Wazazi wanataka nijichanganye, wanahisi kuna jambo linanitatiza

One man army dont trust any body labda Mungu,,watu wengi masnitch
 
Mimi ni kijana wa kiume miaka 19 nimemaliza form 6 na kuapply chuo nasubiri majibu sasa.

Lakini likizo hii imekuwa chungu kwangu maana wazazi kila siku wananisema tu.

Wananilazimisha nijichanganye na watu halafu binafsi sipendi. Napenda niwe peke yangu na muda mwingi nipo chumbani kwangu

Nakereka sana, wazazi wakirudi toka kazini wakifika tu nyumbani kitu cha kwanza ni kuniita na kunilazimisha kukaa sebuleni na familia. Mara nyingi hata nikikaa sebuleni wananiona nimekaa sina furaha, wanaanza kuniuluza mbona huongei? Mimi sina cha kuwajibu sijui sababu, wao wanalalamika kwa sababu wanadai zamani sikuwa hivi.

Kuna maneno yao wanaongea sometimes yananiumiza, mfano wananiongelea wanasema "Huyu mtoto sijui tumfanyeje, tumetumia kila mbinu tumeshindwa. Hivi maisha yako baadaye utaishije ikiwa hujichanganyi na watu?". Wakiniambia hivi huwa nakaa tu kimya ila moyoni huwa nawajibu "kwa nini mnawaza kuhusu maisha yangu ya mbeleni, si mniache tu nitajua mwenyewe"

Licha ya wao kujua kuwa mada yao ya kunilazimisha nijichanganye na watu siipendi lakini hawachoki kuianzisha wakikaa na mimi, kila siki wananikasirisha na hii mada. Sometimes wanazidi hadi nawajibu vibaya kwa hasira, halafu najishtukia kuwa nimekosea kuwajibu hivyo. Naonekana sina maadili ila ukweli ni kwamba wao ndio wananikasirisha

Hata sasahivi naandika hivi ila wametoka kuniita na kuniambia nikae sebuleni. Nimekaa nao dakika chache tu nikanyanyuka nimerudi zangu chumbani, sijisikii vyema kukaa na watu wengi.

Natamani muda wa chuo ufike niende chuo maana maeneo kama shuleni watu hawaniulizi sana kwa nini najitenga. Muda mwingi hawaongei na mimi na hivyo ndio nilikuwa najisikia amani
Kwani upi ni uamuzi wa busara?

Nifuate furaha yangu, niendelee kukaa peke yangu.. au

Nijichanganye na watu kufurahisha wazazi, wakati mimi moyoni sipendi?
Waambie ukweli tu.Kwamba, umeanza mafunzo ya kuwa mchawi mahiri nchini.
 
Kwa Dunia ya sasa unamtafutia mama Ako pressure dogo Fanya wasemacho

(a) Wazazi wako washaingia na hofu kupata wajukuu mbeleni(lazima wanajua unapiga puri huko ndani-mana pangekuwa na bint wakazi kidogo ingewapa haueni)

(b)ukiendelea kujifungia ushoga unakuandama dogo changamka ujifunze sasa changamana
 
Too late, nilisoma uboizini. Nimekula nyeto sana, hadi nikapoteza hisia na mademu.
Nimekaa nalo moyoni nimeshindwa nikamwambia mzee wangu kwamba siku hizi erection zangu hazipo vizuri kwa sababu ya masturbation. Ikabidi tutafute dawa, nikapata Ginsomin ambazo dokta alisema zitarudisha erection yangu vizuri
Well, hazijafanya kazi hizo dawa, so now nasubiria niende University maana huku nilipo hospitali kubwa kubwa hakuna. Nataka nikienda kusoma chuo kwenye mji mkubwa nitaenda hospitali kubwa. Maybe nitakutana na wataalamu wa kunisaidia

Ila suala la nyeto halihusiani kabisa na mimi kutojichanganya. Nimeanza kuacha kujichanganya kabla hata sijaijua nyeto
Basi wazazi wako wako sahihi kabisa na kukuambia ujichanganye. Maisha hayako hivyo, kijana mdogo unaishi kizee mpaka una athirika na nyeto, ona sasa hata erection imegoma. Hebu jichanganye mtaa uone watoto wazuri kama hukupona ugoi goi huo.
 
Wazazi wanakusaidia usiwe papai.
 
Kakudanganya ..sema ujachelewa ukifikisha 25 ujatibu tatizo basi ni forever ...mvulana unatakiwa kuanza sex na wasichana ukiwa darasa la 7 au form 1 ukichelewa sana form 2 au 3 zaidi ya hapo mambo yatakuwa mabaya
Sio kweli ebu acha upotoshaji, Dk Slaa ameanza ana miaka mingapi kwenye game ya ndoa?
 
