Wazazi wazembe wanatoa Elimu kama Urithi, Sheria ya Mirathi inakataa Elimu sio Urithi, Biblia inataka baba kuacha Urithi

Mleta mada uko sahihi sana!


Elimu ni haki ya msingi ya mtoto.

Mtoto hakuja duniani kwa mapenzi yake wala mipango yake.

Mtoto ni matokeo ya kukutana kimwili kati ya huyo baba na mama.

Ni wajibu wa mzazi kuhakikisha anaandaa system ama anaijenga kadiri ya aendeleavyo kwa ajili ya kizazi chake.

Kumnyima mtoto japo mtaji wa kuyaanza maisha rasmi ni ubinafsi wa hali ya juu sana na unyanyasaji kwa watoto ambao hawakuwaomba muwalete hapa duniani.

Watoto wako ni kiwakilishi chako hapa duniani hata baada ya exit yako.

Sasa unamtupaje duniani mwakilishi wako bila kumuandaa na kumpa silaha za kuanzia katika mapambano yake ya Maisha baada ya kumpiga msasa kwa kutumia Elimu?

Watu wazima wengi (hasa wa Afrika) wamekariri mtoto anapaswa kumsujudia mkubwa na wakubwa wamejisahaulisha kuhusu wajibu wao wa kuwaongoza na kuwalinda watoto.

Watu weusi wengi ni wabinafsi sana sana sana!
 

Ushauri kwa mwanaume Miliki mali nyingi mpe mtoto urithi hata kama mwanao akisoma kayumba siku ukifariki litasema baba au mama jembe... ila sasa kosea lipeleke shule za milioni tatu.. limalize shule halafu usilipe mtaji wala nyumba ya urithi.. linasahau ada ulizokuwa unamlipia kila mwaka milioni 3 linaona baba kilaza tu
 
Urithi wa maana nitakao waachia wanangu na kizazi changu ni kutokua wa Tanzania tu.
 
Mlee mtoto katika njia nzuri na ipasayo
Mpe elimu kama haki yake ya msingi
Pamoja na kumrithisha mali pia mfundishe kupambana/ kujitegemea katika kujitafutia mali zake asitegemee urithi tu

cc Smart911

Familia zote zenye nguvu duniani zimepata nguvu ya mali kwa njia ya urithi
 
Wazazi tutafute mali kwa ajili ya watoto wetu
 

Elimu bila pesa na mali inakuwa haina maana
 
Uko sahihi Mkuu nimeshuhudia haya
 
Umeshuhudia nini madam ?
Mzee mmoja alikufa akiwa Na 70+ aliwaachia wanae 100M+ bank nyumba za kupangisha gesti houses Gari Na katika kuishi kwake aliwapa wanae wa kiume mitaji ya Biashara Na kuwapa kiwanja kila mtoto
 
Wakati mwingine elimu inaweza kufubaza akili.
 
naomba nikupe mistari ya biblia

Mithali 13:2 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi;​


Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana”
Lakini Biblia hiyo hiyo...tunaona Yakobo wanae. 12. Hakuwapa mali yeyote zaidi ya kuwatamkia maneno ya baraka.
 
Nafikiri mtoa mada anachanganya hapo, kizazi Cha Sasa Kiko tayari kuua mzazi warithi Mali zake , very sad
Haya mambo ya urithi sijui blahbkah yako Africa! Ulaya mtoto akifikisha miaka 18 anatakiwa atoke kwa wazazi akapambane! Labda wazazi wakifariki ndo hayo mambo ya next of kin na urithi yanakuja! Mtoto anatakiwa umpe elimu ya kujitambua na kupambana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…