Mkuu
MKATA KIU
Kwanza kabisa andiko hili ni zuri, ila huenda kuna kitu kidogo naona hakipo sawa.
Umezungumzia kipindi wazee wetu walikuwa wakiwaachia urithi watoto wao na kipindi cha sasahiv wazazi wetu wakitupa elimu.
Mosi, unaongelea vipindi tofauti hapa,kipindi hicho wazee wa wazee wetu hata elimu ilikuwa ni jambo gumu, hivyo mtoto anakuwa katika kusimamia mali za mzee wake.mfano kuchunga ngo’mbe na mashamba, kijana tangu akiwa mdogo mpaka anakuwa mkubwa anafundishwa ni namna gani ya kusimamia mali ya kwao.
Hivi sasa ni kipindi cha teknolojia tunapatiwa elimu mbadala wa yale yaliyofanyika miaka ile. Elimu ina upana wake, kuna watu wanasomea injinia, ufundi wa magari, majengo, udereva na vitu vingi.
Kama mtu yupo na ujuzi fulani kutokana na elimu tayari ni urithi huo.
Lakini mifumo mibovu ya elimu ya sasa inatengeneza “entitlements mentality” hasa kwa sisi vijana.
Tukitegemea kwamba tutapomaliza shule tutapata favor ya kuwa sehemu fulani sababu ya elimu yetu.
Huwezi kumfananisha kijana aliyeshinda home tangu mdogo akisimamia ngo’mbe na kukosa elimu na aliyeshinda darasani hajui hata ngo’mbe anachungwa vipi.
Elimu ni urithi.