Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,042
- 17,320
Sijui hata mada yako unaielewa! Kwaeli!sio kweli TRUMP mwenyewe karithi mali za baba yake
ulaya wana richest family nyingi sana ambazo zimerithi mali za wazazi wao, mfano glazers family wamiliki wa manchester united.
Mbona unajitekenya na kucheka? Si umeongelea urithi kiafrica Africa? Waafrica wanazaa watoto wengi bila kujari rasilimali za kuwakuza! Bado elimu ndo mkombozi na mbadala!
Tusitoke nje ya madaMlee mtoto katika njia nzuri na ipasayo
Mpe elimu kama haki yake ya msingi
Mfundishe kupambana/ kujitegemea katika kujitafutia mali zake asitegemee urithi tu
cc Smart911
Sijui hata mada yako unaielewa! Kwaeli!
Kwamba hujui kwamba kuna ardhi yenye rutuba Tanzania?Haya sasa! Hayp mashamba makubwa ya kuwakatia watoto wakalime bado yapo? Hata kama yapo bado yanarutuba ya kuotesha na kuzalisha chakula cha kushiba? Bado elimu ndo urithi mbadala wa mashamba! Ukimpa elimu atasoma na kuelewa ulimwengu wa sasa na kama anajitambua atajitafuta nakujipata!
Kwanini uzae watoto 7 ambao huna uwezo wa kuwawezesha?Una kajumba kako ka vyumba viwili na kaeneo ka kuotesha mazao kadhaa au mboga mboga! Umezaa watoto 7! Haya! Nipe mchanganuo wa jinsi ya kugawanya urithi!
Mkuu MKATA KIU
Kwanza kabisa andiko hili ni zuri, ila huenda kuna kitu kidogo naona hakipo sawa.
Umezungumzia kipindi wazee wetu walikuwa wakiwaachia urithi watoto wao na kipindi cha sasahiv wazazi wetu wakitupa elimu.
Mosi, unaongelea vipindi tofauti hapa,kipindi hicho wazee wa wazee wetu hata elimu ilikuwa ni jambo gumu, hivyo mtoto anakuwa katika kusimamia mali za mzee wake.mfano kuchunga ngo’mbe na mashamba, kijana tangu akiwa mdogo mpaka anakuwa mkubwa anafundishwa ni namna gani ya kusimamia mali ya kwao.
Hivi sasa ni kipindi cha teknolojia tunapatiwa elimu mbadala wa yale yaliyofanyika miaka ile. Elimu ina upana wake, kuna watu wanasomea injinia, ufundi wa magari, majengo, udereva na vitu vingi.
Kama mtu yupo na ujuzi fulani kutokana na elimu tayari ni urithi huo.
Lakini mifumo mibovu ya elimu ya sasa inatengeneza “entitlements mentality” hasa kwa sisi vijana.
Tukitegemea kwamba tutapomaliza shule tutapata favor ya kuwa sehemu fulani sababu ya elimu yetu.
Huwezi kumfananisha kijana aliyeshinda home tangu mdogo akisimamia ngo’mbe na kukosa elimu na aliyeshinda darasani hajui hata ngo’mbe anachungwa vipi.
Elimu ni urithi.
Hapo mwisho nimesema vizuri kwamba asitegemee urithi tu mrithishe mali/ vitu pia muelekeze kupambana utamsaidia sana!Tusitoke nje ya mada
Swala la kumfundisha mtoto kupambana au kutegemea urithi is UP TO YOU kama mzazi, Point ni wazazi wanatakiwa kuwatengezea watoto mifumo ya kurithi kitu cha kuendelea kuzalisha fedha au mali si kutoa sababu za kusema ELIMU NDIO URITHI...naona wenzetu kama waarabu wamefanikiwa katika hilo.
Rejea kitabu cha Mwanzo Katika biblia Yule mtoto alieomba urithi kwa babake akaenda kutumia mali ovyo kisha alirejea...ALIOMBA URITHI KWA BABA YAKE KAMA HAKI YAKE NA AKAPEWA.
Mkuu,Baba yake Mo dewji kamsomesha Mo dewji IST na chuo kikuu kikubwa duniani.. ila bado akaja kumpa urithi wa mali yaani kampuni ya Mohammed Enterprises
Unauza figo unawapa mgaoUna kajumba kako ka vyumba viwili na kaeneo ka kuotesha mazao kadhaa au mboga mboga! Umezaa watoto 7! Haya! Nipe mchanganuo wa jinsi ya kugawanya urithi!
🤣🤣🤣🤣Nimesikia love, urithi watajitafutia wenyewe, sisi kazi yetu kuwapeleka shule..
Haya mambo ya urithi sijui blahbkah yako Africa! Ulaya mtoto akifikisha miaka 18 anatakiwa atoke kwa wazazi akapambane! Labda wazazi wakifariki ndo hayo mambo ya next of kin na urithi yanakuja! Mtoto anatakiwa umpe elimu ya kujitambua na kupambana!