Wazazi wazembe wanatoa Elimu kama Urithi, Sheria ya Mirathi inakataa Elimu sio Urithi, Biblia inataka baba kuacha Urithi

tunaanza na mistari ya biblia

Mithali 13:2 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi​

Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana”

NIMEGUNDUA WAZAZI WA ZAMANI WASIOENDA SHULE WANA AKILI KULIKO WAZAZI WA KISASA.

Elimu ya Mzungu imezalisha wazazi wajinga kuliko wazee ambao hawajapata hiyo elimu.

Wazee wa zamani hawakuwa na elimu ila walikuwa na akili sana. Walikuwa wanaandaa ajira za watoto wao.

Walijua mahitaji ya msingi ya binadamu ni nini chakula, Mavazi na malazi.

Baba ilikuwa wajibu wake kuhakikisha kizazi chake kinapata uhakika wa chakula, mavazi na maradhi kwa wakati.

Kijana akifikisha miaka 18 baba yake alikuwa anampa shamba, mifugo na malazi. Kisha anamuozesha.

Hapo maana yake ajira ameshampatia mwanae kwenye hilo shamba na mifugo

Wazazi wa siku hizi mtoto wa miaka 25 hapewi chochote kwa kisingizio amepewa elimu. Na elimu ndio urithi.

Ukweli elimu sio urithi. Hakuna sheria ya mirathi inayotambua elimu kama urithi.

Wazazi wa zama hizi Wanajifanya wanapenda dini ila mafundisho ya dini kuhusu urithi wanayakataa. Biblia inasema Nyumba na mali mtu atapewa na baba yake. Hakuna walipo sema elimu ndio urithi

Wazazi wengi siku hizi wanatumia asilimia kubwa ya vipato vyao kusomesha watoto wao, ila wanasahau wajibu wao wa kidini hasa Wakristo kuwarithisha mali hao watoto wao.

Watoto wengi wamesoma, wamemaliza vyuo vikuu ila hawajapata ajira. Wanashinda wanazurura tu na kulala nyumbani kutwa nzima. Sababu baba hana rasilimali za kumpa mtaji. Ama baba amefariki hajamuachia urithi wa mali, sababu kuu ameshapewa urithi wa elimu.

Elimu ni basic need kama kumpa mtoto chakula, Hivi unaweza wapa watoto chakula ati ndio useme Urithi,
Elimu ni basic need Kwa mtu inayomsaidia kutumia Rasilimali. Mzazi unapaswa uache Urithi WA rasilimali ambazo mtoto atazitumia kuendesha maisha yake baada ya kupewa elimu. Elimu bila Rasilimali ni Sawa na mdomo pasipo Meno.

Baba yake Mo dewji kamsomesha Mo dewji IST na chuo kikuu kikubwa duniani.. ila bado akaja kumpa urithi wa mali yaani kampuni ya Mohammed Enterprises

Tatizo la Ajira linaletwa na Wazazi wahuni.

Hujamrithisha mtoto Mali ataachaje kukosa Ajira?

Maisha ni yaleyale Ila binadamu ndio wanajifanya yaonekane yamebadilika

Kwa maoni yako je elimu ni urithi wa kuwekewa nguvu kuliko urithi wa mali ?
Wewe tafuta mali zako, acha kulia kulia
 
Kama nchi gani ya Ulaya ambayo haina hayo mambo. Isijekuwa unaangalia tamthilia ndio unaiita Ulaya
Nimeishi sweden na uk .hakuna mambo ya kurithi ila baba anakupa mtaji unasepa.mfano trump baba yake alikuwa tilionaire lakini alimpa bil 2 tu akaanze maisha .mali unajitafutia mali ya baba yako ni ya yeye kula bata na mama yako na mademu zake
 
Mkuu,

Katika mfano wako huu sasa.

Kwanza mo dewji amekulia katika familia ya biashara hivyo practical anaelewa nini anafanya.

Ndicho wanachofanya sasahiv makabila ya wakinga iringa, pia watoto wa wahindi na wachaga.

tatizo si kuacha mali, Tatizo ni jinsi ya kuzisimamia mali.

Mtoto hana basic yoyote kuhusu usimamizi wa mali Halafu baba anaacha mali within 2years unamkuta yupo kijiweni anacheza bao na mali zote kashapoteza.

