sababu amemlea mtoto wa Kaka first born mpaka amekua na watoto wa majirani washamzoea na wanamuita Bibi.
Juzi niliitwa kwenye kikao nyumbani wanataka nilete mwanamke nimtambulishe au kama kuna sehemu nina mtoto nimpeleke nyumbani wamjue na waishi nae pale labda wana wasiwasi hapati malezi bora huko halipo. Wanasema umri huu ndo mzuri wa kupata mtoto kwa sababu damu inachemka na nitapata watoto wenye akili na afya bora, niliwajibu kwa sasa sina mwanamke wala mtoto (nilidanganya) wakati nipo chuo nilikuwa na mahusiano binti kutoka Moshi na nilimpaga ujauzito ana mtoto wa kike naishia kumuona kwenye picha tu status maana mama yake hataki niwe karibu na mtoto wala hahitaji matunzo yangu tuligombana na nilicheat akajua nimejaribu kumuomba msamaha hataki kuelewa Nika move on. Ipo siku atakuja kunitafuta mwanangu sijamtelekeza she love so much more my daughter N♥️
Juzi wakati nipo mtaani nilisikia umbea sijui tetesi kwenye vikao vya wamama mama yangu anawasimulia wamama wenzake ana wasiwasi na mimi labda nina matatizo au labda sio rijali na anataka atafute wanawake awape hela ili wanitongoze halafu wanipime kama sina tatizo vijana wezangu niliocheza nao mtaani wameoa na wengine wana watoto
Wakuu mimi ni mhanga wa MAPENZI nimepigwa matukio sana kila mwanamke nayekutana nae nahisi ni walewale JAPO wa kujipozea machungu yupo Ila sio wife material na sina mpango wa kumpeleka home. Hii hali inaniumiza sana nifanyeje au niwaeleza nyumbani nina mtoto sehemu nahisi maswali yatakuwa mengi kwanini muda wote sikusema.
Ushauri wenu na mawazo yenu muhimu wakuu nipate muongozo kidogo au nifanye nini nyumbani wanijua kumbe niko vizuri