Mimi ni kijana wa kiume miaka 19 nimemaliza form 6 na kuapply chuo nasubiri majibu sasa.

Lakini likizo hii imekuwa chungu kwangu maana wazazi kila siku wananisema tu.

Wananilazimisha nijichanganye na watu halafu binafsi sipendi. Napenda niwe peke yangu na muda mwingi nipo chumbani kwangu

Nakereka sana, wazazi wakirudi toka kazini wakifika tu nyumbani kitu cha kwanza ni kuniita na kunilazimisha kukaa sebuleni na familia. Mara nyingi hata nikikaa sebuleni wananiona nimekaa sina furaha, wanaanza kuniuluza mbona huongei? Mimi sina cha kuwajibu sijui sababu, wao wanalalamika kwa sababu wanadai zamani sikuwa hivi.

Kuna maneno yao wanaongea sometimes yananiumiza, mfano wananiongelea wanasema "Huyu mtoto sijui tumfanyeje, tumetumia kila mbinu tumeshindwa. Hivi maisha yako baadaye utaishije ikiwa hujichanganyi na watu?". Wakiniambia hivi huwa nakaa tu kimya ila moyoni huwa nawajibu "kwa nini mnawaza kuhusu maisha yangu ya mbeleni, si mniache tu nitajua mwenyewe"

Licha ya wao kujua kuwa mada yao ya kunilazimisha nijichanganye na watu siipendi lakini hawachoki kuianzisha wakikaa na mimi, kila siki wananikasirisha na hii mada. Sometimes wanazidi hadi nawajibu vibaya kwa hasira, halafu najishtukia kuwa nimekosea kuwajibu hivyo. Naonekana sina maadili ila ukweli ni kwamba wao ndio wananikasirisha

Hata sasahivi naandika hivi ila wametoka kuniita na kuniambia nikae sebuleni. Nimekaa nao dakika chache tu nikanyanyuka nimerudi zangu chumbani, sijisikii vyema kukaa na watu wengi.

Natamani muda wa chuo ufike niende chuo maana maeneo kama shuleni watu hawaniulizi sana kwa nini najitenga. Muda mwingi hawaongei na mimi na hivyo ndio nilikuwa najisikia amani
Kwani upi ni uamuzi wa busara?

Nifuate furaha yangu, niendelee kukaa peke yangu.. au

Nijichanganye na watu kufurahisha wazazi, wakati mimi moyoni sipendi?
Siku ukifiwa na mzazi wako utaelewa faida ya kujichanganya na watu.
 
Ongea na watu uvae viatu mkuu
Kwa umri wako unaweza kuona sawa lkn miaka ya mbele huko, jichanganye. Unakaa kaa ndani unafanya huko nini? Angalia usije kupata msongo wa mawazo ukajidhuru
 
Too late, nilisoma uboizini. Nimekula nyeto sana, hadi nikapoteza hisia na mademu.
Nimekaa nalo moyoni nimeshindwa nikamwambia mzee wangu kwamba siku hizi erection zangu hazipo vizuri kwa sababu ya masturbation. Ikabidi tutafute dawa, nikapata Ginsomin ambazo dokta alisema zitarudisha erection yangu vizuri
Well, hazijafanya kazi hizo dawa, so now nasubiria niende University maana huku nilipo hospitali kubwa kubwa hakuna. Nataka nikienda kusoma chuo kwenye mji mkubwa nitaenda hospitali kubwa. Maybe nitakutana na wataalamu wa kunisaidia

Ila suala la nyeto halihusiani kabisa na mimi kutojichanganya. Nimeanza kuacha kujichanganya kabla hata sijaijua nyeto
Mabosi wengi vibamia,Nyeto
 
Hama hapo kwa wazazi, ukiwa unaishi mwenyewe hakuna wa kukupangia huishi vipi
Hii kitu imenifanya niamue kuondoka nyumbani ili kadri navyopata changamoto ndivyo nitazoeana na watu na kutojitenga. Maana sitokubali kujitenga/kutojichanganya, endapo kama sitakuwa na wakunitafutia. Mimi pia ni 19yrs lakin sio mwanafunzi kama yeye, avumilie akishahitim ndio aondoke. Hata mimi ningelikuwa mwanafunzi nisingeamua hayo.
 
Mimi kukaa ndani nina tuzo,,

Maybe unaweza kuwa ndani na sio mchangamfu,, mimi ni mchangamfu ikiwa nimekuzoea au Kuna sababu ya kukuchangamkia,

Ila jikite kuchangamana na watu ndo vzr,,
 
Back
Top Bottom