2006 huyu!
1. Introversion (Utabia wa ndani) – Sio tatizo la kiafya.
- Watu wa aina hii hupata nguvu wakiwa peke yao.
- Hupenda utulivu, huongea kidogo na mara nyingi hupendelea mahusiano ya karibu kuliko makundi makubwa.
- Hii ni tabia ya kawaida na sio ugonjwa, isipokuwa ikizidi huathiri maisha ya kawaida na kuleta unyogofu.
2. Social Anxiety Disorder (Hofu ya kijamii)
- Anaweza kuwa na hofu kubwa ya kuhukumiwa au kuonekana vibaya mbele za watu.
- Huogopa kuanzisha mazungumzo au kuwa sehemu ya kundi.
- Hutamani kujichanganya lakini huzuia kutokana na hofu(kuto jiamini kwa nafsi eidha kwakujihisi una mapungufu au kwa kuona wengine Wana mapungufu wkt sio kweli)
3. Depression (Msongo wa mawazo)
- Kujitenga ni mojawapo ya dalili za huzuni au msongo wa muda mrefu.
- Mtu hupoteza hamu ya kushirikiana na watu, kuongea au hata kufanya shughuli za kawaida, kiasi hupelekea kujihisi huoni thamani ya maisha wala thamani ya watu kwakuhisi Hawana msaada na Hali hii ikiwa chronic wengi hukata tamaa na kujiua.
4. Avoidant Personality Disorder
- Hali ya kudumu ya kuepuka mawasiliano au mahusiano kutokana na kujiamini kidogo, hofu ya kudharauliwa au kukataliwa( hapa imejikita kwenye mapungufu ya kimwili mtu kuanza kujitoa kasoro na kutoa kasoro kwa wengine kiasi hupelekea kukaa mbali zaidi ili kutunza usiri wa ndani wake.
5. Autism Spectrum Disorder (ASD) – endapo ni hali ya kudumu tangu utoto
- Mtu anaweza kuwa na ugumu wa mawasiliano ya kijamii na mara nyingi hupendelea kuwa peke yake.( akiwa tayari amesha tambua maisha yake ni yakipekee zaidi ya upweke ambapo madhara yake ni pale ataamua kutafuta kampan nje ya watu na kuanza kutumia baadhi ya vilevi, burudani frani mbadala ya Amani yake ili adumishe dhima ya maisha yake.
NB: jitahid kujihusisha na michezo ili kuboresha afya ya akiri, unapokuwa na changamoto yoyote inayogusa akiri jaribu kumshirikisha mtu unayehisi unamuamini zaidi, pia jifanyie tathimini ikiwa wew binafsi umetambua kwamba umebadirika eidha kwa hatua za ukuaji au mabadiriko ya kimazingira, basi andika kila siku tabia mpya zinazojitokeza.