Wazazi wazembe wanatoa Elimu kama Urithi, Sheria ya Mirathi inakataa Elimu sio Urithi, Biblia inataka baba kuacha Urithi

Wewe tafuta mali zako, acha kulia kulia
 
Kama nchi gani ya Ulaya ambayo haina hayo mambo. Isijekuwa unaangalia tamthilia ndio unaiita Ulaya
Nimeishi sweden na uk .hakuna mambo ya kurithi ila baba anakupa mtaji unasepa.mfano trump baba yake alikuwa tilionaire lakini alimpa bil 2 tu akaanze maisha .mali unajitafutia mali ya baba yako ni ya yeye kula bata na mama yako na mademu zake
 

Nimeishi sweden na uk .hakuna mambo ya kurithi ila baba anakupa mtaji unasepa.mfano trump baba yake alikuwa tilionaire lakini alimpa bil 2 tu akaanze maisha .mali unajitafutia mali ya baba yako ni ya yeye kula bata na mama yako na mademu zake

acha uongo. bilioni mbili alikopeshwa kipindi baba yake yupo na hakudaiwa alipe. Na pia baada ya kufariki Mali za baba yake zote waliachiwa urithi Trump na ndugu zake wengine
 

 
Huu uzi bora zaidi kwa 2024. Wazazi waache kujificha kwenye kichaka cha "elimu ni urithi"... mtoto anatakiwa arithishwe mali na vitega uchumi. Tuache longolongo ya kusema elimu ni urithi. Ubaya ni kwamba siku hizi watoto ndo wanawarithisha wazazi. Mtoto akishapata ajira anajitokeza mshenzi mmoja kwa jina la mzazi na kuanza kutaka mwanae amtunze ikiwemo kumjengea nyumba wakati yeye ndo alitakiwa kumpa nyumba mwanae.
 

umesema ukweli Moja ya haki kubwa ya mtoto ni kupata urithi wa mali kutoka kwa mzazi wake. Ikiwa umemrithisisha lugha, vyakula, miiko, mavazi, dini na mengineyo. Kwa nini utoe udhuru kwenye ishu ya kumrithisha mtoto Mali ambayo ni haki yake ya msingi.
 
Umesahau kitu kimoja... wazazi wengi wanarithisha watoto roho za upigaji makazini. Yaani vijana wakiingia kazini wanachowaza ni upigaji. Watoto wengi kutoka familia maskini huambiwa na wazazi wao wasome kwa bidii waje wapate kazi sehemu zenye marupurupu (upigaji). Hata kama kijana hana roho ya wizi hujikuta analazimika baada ya wazazi kuanza kumrushia maneno kuwa ni mzembe mbona mtoto wa fulani kaanza kazi juzi tu sasa hivi kashajengea wazazi wake? Kama hana bahati ndo hujikuta mara baada ya kuanza upigaji hukamatwa na kupelekwa mahakamani huku akifukuzwa kazi. Enzi za JPM vijana wengi sana waliingia matatizoni kwa kuponzwa na wazazi wao.
 
acha uongo. bilioni mbili alikopeshwa kipindi baba yake yupo hai miaka . ila baada ya kufariki Mali za baba yake zote waliachiwa urithi Trump na ndugu zake wengine
Yaan urith ni akifa .mi nlijua slimpa umeona sasa unakopeshwa hakuna kuenjoy hela za baba kasake zako.bill gates kasema akifa 95 per ya mali zitolewe msisaada.warren buffet pia yaani hawana mambo ya kuachia mtu urithi ale bata atafute zake
 
Yaan urith ni akifa .mi nlijua slimpa umeona sasa unakopeshwa hakuna kuenjoy hela za baba kasake zako.bill gates kasema akifa 95 per ya mali zitolewe msisaada.warren buffet pia yaani hawana mambo ya kuachia mtu urithi ale bata atafute zake

deni lenyewe hakulipa. nenda kafanye research, alipewa kwa kuambiwa nakukopesha. ila hakudaiwa
 
deni lenyewe hakulipa. nenda kafanye research, alipewa kwa kuambiwa nakukopesha. ila hakudaiwa
Unaniunga basi mkono yaan tilionaire hata bil 2 mwanae nae anamkopesha yaan wazungu wanachukia kurithisha .watoto unawawezesha wajitafutie ikiwemo kuwakopesha
 
Elimu siyo urithi

Sheria ipi ya Tanzania imetamka elimu ni urithi?

Mpeleke shule mwanao lakini usifikiri ndiyo urithi

Kuna jamaa wanateseka mitaani lakini ukiuliza unaambiwa baba yake ana nyumba tano hapa mjini lakini hawezi kumpa mwanae hata moja tu kwa madai kwamba alimsomesha shule!!
 
Uko sahihi; najaribu kufikiria cheti changu cha u-profesa nimrithishe sijui bibi yangu? Alafu mbaya zaidi ata kwenye kesi za mirathi hakuna anayekigombania.
 
Sasa hivi kila mmoja anasomesha, na ajira hakuna; hapo unasemaje? Lengo kuu la masikini kusomesha, ni mtoto aje aajiriwe na si kujiajiri kwa sababu wazazi wake walishindwa kujisimamia na kujenga kiwanda n.k
 
Elimu haiwezi kuwa urithi, bali elimu ni nyenzo itakayokuwezesha kuuendeleza urithi......ndo maana elimu inapatikana kwa jitihada binafsi za muhusika kwenda shule na kupata maarifa na kamwe hairithiwi.​
 
Urithi katika agano jipya pia unaonesha uko tofauti, je umesoma hii:m toka kwa Yesu mwenyewe?

‭‭Lk‬ ‭12:13‭-‬15‬ ‭SUV‬‬
[13] Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu. [14] Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu? [15] Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
 
Familia zote zenye nguvu ya kiuchumi Duniani zinarithisha mali kwa vizazi vyao.

Mfano wa familia zenye mafanikio zaidi ni hizi
Bajaj family ( bajaj tunazozipanda )
The Rothschild family(bankers)
Bush family(politicians)
Sinclair(nobles)
Toyoda family (Toyota)
Lee family(Samsung)
Waltons family
Mars family
Al Saud family
Ambani family
Koch family
Hizo familia zote zimefika hapo zilipo kwa kurithishana mali, kurithi ni suala na uumbaji na muendelezo wa maisha ya binadamu na urthi pekee ulio halali ni ule mtoto kurithi kwa mzazi wake (BABA).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…