Tena wapo wengi tumeona tunakua wanashinda kwenye mageti na mbwa wakali lakini wazazi wanapoondoka vyote vinapotea.

Elimu ni urithi hili haliwezi kupingwa.

Nimeishi sweden na uk .hakuna mambo ya kurithi ila baba anakupa mtaji unasepa.mfano trump baba yake alikuwa tilionaire lakini alimpa bil 2 tu akaanze maisha .mali unajitafutia mali ya baba yako ni ya yeye kula bata na mama yako na mademu zake

acha uongo. bilioni mbili alikopeshwa kipindi baba yake yupo na hakudaiwa alipe. Na pia baada ya kufariki Mali za baba yake zote waliachiwa urithi Trump na ndugu zake wengine
 
Kuna familia moja baba alikuwa fundi cherehani na mama anauza genge walikuwa wanaishi gongolamboto miaka ya 1980s. Walikuwa wanaishi nyumba ya kawaida sana ndogo kiasi kwamba watoto walikuwa wanalala sebuleni. Na sisi tulivyokuwa tunaenda kuwatembelea kutoka kijijini tulikuwa tunalazwa sebuleni tena kwenye mkeka asubuhi sana mnaamka! Huyo mzee alikuwa mkali kuwaamsha watoto kwenda shule! Alikomaa nao hao watoto kwa shule za serikali mpaka wote wakapata shahada na wengine wakabakizwa chuo kuwa lecturer! Sasa hivi hiyo familia ni tajili kwasababu watoto waliwahamisha wazazi wao na kuwajengea mjengo huko tegeta eneo kubwa! I salute elimu! Shikamoo elimu! Masikiniwanalishwa uongo kuwa elimu sio kitu! Waache watakuwa walinzi kwenye magate ya walioshiba!

WhatsApp Image 2024-02-08 at 12.40.41.jpeg
 
Huu uzi bora zaidi kwa 2024. Wazazi waache kujificha kwenye kichaka cha "elimu ni urithi"... mtoto anatakiwa arithishwe mali na vitega uchumi. Tuache longolongo ya kusema elimu ni urithi. Ubaya ni kwamba siku hizi watoto ndo wanawarithisha wazazi. Mtoto akishapata ajira anajitokeza mshenzi mmoja kwa jina la mzazi na kuanza kutaka mwanae amtunze ikiwemo kumjengea nyumba wakati yeye ndo alitakiwa kumpa nyumba mwanae.
 
umesema ukweli Moja ya haki kubwa ya mtoto ni kupata urithi wa mali kutoka kwa mzazi wake. Ikiwa umemrithisisha lugha, vyakula, miiko, mavazi, dini na mengineyo. Kwa nini utoe udhuru kwenye ishu ya kumrithisha mtoto Mali ambayo ni haki yake ya msingi.
 
Umesahau kitu kimoja... wazazi wengi wanarithisha watoto roho za upigaji makazini. Yaani vijana wakiingia kazini wanachowaza ni upigaji. Watoto wengi kutoka familia maskini huambiwa na wazazi wao wasome kwa bidii waje wapate kazi sehemu zenye marupurupu (upigaji). Hata kama kijana hana roho ya wizi hujikuta analazimika baada ya wazazi kuanza kumrushia maneno kuwa ni mzembe mbona mtoto wa fulani kaanza kazi juzi tu sasa hivi kashajengea wazazi wake? Kama hana bahati ndo hujikuta mara baada ya kuanza upigaji hukamatwa na kupelekwa mahakamani huku akifukuzwa kazi. Enzi za JPM vijana wengi sana waliingia matatizoni kwa kuponzwa na wazazi wao.
 
acha uongo. bilioni mbili alikopeshwa kipindi baba yake yupo hai miaka . ila baada ya kufariki Mali za baba yake zote waliachiwa urithi Trump na ndugu zake wengine
Yaan urith ni akifa .mi nlijua slimpa umeona sasa unakopeshwa hakuna kuenjoy hela za baba kasake zako.bill gates kasema akifa 95 per ya mali zitolewe msisaada.warren buffet pia yaani hawana mambo ya kuachia mtu urithi ale bata atafute zake
 
deni lenyewe hakulipa. nenda kafanye research, alipewa kwa kuambiwa nakukopesha. ila hakudaiwa
 
Unaniunga basi mkono yaan tilionaire hata bil 2 mwanae nae anamkopesha yaan wazungu wanachukia kurithisha .watoto unawawezesha wajitafutie ikiwemo kuwakopesha
 
Mkuu MKATA KIU

Kwanza kabisa andiko hili ni zuri, ila huenda kuna kitu kidogo naona hakipo sawa.

