Mimi ni kijana wa kiume miaka 19 nimemaliza form 6 na kuapply chuo nasubiri majibu sasa.
Lakini likizo hii imekuwa chungu kwangu maana wazazi kila siku wananisema tu.
Wananilazimisha nijichanganye na watu halafu binafsi sipendi. Napenda niwe peke yangu na muda mwingi nipo chumbani kwangu
Nakereka sana, wazazi wakirudi toka kazini wakifika tu nyumbani kitu cha kwanza ni kuniita na kunilazimisha kukaa sebuleni na familia. Mara nyingi hata nikikaa sebuleni wananiona nimekaa sina furaha, wanaanza kuniuluza mbona huongei? Mimi sina cha kuwajibu sijui sababu, wao wanalalamika kwa sababu wanadai zamani sikuwa hivi.
Kuna maneno yao wanaongea sometimes yananiumiza, mfano wananiongelea wanasema "Huyu mtoto sijui tumfanyeje, tumetumia kila mbinu tumeshindwa. Hivi maisha yako baadaye utaishije ikiwa hujichanganyi na watu?". Wakiniambia hivi huwa nakaa tu kimya ila moyoni huwa nawajibu "kwa nini mnawaza kuhusu maisha yangu ya mbeleni, si mniache tu nitajua mwenyewe"
Licha ya wao kujua kuwa mada yao ya kunilazimisha nijichanganye na watu siipendi lakini hawachoki kuianzisha wakikaa na mimi, kila siki wananikasirisha na hii mada. Sometimes wanazidi hadi nawajibu vibaya kwa hasira, halafu najishtukia kuwa nimekosea kuwajibu hivyo. Naonekana sina maadili ila ukweli ni kwamba wao ndio wananikasirisha
Hata sasahivi naandika hivi ila wametoka kuniita na kuniambia nikae sebuleni. Nimekaa nao dakika chache tu nikanyanyuka nimerudi zangu chumbani, sijisikii vyema kukaa na watu wengi.
Natamani muda wa chuo ufike niende chuo maana maeneo kama shuleni watu hawaniulizi sana kwa nini najitenga. Muda mwingi hawaongei na mimi na hivyo ndio nilikuwa najisikia amani
Kwani upi ni uamuzi wa busara?
Nifuate furaha yangu, niendelee kukaa peke yangu.. au
Nijichanganye na watu kufurahisha wazazi, wakati mimi moyoni sipendi?