Umezungumzia kipindi wazee wetu walikuwa wakiwaachia urithi watoto wao na kipindi cha sasahiv wazazi wetu wakitupa elimu.

Mosi, unaongelea vipindi tofauti hapa,kipindi hicho wazee wa wazee wetu hata elimu ilikuwa ni jambo gumu, hivyo mtoto anakuwa katika kusimamia mali za mzee wake.mfano kuchunga ngo’mbe na mashamba, kijana tangu akiwa mdogo mpaka anakuwa mkubwa anafundishwa ni namna gani ya kusimamia mali ya kwao.

Hivi sasa ni kipindi cha teknolojia tunapatiwa elimu mbadala wa yale yaliyofanyika miaka ile. Elimu ina upana wake, kuna watu wanasomea injinia, ufundi wa magari, majengo, udereva na vitu vingi.

Kama mtu yupo na ujuzi fulani kutokana na elimu tayari ni urithi huo.
Lakini mifumo mibovu ya elimu ya sasa inatengeneza “entitlements mentality” hasa kwa sisi vijana.

Tukitegemea kwamba tutapomaliza shule tutapata favor ya kuwa sehemu fulani sababu ya elimu yetu.

Huwezi kumfananisha kijana aliyeshinda home tangu mdogo akisimamia ngo’mbe na kukosa elimu na aliyeshinda darasani hajui hata ngo’mbe anachungwa vipi.

Elimu ni urithi.
Elimu siyo urithi

Sheria ipi ya Tanzania imetamka elimu ni urithi?

Mpeleke shule mwanao lakini usifikiri ndiyo urithi

Kuna jamaa wanateseka mitaani lakini ukiuliza unaambiwa baba yake ana nyumba tano hapa mjini lakini hawezi kumpa mwanae hata moja tu kwa madai kwamba alimsomesha shule!!
 
Uko sahihi; najaribu kufikiria cheti changu cha u-profesa nimrithishe sijui bibi yangu? Alafu mbaya zaidi ata kwenye kesi za mirathi hakuna anayekigombania.
 
Kuna familia moja baba alikuwa fundi cherehani na mama anauza genge walikuwa wanaishi gongolamboto miaka ya 1980s. Walikuwa wanaishi nyumba ya kawaida sana ndogo kiasi kwamba watoto walikuwa wanalala sebuleni. Na sisi tulivyokuwa tunaenda kuwatembelea kutoka kijijini tulikuwa tunalazwa sebuleni tena kwenye mkeka asubuhi sana mnaamka! Huyo mzee alikuwa mkali kuwaamsha watoto kwenda shule! Alikomaa nao hao watoto kwa shule za serikali mpaka wote wakapata shahada na wengine wakabakizwa chuo kuwa lecturer! Sasa hivi hiyo familia ni tajili kwasababu watoto waliwahamisha wazazi wao na kuwajengea mjengo huko tegeta eneo kubwa! I salute elimu! Shikamoo elimu! Masikiniwanalishwa uongo kuwa elimu sio kitu! Waache watakuwa walinzi kwenye magate ya walioshiba!
Sasa hivi kila mmoja anasomesha, na ajira hakuna; hapo unasemaje? Lengo kuu la masikini kusomesha, ni mtoto aje aajiriwe na si kujiajiri kwa sababu wazazi wake walishindwa kujisimamia na kujenga kiwanda n.k
 
Haya sasa! Hayp mashamba makubwa ya kuwakatia watoto wakalime bado yapo? Hata kama yapo bado yanarutuba ya kuotesha na kuzalisha chakula cha kushiba? Bado elimu ndo urithi mbadala wa mashamba! Ukimpa elimu atasoma na kuelewa ulimwengu wa sasa na kama anajitambua atajitafuta nakujipata!
Elimu haiwezi kuwa urithi, bali elimu ni nyenzo itakayokuwezesha kuuendeleza urithi......ndo maana elimu inapatikana kwa jitihada binafsi za muhusika kwenda shule na kupata maarifa na kamwe hairithiwi.​
 
View attachment 2897775

tunaanza na mistari ya biblia

Mithali 13:2 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi​

Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na
Bwan
a”

NIMEGUNDUA WAZAZI WA ZAMANI WASIOENDA SHULE WANA AKILI KULIKO WAZAZI WA KISASA.

Elimu ya Mzungu imezalisha wazazi wajinga kuliko wazee ambao hawajapata hiyo elimu.

Wazee wa zamani hawakuwa na elimu ila walikuwa na akili sana. Walikuwa wanaandaa ajira za watoto wao.

Walijua mahitaji ya msingi ya binadamu ni nini chakula, Mavazi na malazi.

Baba ilikuwa wajibu wake kuhakikisha kizazi chake kinapata uhakika wa chakula, mavazi na maradhi kwa wakati.

Kijana akifikisha miaka 18 baba yake alikuwa anampa shamba, mifugo na malazi. Kisha anamuozesha.

Hapo maana yake ajira ameshampatia mwanae kwenye hilo shamba na mifugo

Wazazi wa siku hizi mtoto wa miaka 25 hapewi chochote kwa kisingizio amepewa elimu. Na elimu ndio urithi.

Ukweli elimu sio urithi. Hakuna sheria ya mirathi inayotambua elimu kama urithi.

Wazazi wa zama hizi Wanajifanya wanapenda dini ila mafundisho ya dini kuhusu urithi wanayakataa. Biblia inasema Nyumba na mali mtu atapewa na baba yake. Hakuna walipo sema elimu ndio urithi

Wazazi wengi siku hizi wanatumia asilimia kubwa ya vipato vyao kusomesha watoto wao, ila wanasahau wajibu wao wa kidini hasa Wakristo kuwarithisha mali hao watoto wao.

Watoto wengi wamesoma, wamemaliza vyuo vikuu ila hawajapata ajira. Wanashinda wanazurura tu na kulala nyumbani kutwa nzima. Sababu baba hana rasilimali za kumpa mtaji. Ama baba amefariki hajamuachia urithi wa mali, sababu kuu ameshapewa urithi wa elimu.

Elimu ni basic need kama kumpa mtoto chakula, Hivi unaweza wapa watoto chakula ati ndio useme Urithi,
Elimu ni basic need Kwa mtu inayomsaidia kutumia Rasilimali. Mzazi unapaswa uache Urithi WA rasilimali ambazo mtoto atazitumia kuendesha maisha yake baada ya kupewa elimu. Elimu bila Rasilimali ni Sawa na mdomo pasipo Meno.

Baba yake Mo dewji kamsomesha Mo dewji IST na chuo kikuu kikubwa duniani.. ila bado akaja kumpa urithi wa mali yaani kampuni ya Mohammed Enterprises

Tatizo la Ajira linaletwa na Wazazi wahuni.

Hujamrithisha mtoto Mali ataachaje kukosa Ajira?

Maisha ni yaleyale Ila binadamu ndio wanajifanya yaonekane yamebadilika

Kwa maoni yako je elimu ni urithi wa kuwekewa nguvu kuliko urithi wa mali ?
Urithi katika agano jipya pia unaonesha uko tofauti, je umesoma hii:m toka kwa Yesu mwenyewe?

‭‭Lk‬ ‭12:13‭-‬15‬ ‭SUV‬‬
[13] Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu. [14] Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu? [15] Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
 
Familia zote zenye nguvu ya kiuchumi Duniani zinarithisha mali kwa vizazi vyao.

Mfano wa familia zenye mafanikio zaidi ni hizi
Bajaj family ( bajaj tunazozipanda )
The Rothschild family(bankers)
Bush family(politicians)
Sinclair(nobles)
Toyoda family (Toyota)
Lee family(Samsung)
Waltons family
Mars family
Al Saud family
Ambani family
Koch family
Hizo familia zote zimefika hapo zilipo kwa kurithishana mali, kurithi ni suala na uumbaji na muendelezo wa maisha ya binadamu na urthi pekee ulio halali ni ule mtoto kurithi kwa mzazi wake (BABA).
 
Back
Top Bottom